
Kichwa: | Kiambatisho cha Viashiria |
Msimbo: | A—SRCL-B-CH |
Toleo: | 1.1 |
Inatumika kwa: | Wamiliki wa Vyeti vya Shamba |
Utekelezaji: | Maudhui ya kuunganisha |
Kuanzia: | Machi 1, 2026 |
Inakamilika ifikapo: | Hadi itakapotangazwa vinginevyo |
Imechapishwa mnamo: | Septemba 17, 2025 |
Imeunganishwa na: | A-1-S-B-F-V1.4 Kiwango cha Kilimo Endelevu cha shirika la Rainforest Alliance. A-33-R-B-FA-V1.0 Kiwango cha Kilimo Rejelevu cha shirika la Rainforest Alliance. |
Inachukua nafasi ya: |
Hati hii inahusu nini?
Kiambatisho hiki kinatoa taarifa za ziada za lazima kuhusu utekelezaji wa sharti la 1.7.1 la Viwango vya Uidhinishaji vya shirika la Rainforest Alliance. Inaainisha viashiria ambavyo Wamiliki wa Vyeti wa Mashamba wanatakiwa kukusanya na kuwasilisha kila mwaka. Isipokuwa pale ambapo imeelezwa vinginevyo, Wamiliki wa Vyeti lazima wakusanye kila mwaka data ya mwaka uliotangulia. Tunachomaanisha hapa ni kwamba data inapaswa kujumuisha kipindi kati ya ukaguzi wa mwisho na ukaguzi wa sasa. Kwa mfano, ikiwa ukaguzi utafanywa Oktoba 2026, kipindi husika cha ukusanyaji wa data kitakuwa kuanzia Oktoba 2025 hadi Septemba 2026. Data hii itapitiwa wakati wa ukaguzi wa Oktoba 2026.
Kwa mashamba yaliyo ndani ya kikundi kinachofanya ukaguzi wa ndani kwa nyakati tofauti mwaka mzima, data iliyokusanywa katika kiwango cha shamba inapaswa kuakisi miezi 12 inayotangulia mwezi wa ukaguzi wa ndani. Kwa mfano, kwa ukaguzi ujao wa Oktoba 2026, taarifa za kiwango cha kikundi zitajumuisha ukaguzi uliopita (Oktoba 2025) hadi tarehe iliyo zaidi na Oktoba 2026. Ikiwa wanachama wa kikundi watakaguliwa ndani ya kikundi mwezi Machi 2026, data husika ya kiwango cha shamba inapaswa kujumuisha kipindi cha kuanzia Aprili 2025 hadi Machi 2026.
Aidha, pale ambapo Wamiliki wa Vyeti wana mazao mengi yaliyoidhinishwa, data inalenga zao lililoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance lenye kiasi kikubwa zaidi cha uzalishaji.
Lini na jinsi ya kutumia hati hii?
Hati hii inawapa Wamiliki wa Vyeti taarifa kuhusu viashiria vinavyotakiwa na Viwango vya shirika la Rainforest Alliance, vinavyohusiana na sharti la 1.7.1 na jinsi ya kukusanya data hiyo kwa njia ifaayo na sahihi. Mashirika ya Uidhinishaji yatarejelea hati hii kwa maelezo zaidi kuhusu utekelezaji wa sharti hilo.
Maudhui yamehifadhiwa katika kiwango cha juu ili kuhakikisha yanapatikana kwa urahisi. Kwa maelezo zaidi, tafadhali rejelea Mwongozo wa shirika la Rainforest Alliance: Vipengelee vya Data na nyaraka nyingine za mwongozo zilizorejelewa. Kwa ufafanuzi wa istilahi, rejelea Kiambatisho cha Kamusi ya Istilahi cha shirika la Rainforest Alliance.
Kiambatisho cha Kiashirio kina sehemu 3 kuu:
Viashiria vya Msingi
Viashiria vya Kilimo Endelevu
Viashiria vya Kilimo Rejelevu
Viashiria vya Msingi vinatumika kwa Viwango vyote. Hata hivyo, seti nyingine ya viashiria zinaweza kupatikana chini ya kila sehemu ya Viwango husika, na hutumika ipasavyo.
Mabadiliko yaliyofanywa katika sasisho kutoka toleo la v1.0 hadi la v1.2
Sehemu | Nini kimebadilika |
Hati hii inahusu nini? | Imerekebishwa: maandishi yaliyosasishwa, mabadiliko na ufafanuzi vimefanywa kuhusu kipindi ambacho data inayokusanywa na Wamiliki wa Vyeti inapaswa kuonekana. |
Wakati na jinsi ya kutumia hati hii | Imerekebishwa: maandishi yameongezwa kueleza mpangilio mpya. |
Utumikaji wa Vipengele vya Data ya Viashiria | Imerekebishwa: ufafanuzi kwenye maandishi. |
Maelezo kuhusu utumikaji wa muda | Imerekebishwa: ufafanuzi umetolewa kuhusu kipindi cha ukusanyaji wa viashiria. |
Viashiria vya Msingi | Mpya: Shirika la Rainforest Alliance limeainisha aina tofauti za viashiria, huku viashiria vya msingi vikitumika kwa viashiria vya viwango vyote. Kumbuka, Viashiria vya msingi sio vipya, vimeainishwa tu kwa namna tofauti sasa. |
Kiwango cha Kilimo Endelevu | Imerekebishwa: mpangilio wa viashiria chini ya kiwango mahususi. |
Viashiria vya Kiwango cha Kilimo Rejelevu | Mpya: Viashiria vya Kiwango cha Kilimo Rejelevu vimeongezwa. |
Viashiria vya Kiwango cha Kilimo Rejelevu | Dokezo kwa Wamiliki wa Vyeti wanaofuata viwango vya Kilimo Endelevu na Kilimo Rejelevu, dokezo limeongezwa chini ya Viashiria vya Kilimo Rejelevu. Dokezo hili linabainisha kuwa kila kiashiria mahususi kinapaswa kuripotiwa mara moja kwa viwango vyote viwili, badala ya kuwasilishwa kando. |
Utumikaji wa Vipengele vya Data ya Viashiria
Utumikaji wa kipengele cha data huonyeshwa kwa alama ya tiki. Kwa ujumla, alama ya tiki huonyesha mhusika au kiwango ambacho data inapaswa kukusanywa kutoka kwake.
Tafadhali kumbuka kuwa kwa vikundi, bila kujali mahali alama ya tiki, usimamizi wa kikundi daima una jukumu la mwisho la kuhakikisha data inakusanywa na kuripotiwa kwenye mfumo wa shirika la Rainforest Alliance. Kwa vikundi, viashiria huripotiwa kila mwaka wakati wa ukaguzi wa ndani/tathmini binafsi. Aidha, kwa vikundi, usimamizi wa kikundi unapaswa kuripoti data kwa mashamba yenye sampuli ya ukusanyaji wa data inayolingana na sampuli ya ukaguzi wa ndani.
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | |||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/ Kubwa | |
Alama ya tiki kwa mashamba madogo na makubwa yaliyo chini ya uidhinishaji wa kibinafsi | ||||
Mashamba madogo au makubwa yaliyoidhinishwa kibinafsi lazima yakusanye vipengele hivi vya data. |
| |||
Alama ya tiki kwa usimamizi wa kikundi | ||||
Kipengele cha data kinatumika kwa kundi zima, na wafanyakazi wa usimamizi wa kundi wanawajibika kukusanya vipengele hivyo vya data kwa niaba ya wanachama wote wa kundi (shamba ndogo na kubwa) pamoja na shughuli zao wenyewe. |
| |||
Alama ya tiki kwa mashamba makubwa yaliyo sehemu ya kikundi | ||||
Usimamizi wa shamba kubwa unawajibika kukusanya vipengele vya data vya shamba lao. Usimamizi wa kikundi lazima ulisaidie shamba kutekeleza jukumu hili na una jukumu la mwisho la kuwasilisha data. |
| |||
Alama ya tiki kwa mashamba madogo yaliyo sehemu ya kikundi | ||||
Kipengele hiki cha data kinatumika kwa mashamba madogo, lakini data hiyo lazima ikusanywe na usimamizi wa kikundi. |
| |||
Alama ya tiki kwa mashamba kubwa yaliyo sehemu ya kikundi na usimamizi wa kikundi | ||||
Usimamizi wa shamba kubwa lazima ukusanye vipengele vya data vya mashamba yao, ilhali usimamizi wa kikundi hushughulikia vipengele vya data vya mashamba madogo yaliyo ndani ya kikundi (ikiwa inafaa) na kusaidia mashamba makubwa yaliyo ndani ya kikundi. |
|
| ||
Alama ya tiki kwa mashamba madogo na makubwa yaliyo sehemu ya kikundi | ||||
Kipengele cha data kinatumika kwa mashamba madogo na makubwa yaliyo ndani ya kikundi, lakini kwa mashamba madogo, data hiyo lazima ikusanywe na uongozi wa kikundi. |
|
| ||
Alama ya tiki kwa mashamba madogo, mashamba makubwa na usimamizi wa kikundi | ||||
Vipengele hivi vya data vinatumika kwa mashamba madogo, mashamba makubwa na usimamizi wa kikundi ndani ya kikundi. |
|
|
| |
Viashiria
Viashiria vya Msingi
Kiasi kinachokadiriwa cha uzalishaji ulioidhinishwa katika mwaka uliotangulia, kwa kilogramu
Maelezo:
Jumla ya kiasi kilichokadiriwa cha mazao yaliyoidhinishwa. Haya ni makadirio yaliyochukuliwa kutoka mwaka uliotangulia.
Kufuatilia makadirio ya awali ya kiasi cha uzalishaji ulioidhinishwa huwasaidia wazalishaji na usimamizi wa kikundi kusimamia vyema mashamba yao, kunahimiza matumizi ya mbinu bora za kilimo na kuimarisha uwazi katika mnyororo wa ugavi. Ni muhimu katika kufuatilia mienendo ya makadirio ya mavuno kwa mwaka wa sasa. Makadirio hayo yanalinganishwa na mavuno halisi. Inachangia kuhakikisha uaminifu wa mpango wa uidhinishaji wa shirika la Rainforest Alliance na mfumo wake wa ufuatiliaji.
Ukusanyaji wa data:
Inakusanywa kama thamani ya nambari
Jumla ya kilogramu za makadirio ya uzalishaji ulioidhinishwa.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
Tafadhali rejelea Mwongozo G wa shirika la Rainforest Alliance: Makadirio ya Mavuno, ambayo yanashughulikia mazao mbalimbali na miktadha tofauti ya uzalishaji. Kanuni za msingi zimefafanuliwa ili kuwezesha makadirio sahihi zaidi ya mavuno.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
| ||
Makadirio ya kiasi cha uzalishaji ulioidhinishwa katika mwaka uliotangulia, kwa idadi ya mashina: Inatumika kwa maua pekee
Maelezo:
Jumla ya kiasi kilichokadiriwa cha mazao yaliyoidhinishwa. Haya ni makadirio yaliyochukuliwa kutoka mwaka uliotangulia.
Kufuatilia makadirio ya awali ya kiasi cha uzalishaji ulioidhinishwa huwasaidia wazalishaji na usimamizi wa kikundi kusimamia vyema mashamba yao, kunahimiza matumizi ya mbinu bora za kilimo na kuimarisha uwazi katika mnyororo wa ugavi. Ni muhimu katika kufuatilia mienendo ya makadirio ya mavuno kwa mwaka wa sasa. Makadirio hayo yanalinganishwa na mavuno halisi. Inachangia kuhakikisha uaminifu wa mpango wa uidhinishaji wa shirika la Rainforest Alliance na mfumo wake wa ufuatiliaji.
Ukusanyaji wa data:
Hukusanywa kama thamani ya nambari.
Jumla ya mashina ya uzalishaji ulioidhinishwa yanayokadiriwa.
Data iliyowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
Tafadhali rejelea Mwongozo G wa shirika la Rainforest Alliance: Makadirio ya Mavuno, ambayo yanashughulikia mazao mbalimbali na miktadha tofauti ya uzalishaji. Kanuni za msingi zimefafanuliwa ili kuwezesha makadirio sahihi zaidi ya mavuno.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
| ||
Ukubwa wa shamba kwa hekta (ha)
Maelezo:
Jumla ya eneo la mashamba yaliyoidhinishwa. Lengo ni kuhakikisha kuwa kumbukumbu za jumla ya eneo lililoidhinishwa zinasasishwa mara kwa mara, kama sehemu ya taarifa zinazohitajika kuthibitisha wigo wa uidhinishaji wa Mmiliki wa Cheti (CH)/kila mwanachama wa kikundi. Katika vikundi, unaweza kutumia fomu ya Rejesta ya Wanachama wa Kikundi (GMR) iliyotolewa na shirika la Rainforest Alliance kukusanya taarifa hizi.
Ukusanyaji wa data:
Imekusanywa kama thamani ya nambari.
Kwa kutumia nyaraka za umiliki/ haki ya umiliki au utumiaji wa ardhi, kama vile hati, mikataba ya ukodishaji, na vyeti vya umiliki, pamoja na ramani za eneo husika, mzalishaji lazima arekodi jumla ya eneo lote litakalojumuishwa katika wigo wa uidhinishaji kwa kutumia fomu zilizotolewa na shirika la Rainforest Alliance (kama vile GMR, jukwaa la shirika la Rainforest Alliance).
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
| ||
Ukubwa wa eneo la uzalishaji kwa hekta (ha)
Maelezo:
Eneo la uzalishaji wa mazao yaliyoidhinishwa. Hifadhi rekodi iliyosasishwa ya eneo linalokuza zao lililoidhinishwa kama sehemu ya taarifa muhimu zinazohitajika kuthibitisha wigo wa uidhinishaji wa Mmliki wa Cheti/kila mwanachama wa kikundi.
Ukusanyaji wa data:
Mwanzoni mwa mwaka, wakati wa kusasisha mpango wa usimamizi wa kila mwaka.
Thibitisha na usasishe mabadiliko yoyote kabla ya ukaguzi wa ndani.
Kwa kutumia nyaraka za umiliki/haki ya umiliki au utumiaji wa ardhi, kama vile hati, mikataba ya ukodishaji na vyeti vya umiliki, pamoja na ramani za eneo husika. Mzalishaji lazima arekodi jumla ya eneo litakalojumuishwa katika ya wigo wa uidhinishaji kwa kutumia fomu zilizotolewa na shirika la Rainforest Alliance (GMR, jukwaa).
Tofauti zozote kati ya nyaraka mbalimbali zinapaswa kutambuliwa na kurekodiwa ili kuhakikisha kuwa data iliyoingizwa katika mifumo ya shirika la Rainforest Alliance inaweza kuhalalishwa kwa kutumia ushahidi wakati wa mchakato wa uhakiki na uidhinishaji unaofanywa na shirika la Rainforest Alliance au Shirika la Uidhinishaji (CB).
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
| ||
Idadi ya visa vilivyoripotiwa vilivyogawanywa kulingana na jinsia, kwa ajili ya: Ajira ya Watoto, Ajira ya Lazima, Ubaguzi wa Kijinsia, Aina nyingine za Ubaguzi, Ukatili na Unyanyasaji Mahali pa Kazi
Maelezo:
Jumla ya idadi ya visa vilivyoripotiwa na kamati ya kushughulikia malalamiko, ikigawanywa kulingana na jinsia na kuanishwa katika makundi yafuatayo: ajira ya watoto, ajira ya lazima, ubaguzi wa kijinsia, aina nyingine za ubaguzi, pamoja na vitendo vya ukatili au unyanyasaji mahali pa kazi.
Ukusanyaji wa data:
Data inayowasilishwa kwenye jukwaa la shirika la Rainforest Alliance ni ya mwaka uliotangulia.
Kwa taarifa zaidi:
Mwongozo wa E wa shirika la Rainforest Alliance: Utaratibu wa kushughulikia malalamiko.
Mwongozo wa R wa shirika la Rainforest Alliance: Zana ya Mwongozo wa Ufuatiliaji wa Tathmini-na Kushughulikia Masuala.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Idadi ya visa vilivyothibitishwa, vilivyogawanywa kulingana na jinsia, kwa ajili ya: Ajira ya Watoto, Ajira ya Lazima, Ubaguzi wa Kijinsia, aina nyingine ya Ubaguzi, Ukatili na Unyanyasaji Mahali pa Kazi.
Maelezo:
Jumla ya idadi ya visa vilivyothibitishwa na kamati ya kushughulikia malalamiko kulingana na jinsia zilizothibitishwa na kamati ya malalamiko, vilivyogawanywa kulingana na jinsia na kuanishiwa katika makundi ya ajira ya watoto, ajira ya kulazimishwa, ubaguzi wa kijinsia, aina nyingine za ubaguzi, na ukatitili au unyanyasaji mahali pa kazi.
Ukusanyaji wa data:
Data inayowasilishwa kwenye jukwaa la shirika la Rainforest Alliance ni ya mwaka uliotangulia.
Kwa taarifa zaidi:
Mwongozo wa E wa shirika la Rainforest Alliance: Utaratibu wa kushughulikia malalamiko.
Kwa kiolezo na zana, rejelea mwongozo R wa shirika la Rainforest Alliance: Zana ya Mwongozo wa Ufuatiliaji wa Tathmini-na Kushughulikia Masuala.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Idadi ya visa vilivyorekebishwa vilivyogawanywa kulingana na jinsia kwa Ajira ya Watoto, Ajira ya Lazima, Ubaguzi wa Kijinsia, Aina nyingine za ubaguzi, Ukatili na Unyanyasaji Mahali pa Kazi
Maelezo:
Jumla ya idadi ya visa vilivyorekebishwa, vilivyogawanywa kulingana na jinsia na kuanishwa katika makundi ya ajira ya watoto, ajira ya lazima, ubaguzi wa kijinsia, aina nyingine za ubaguzi, na ukatili au unyanyasaji mahali pa kazi.
Ukusanyaji wa data:
Data inayowasilishwa kwenye jukwaa la shirika la RA ni ya mwaka uliotangulia.
Kwa taarifa zaidi:
Mwongozo S wa shirika la Rainforest Alliance: Itifaki ya Kushughulikia na Kurekebisha Ukiukaji wa Mahitaji.
Kwa kiolezo na zana, rejelea Mwongozo R wa shirika la Rainforest Alliance Zana ya Mwongozo wa Ufuatiliaji wa Tathmini na Kushughulikia Masuala.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Viashiria vya Kiwango cha Kilimo Endelevu
Kilimo endelevu hakijawahi kuwa muhimu zaidi kuliko sasa. Kiwango cha Kilimo Endelevu kinatoa mfumo wa vitendo na ubunifu mahususi unaolenga kuwasaidia wazalishaji kukuza mazao bora, kuongeza uzalishaji, kupata maarifa muhimu kuhusu shughuli zao katika masuala ya uendelevu, na kuelekeza uwekezaji katika maeneo yenye hatari kubwa zaidi. Viashiria vya Kiwango cha Kilimo Endelevu vimeundwa ili kuwasaidia Wamiliki wa Vyeti kufuatilia maendeleo yao katika kufikia malengo ya uendelevu na kuhakikisha wanapata fursa katika masoko yanayoendelea kubadilika, huku vikiwezesha wafanyabiashara kuwa na uwezo wa kukabiliana na shinikizo linaloongezeka la kutoa taarifa kuhusu athari za shughuli zao kwa kijamii na kimazingira.
Idadi ya Aina za Miti ya Kivuli katika kila shamba
Maelezo:
Jumla ya idadi ya aina za spishi za miti ya kivuli zilizopo shambani.
Hii inalenga kuongeza wingi wa spishi mbalimbali miti ya kivuli katika kila shamba ili kuboresha ubora wa udongo, kuhifadhi bioanuwai, kuimarisha ulinzi wa vyanzo vya maji na kuchangia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia ufyonzaji wa kaboni.
Ukusanyaji wa Data:
Imekusanywa kama thamani ya nambari.
Hesabu idadi ya spishi za miti inayotumika kutoa kivuli katika eneo ambapo zao lililoidhinishwa na RA linakuzwa.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Idadi ya miti ya kivuli kwa hekta
Maelezo:
Jumla ya idadi ya miti ya kivuli iliyopo shambani kwa kila hekta ya eneo ambapo mazao yaliyoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance yanakuzwa. Kiashiria hiki kinalenga kuongeza idadi ya miti ya kivuli katika kila shamba ili kuboresha ubora wa udongo, kuhifadhi bioanuwai, kuimarisha ulinzi wa vyanzo vya maji na kuchangia katika kukabiliana na mabadilika ya tabianchi kupitia ufyonzaji wa kaboni.
Ukusanyaji wa Data:
Imekusanywa kama thamani ya nambari.
Hesabu idadi ya miti ya kivuli kwa kila hekta.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Lita / Kilogramu za Mbolea za Asili
Maelezo:
Kiashiria hiki hufuatilia kiasi cha mbolea za asili kilichotumika kwenye mazao yaliyoidhinishwa shambani katika kipindi cha mwaka uliopita. Lengo ni kutumia data hii kubainisha na kutekeleza hatua za kuboresha ufanisi wa matumizi ya mbolea katika mwaka unaofuatia. Kwa kipengele hiki cha data, shirika la Rainforest Alliance limefafanua mbolea ya asili kulingana na ufafanuzi uliotolewa katika faharasa ya istilahi. Hii inazingatia tu mbolea zinazopatikana kutoka vyanzo vya kibiashara na haijumuishi samadi.
Ukusanyaji wa Data:
Inakusanywa kama thamani ya nambari inayoripotiwa kwa kilogramu (kg) na/au lita (L).
Jumla ya kiasi cha mbolea ya asili kilichotumiwa shambani kwenye zao kuu lililoidhinishwa na shirika la RA.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Lita / Kilogramu za Mbolea za Kemikali
Maelezo:
Kufuatilia matumizi ya kila mwaka ya mbolea za kemikali shambani kwa ajili ya zao lililoidhinishwa katika kipindi cha mwaka uliopita. Data hii hutumika kutambua mapema na kutekeleza fursa za kuboresha ufanisi wa matumizi ya mbolea katika mwaka unaofuatia.
Ukusanyaji wa Data:
Imekusanywa kama thamani ya nambari.
Jumla ya kiasi cha mbolea ya kemikali kilichotumika kwenye zao kuu lililoidhinishwa na shirika la RA.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Lita / Kilogramu za Viuatilifu, zilizogawanywa katika makundi yafuatayo; Viua-dudu, Viua- panya, Viua-kuvu, Viua-magugu, na Vinginevyo
Maelezo:
Jumla ya kiasi cha viuatilifu vyote vilivyotumika shambani katika mwaka uliotangulia.
Lengo ni kuhakikisha matumizi ya mbinu endelevu za kudhibiti visumbufu kwa kufuatilia kwa usahihi matumizi ya viuatilifu kila mwaka, kuhimiza matumizi ya kuwajibika, kupunguza athari za kimazingira na kupunguza matumizi ya bidhaa zenye sumu kali na zilizopigwa marufuku.
Ukusanyaji wa Data:
Hukusanywa kama thamani ya namba katika lita na/au kilogramu.
Kwa kutumia rekodi za viuatilifu na kumbukumbu za matumizi yake, Mmiliki wa Cheti (CH) atakusanya taarifa kuhusu jumla ya kiasi cha viuatilifu vilivyotumika kwa zao lililoidhinishwa katika mwaka uliotangulia. Data hii imegawanywa kwa ajili ya dawa za viua-dudu, viua-panya, viua-kuvu, viua-magugu na vingine.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
|
|
Maji ya umwagiliaji mimea (Lita)
Maelezo:
Jumla ya kiasi cha maji yaliyotumika kwa ajili ya umwagiliaji mimea.
Kuhimiza usimamizi bora wa maji kwa kufuatilia matumizi ya maji ya umwagiliaji mimea kuanzia mwaka wa 1 na kuendelea, ili kuwawezesha wazalishaji kufuatilia matumizi ya maji, kuboresha matumizi ya rasilimali za maji, na kuimarisha mbinu endelevu za kilimo.
Ukusanyaji wa data:
Kumbuka: Kipengele hiki cha data kinatumika tu wakati umwagiliaji maji shambani unaporipotiwa.
Thamani ya nambari inayowakilisha jumla ya kiasi cha maji yaliyotumika kwa umwagiliaji, kwa lita.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Maji yanayotumika katika uchakataji (Lita)
Maelezo:
Jumla ya kiasi cha maji yaliyotumika kwa ajili ya uchakataji wa zao lililoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance katika mwaka uliopita. Lengo ni kuhimiza usimamizi bora wa maji kwa kufuatilia matumizi yake katika shughuli za uchakataji, na hivyo kuwawezesha wazalishaji kufuatilia matumizi ya maji, kuboresha matumizi ya rasilimali za maji, na kuimarisha mbinu endelevu za kilimo.
Ukusanyaji wa data:
Kumbuka: Kwa Usimamizi wa Vikundi, hii inatumika ikiwa vikundi vina vituo vya kati vya uchakataji.
Thamani ya nambari inayowakilisha jumla ya kiasi cha maji yaliyotumika katika shughuli za uchakataji, kwa lita.
Rekodi (kulingana na marudio ya shughuli za uchakataji) za kiasi cha matumizi ya maji kulingana na vipimo vinavyoonyeshwa na mfumo wa mita uliowekwa kwenye eneo la uchakataji. Angalia kipimo kilichotumika na, ikihitajika, fanya mabadiliko ya vipimo ili kupata data kwa lita.
Ikiwa mfumo wa mita haupatikani katika eneo la uchakataji, pima kiasi cha maji kilichokusanywa kwa ajili ya shughuli za uchakataji.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Matumizi ya kuni katika shughuli za uchakataji
Maelezo:
Jumla ya kuni zilizotumika katika uchakataji wa zao lililoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance katika mwaka uliotangulia. Lengo ni kuhimiza usimamizi bora wa matumizi ya kuni kwa kufuatilia kiasi cha kuni kinachotumika, ili kuwezesha wazalishaji kufuatilia matumizi yake.
Ukusanyaji wa data:
Kumbuka: Kwa Usimamizi wa Vikundi, hii inatumika ikiwa vikundi vina vituo vya kati vya uchakataji.
Thamani ya nambari inayowakilisha jumla ya kiasi cha kuni zilizotumika katika shughuli za uchakataji, kwa kilogramu.
Rekodi kuni zilizotumika kulingana na kiasi kilichonunuliwa/ kilichotumika kwa madhumuni ya uchakataji.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Asilimia ya eneo la shamba lililofunikwa na uoto wa asili
Maelezo:
Jumla ya eneo la shamba linalohifadhiwa chini ya uoto wa asili.
Lengo ni kudumisha na kufuatilia uoto wa asili kwa muda wote, huku taarifa zikiwasilishwa kila mwaka ili kufuatilia maendeleo. Ikiwa uoto wa asili utashuka chini ya 10% ya eneo lote la shamba, au chini ya 15% kwa mashamba yenye mazao yanayostahimili kivuli, weka malengo ya kuboresha na utekeleze hatua za kufikia na kudumisha viwango hivi kwa muda mrefu.
Ukusanyaji wa data:
Mzalishaji atapima (kwa kutumia poligoni au mbinu nyingine iliyobainishwa) eneo lililofunikwa na uoto wa asili, na kuripoti taarifa hii kwenye Fomu ya Kipengele cha Data.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia
Mwongozo M wa shirika la Rainforest Alliance: Mifumo asili ya Ikolojia na Uoto hutoa mwongozo kuhusu jinsi ya kupima uoto wa asili katika ardhi ya uhifadhi iliyotengwa na maeneo ya uzalishaji (kama vile uoto wa kivuli wa kilimo-mseto).
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
|
|
Jumla ya matumizi ya nishati ya visukuku kwa mwaka
Maelezo:
Hupima jumla ya nishati ya kisukuku inayotumika katika uzalishaji na uchakataji wa bidhaa zilizoidhinishwa. Hii inajumuisha vyanzo vya nishati kama vile dizeli, petroli, Gesi ya Petroli Iliyoyeyushwa (LPG) (propani), makaa ya mawe, gesi asilia, pamoja na mafuta. Inaripotiwa kwa ujazo wa nishati (Lita, mita za ujazo), au uzito (kg), iwe ni kwa ajili ya matumizi ya vifaa visivyohamishika (kama vile mabwela, mitambo ya kukaushia) au vifaa vinavyohamishika (kama vile matrekta). Matumizi ya nishati ya mimea (biofuels) hayapaswi kujumuishwa. Lengo ni kutathmini matumizi ya kawaida ya nishati shambani ili kutafuta njia za kuboresha ufanisi au kupunguza matumizi yake.
Ukusanyaji wa data:
Kumbuka: Hii inatumika kwa Usimamizi wa Vikundi pekee ikiwa vikundi vinatumia nishati ya visukuku kwa shughuli za uchakataji
Matumizi ya nishati ya visukuku katika shughuli za uchakataji na uzalishaji.
Thamani ya nambari yenye kipimo: lita, kilogramu, na mita za ujazo
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia
Mwongozo N wa shirika la Rainforest Alliance: Ufanisi wa Nishati unatoa miongozo kwa Wamiliki wa Vyeti ili kuwasaidia kurekodi taarifa hizi kulingana na Mahitaji ya Shamba ya Kiwango cha Kilimo Endelevu cha shirika la Rainforest Alliance
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Jumla ya matumizi ya umeme (kWh) kila mwaka
Maelezo:
Kipengele cha data cha jumla ya matumizi ya umeme kinahusu umeme unaotumika katika uzalishaji na uchakataji wa bidhaa zilizoidhinishwa, kama vile matumizi ya mashine za uchakataji. Hii inajumuisha vyanzo vya nishati jadidifu vinavyozalishwa shambani (nishati ya jua, upepo, maji) na umeme unaotoka kwenye gridi, na inaripotiwa kwa kWh za umeme uliotumika. Lengo ni kutathmini matumizi ya kawaida ya umeme shambani ili kutafuta njia za kuboresha ufanisi au kupunguza matumizi yake.
Ukusanyaji wa data:
Kumbuka: Hii inatumika kwa Usimamizi wa Kikundi pekee ikiwa vikundi vinatumia nishati katika shughuli za uchakataji.
Hukusanywa kama thamani ya nambari kwa kilowati-saa (kWh)
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia
Mwongozo N wa shirika la Rainforest Alliance: Ufanisi wa Matumizi ya Nishati hutoa miongozo kwa Wamiliki wa Vyeti ili kuwasaidia kurekodi taarifa hizi kulingana na Mahitaji ya Shamba ya Kiwango cha Kilimo Endelevu cha shirika la Rainforest Alliance.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Aina ya chanzo cha nishati jadidifu: nishati ya jua, upepo, maji, na nishati ya mimea (biofuels)
Maelezo:
Matumizi ya nishati jadidifu (ndiyo au hapana) na aina zinazotumiwa (nishati ya jua, upepo, maji, au nishati ya mimea). Lengo ni kuripoti au kubaini fursa za kutumia vyanzo vya nishati jadidifu ili kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi na uchafuzi wa hewa, na hivyo kuchangia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuboresha ustawi wa jamii zinazozunguka.
Ukusanyaji wa Data:
Bainisha iwapo shamba/mashamba haya yanatumia vyanzo vyovyote vya nishati jadidifu na kuyarekodi.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Viashiria vya Kiwango cha Kilimo Rejelevu (RAS)
Kilimo rejelevu ni mfumo wa kilimo unaozingatia kufanya kazi kwa kushirikiana na mifumo ya asili ili kuboresha afya ya udongo, kuhakikisha uendelevu wa muda mrefu. Huwasaidia wazalishaji kujenga mashamba yenye ustahimilivu zaidi, yaliyo na vifaa bora vya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na changamoto za kiuchumi.
Taarifa zinazokusanywa kupitia RAS zinaweza kutumika kutoa mwongozo katika upangaji, kufuatilia maendeleo ya usanifu upya wa mashamba, na kuimarisha ushirikiano katika mnyororo wa ugavi, huku zikionyesha yanayohitaji uboreshaji endelevu katika afya ya mazingira, usimamizi wa shamba na maisha ya wakulima.
Matokeo muhimu yanayofuatiliwa kupitia Uidhinishaji wa Kilimo Rejelevu:
Afya ya udongo: kuongezeka kwa kiwango cha mabaki ya viumbe hai, kuboreka kwa muundo na rutuba ya udongo, pamoja na uwezekano wa ongezeko la mavuno.
Ufanisi wa pembejeo: kupunguza matumizi ya pembejeo kutoka nje ya shamba na kuboresha mzunguko wa virutubisho, hivyo kupunguza gharama za uzalishaji.
Ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi: uwezo mkubwa wa kukabiliana na athari zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, wadudu waharibifu na magonjwa.
Fursa za masoko: upatikanaji wa masoko tofauti na kutambuliwa katika mnyororo wa ugavi.
Ustawi wa mkulima na mitandao ya ushirikiano: kuboreka kwa maisha ya wakulima na ushirikiano thabiti kati yao na wazalishaji wenzao.
Idadi ya Aina za Miti ya Kivuli kwa kila shamba
Maelezo:
Jumla ya idadi ya aina za spishi za miti ya kivuli zilizopo shambani.
Hii inalenga kuongeza wingi wa spishi mbalimbali miti ya kivuli katika kila shamba ili kuboresha ubora wa udongo, kuhifadhi bioanuwai, kuimarisha ulinzi wa vyanzo vya maji na kuchangia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia ufyonzaji wa kaboni.
Ukusanyaji wa Data:
Imekusanywa kama thamani ya nambari.
Hesabu idadi ya aina za miti inayotumika kutoa kivuli katika eneo ambapo zao lililoidhinishwa na shirika la RA, linakuzwa.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
*Ikiwa Mmiliki wa Cheti ameidhinishwa chini ya Kiwango cha Kilimo Endelevu, Kiashiria hiki huripotiwa mara moja tu.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Idadi ya miti ya kivuli kwa hekta
Maelezo:
Jumla ya idadi ya miti ya kivuli iliyopo shambani kwa kila hekta ya eneo ambapo mazao yaliyoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance yanakuzwa. Inalenga kuongeza idadi ya miti ya kivuli katika kila shamba ili kuboresha ubora wa udongo, kuhifadhi bioanuwai, kuimarisha ulinzi wa vyanzo vya maji na kuchangia katika kupunguza mabadiliko ya tabianchi kupitia ufyonzaji wa kaboni.
Ukusanyaji wa Data:
Imekusanywa kama thamani ya nambari.
Hesabu idadi ya miti ya kivuli kwa kila hekta ndani ya eneo ambapo mazao yaliloidhinishwa na shirika la RA, yanakuzwa.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
*Ikiwa Mmiliki wa Cheti ameidhinishwa chini ya Kiwango cha Kilimo Endelevu, Kiashiria hiki huripotiwa mara moja tu.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Idadi ya aina za miti asilia shambani
Maelezo:
Kiashiria hiki hupima jumla ya idadi ya aina tofauti za miti asilia iliyopo shambani, iwe imeota yenyewe kiasili au imepandwa kwa makusudi. Inaakisi utofauti wa aina za miti shambani na kiwango ambacho mifumo ya ikolojia ya eneo husika inahifadhiwa au kurejeshwa, huku pia ikikuza uhifadhi wa bioanuwai na kuimarisha ustahimilivu wa shamba. Miti asilia inaweza kupatikana katika mifumo ya kilimo mseto, kando ya mipaka ya mashamba, katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya upandaji wa miti au kuunganishwa katika mifumo ya uzalishaji kama vile ufugaji unaochanganya miti na malisho ya mifugo.
Ukusanyaji wa Data:
Imekusanywa kama thamani ya nambari.
Hesabu jumla ya idadi ya aina tofauti za miti asilia shambani.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Asilimia ya eneo la shamba linalotumika kwa kilimo mseto
Maelezo:
Kiashiria hiki hupima sehemu ya jumla ya eneo la shamba linalosimamiwa chini ya mifumo ya kilimo mseto. Inaakisi kiwango ambacho mbinu za kilimo-ikolojia zinatekelezwa ili kuimarisha bioanuwai, afya ya udongo, kulinda vyanzo vya maji, na kuimarisha ustahimilivu wa jumla wa shamba.
Ukusanyaji wa Data:
Inakusanywa kama asilimia ya jumla ya eneo la shamba.
Kwa vikundi vya mashamba ndogo, ripoti wastani wa asilimia katika mashamba yote ndani ya ukusanyaji wa data wa kikundi.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Asilimia ya eneo la shamba lililofunikwa na uoto wa asili
Maelezo:
Jumla ya eneo la shamba linalohifadhiwa chini ya uoto wa asili.
Kiashiria hiki hupima sehemu ya jumla ya eneo la shamba inayohifadhiwa au kurejeshwa katika hali ya uoto wa asili. Hii inajumuisha misitu ya asili, mifumo ya kilimo mseto, maeneo ya uoto wa asili kando ya kingo za mito, au maeneo yoyote yasiyolimwa ambayo hayajabadilishwa au kuharibiwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za kilimo. Kutunza uoto wa asili husaidia kulinda bioanuwai, kuboresha afya ya udongo na maji, na kuimarisha ustahimilivu wa jumla wa shamba.
Ukusanyaji wa Data:
Zimekusanywa kama asilimia ya jumla ya eneo la shamba.
Kwa vikundi vya mashamba ndogo, ripoti wastani wa asilimia katika mashamba yote ndani ya ukusanyaji wa data wa kikundi.
Mzalishaji atapima eneo lililofunikwa na uoto wa asili kwa kutumia poligoni au mbinu nyingine zinazokubalika, na kuripoti hili katika aua ya viashiria kwenye RACP.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
*Ikiwa Mmiliki wa Cheti ameidhinishwa chini ya Kiwango cha Kilimo Endelevu, Kiashiria hiki huripotiwa mara moja tu.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Lita au kilogramu za mbolea zisizo za kikaboni
Maelezo:
Kiasi cha mbolea zisizo za kikaboni (mbolea sanisi) kilichotumika kwenye zao kuu lililoidhinishwa katika mwaka uliotangulia, kikionyeshwa kwa kilogramu (Kg) au lita (L). Kufuatilia hili huwasaidia wazalishaji kuboresha usimamizi wa virutubisho, kupunguza matumizi ya pembejeo kupita kiasi na kusaidia afya ya udongo na mazingira.
Ukusanyaji wa Data:
Hukusanywa kama thamani ya nambari iliyoripotiwa kwa kutumia kilogramu (kg) na/au lita (L).
Jumla ya kiasi cha mbolea zisizo za kikaboni kilichotumika kwenye zao kuu.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
*Ikiwa Mmiliki wa Cheti ameidhinishwa chini ya Kiwango cha Kilimo Endelevu, Kiashiria hiki huripotiwa mara moja tu.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
|
|
Lita au kilogramu za mbolea za kikaboni
Maelezo:
Kiasi cha mbolea za kikaboni kilichotumika katika mwaka uliotangulia.
Mbolea za kikaboni zinajumuisha vitu vinavyotokana na mimea au wanyama, vinavyotoa virutubisho kwa mazao, kama vile mboji, samadi, udongo wa mabaki ya mimea iliyooza, na samadi ya majimaji. Ufuatiliaji wa matumizi ya mbolea za kikaboni husaidia kusimamia virutubisho kwa uwajibikaji, kuboresha afya ya udongo na kuendeleza mbinu endelevu za kilimo.
Ukusanyaji wa Data:
Hukusanywa kama thamani ya nambari iliyoripotiwa kwa kutumia kilogramu (kg) na/au lita (L).
Jumla ya kiasi cha mbolea za kikaboni kilichotumika kwenye zao kuu.
Data iliyoripotiwa ni ya mwaka uliotangulia.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
|
|
Idadi ya matumizi ya viuatilifu
Maelezo:
Kiashiria hiki hupima mara ngapi viuatilifu vinatumika kwenye zao katika mwaka uliotangulia. Kufuatilia marudio ya matumizi ya viuatilifu huwasaidia wazalishaji kufanya maamuzi sahihi na kutumia mbinu kama vile Usimamizi Jumuishi wa Wadudu Waharibifu na Magonjwa (IPM), ambazo hukuza udhibiti wa visumbufu kwa njia za asili na kusaidia uzalishaji wa mazao yenye uwezo mkubwa wa kustahimili changamoto na kuboresha afya ya udongo.
Ukusanyaji wa Data:
Imekusanywa kama thamani ya nambari.
Marudio ya matumizi ya viuatilifu kwa kila kiambato amilifu.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
|
|
Kiasi cha viuatilifu vilivyotumika (kg/ha, kikigawanywa kulingana na kila kiambato amilifu)
Maelezo:
Kiashiria hiki hupima kiasi cha viuatilifu vilivyotumika kwenye zao katika mwaka uliotangulia, kikigawanywa kulingana na kila kiambato amilifu.
Ukusanyaji wa Data:
Hukusanywa kama thamani ya nambari.
Jumla ya kiasi cha viuatilifu kilichotumika kwa kila kiambato amilifu.
Hurekodiwa kwa Kilogramu (Kg) kwa kila hekta.
Data iliyoripotiwa ni ya mwaka uliotangulia.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
|
|
Idadi ya viambato amilifu vilivyotumika chini ya misamaha
Maelezo:
Kiashiria hiki hupima idadi ya viambato amilifu vya viuatilifu vilivyoidhinishwa chini ya Sera ya Matumizi ya Kipekee (EUP) ya shirika la RA na/au Ombi la Matumizi ya Dharura, ambavyo vilitumika kwenye zao katika mwaka uliotangulia. Kufuatilia matumizi ya EUP husaidia kuhakikisha usimamizi unaowajibika wa matumizi ya viuatilifu, kuzingatia matakwa ya Kiwango cha Kilimo Rejelevu na kukuza mbinu salama na endelevu zaidi za kudhibiti visumbufu vya mazao.
Ukusanyaji wa Data:
Imekusanywa kama thamani ya nambari.
Jumla ya idadi ya viambato amilifu vilivyoorodheshwa chini ya EUP na/au vilivyoidhinishwa kupitia Maombi ya Matumizi ya Dharura na kutumika.
Data iliyoripotiwa ni ya mwaka uliotangulia.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
|
|
Asilimia ya eneo la uzalishaji linalotumia mbinu za ukarabati au urejeshaji
Maelezo:
Kiashiria hiki kinapima asilimia ya eneo linalozalisha mazao ambapo mbinu za ukarabati au urejeshaji hutumika, ikiwa ni pamoja na upogoaji kulingana na hali ya shamba. Kufuatilia utekelezaji wa mbinu hizi husaidia kuboresha afya ya mazao, kuongeza uzalishaji, na kuimarisha ustahimilivu wa shamba kwa muda mrefu.
Ukusanyaji wa Data:
Imekusanywa kama thamani ya nambari.
Asilimia ya wastani ya eneo la uzalishaji linalotumia mbinu za ukarabati na/au urejeshaji.
Hurekodiwa kwa asilimia.
Data iliyoripotiwa ni ya mwaka uliotangulia
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Asilimia ya eneo la uzalishaji lililofunikwa na mazao funikizi, mtandazo na/au magugu laini
Maelezo:
Sehemu ya eneo la uzalishaji linalodumisha ufunikaji wa udongo kupitia mazao funikizi, mtandazo asili, au magugu laini yanayoota kiasili. Kudumisha na kufuatilia ufuniko wa udongo husaidia kuboresha afya ya udongo, kuzuia mmomonyoko, kuhifadhi unyevunyevu na kuonyesha dhamira ya mzalishaji ya kutekeleza mbinu za kilimo rejelevu zinazoongeza ustahimilivu wa shamba kwa muda mrefu.
Ukusanyaji wa Data:
Imekusanywa kama thamani ya nambari.
Asilimia ya wastani ya eneo la uzalishaji lililofunikwa na mazao funikizi, mtandazo wa udongo na/au magugu laini.
Hurekodiwa kwa asilimia.
Data iliyoripotiwa ni ya mwaka uliotangulia
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Asilimia ya enelo lililoathirika na mmomonyoko wa udongo
Maelezo:
Kiashiria hiki hupima asilimia ya eneo la uzalishaji lililoathiriwa na mmomonyoko wa udongo.
Kufuatilia mmomonyoko wa udongo husaidia kutathmini ufanisi wa mbinu za uhifadhi wa udongo kama vile kama vile upandaji wa mimea kwa kufuata mistari ya kontua, uwekaji wa matandazo, kilimo mseto, na upandaji wa mazao funikizi ya udongo. Hii huchangia kuboresha afya ya udongo na kuimarisha ustahimilivu wa shamba wa muda mrefu.
Ukusanyaji wa Data:
Imekusanywa kama thamani ya nambari.
Asilimia ya wastani ya eneo la uzalishaji lililoathiriwa na mmomonyoko wa udongo
Hurekodiwa kwa asilimia.
Data iliyoripotiwa ni ya mwaka uliotangulia
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Asilimia ya mabaki ya viumbe hai kwenye udongo na/au hesabu ya nyungunyungu, na/au Idadi ya vijidudu
Maelezo:
Ili kufuatilia afya ya udongo kwa kuzingatia mbinu ya kilimo rejelevu, wazalishaji wanaweza kuchagua kuripoti kuhusu kiashiria kimoja au zaidi kati ya vifuatavyo: kiwango cha mabaki ya viumbe hai kwenye udongo, hesabu ya nyungunyungu, na/au Idadi ya vijidudu kwenye udongo. Kila kimoja cha viashiria hivi huakisi vipengele muhimu vya mfumo wa udongo wenye afya na viumbe hai.
Ukusanyaji wa Data:
Imekusanywa kama thamani ya nambari.
Ripoti kiwango cha mabaki ya viumbe hai kwenye udongo kwa asilimia.
Ripoti hesabu ya nyungunyungu kwa uzito (Kg/ha).
Ripoti Idadi ya vijidudu kwenye udongo kama idadi kwa kila gramu ya udongo.
Kwa vikundi vya mashamba ndogo, inapaswa kuwa wastani wa viashiria vyovyote walivyochagua kuripoti.
Data iliyoripotiwa ni ya mwaka uliotangulia
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
|
|
Jumla ya matumizi ya maji kwa ajili ya umwagiliaji (Lita)
Maelezo:
Jumla ya kiasi cha maji kilichotumika kwa umwagiliaji shambani (kwa lita). Kuhamasisha usimamizi bora wa maji kwa kufuatilia matumizi ya maji ya umwagiliaji kuanzia mwaka wa 1 na kuendelea, ili kuwawezesha wazalishaji kufuatilia matumizi ya maji, kuboresha rasilimali za maji na kuendeleza mbinu endelevu za kilimo.
Ukusanyaji wa data:
Kumbuka: Hututumika tu pale ambapo umwagiliaji unafanyika na taarifa zake kuripotiwa shambani.
Thamani ya nambari inayowakilisha jumla ya kiasi cha maji yaliyotumika kwa umwagiliaji, kwa lita.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
*Ikiwa Mmiliki wa Cheti ameidhinishwa chini ya Kiwango cha Kilimo Endelevu, Kiashiria hiki huripotiwa mara moja tu.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Jumla ya matumizi ya maji kwa ajili ya usindikaji (Lita)
Maelezo:
Jumla ya maji yaliyotumika kusindika zao lililoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance katika mwaka uliotangulia. Kufuatilia matumizi ya maji katika shughuli za usindikaji kunahimiza usimamizi bora wa maji, kunawawezesha wazalishaji kufuatilia matumizi yake, kuboresha rasilimali za maji na kuendeleza mbinu za kilimo endelevu.
Ukusanyaji wa data:
Kumbuka: Kwa Usimamizi wa Vikundi, hii inatumika ikiwa vikundi vina vituo vya kati vya uchakataji.
Thamani ya nambari kwa lita.
Rekodi jumla ya kiasi cha maji yaliyotumika kulingana na mfumo wa kurekodi taarifa za usimamizi uliowekwa katika eneo au maeneo ya usindikaji. Hakikisha kipimo kilichotumika na ubadilishe kuwa lita inapohitajika.
Ikiwa hakuna mfumo wa kurekodi taarifa uliopo, pima kiasi cha maji yaliyokusanywa kwa ajili ya shughuli za usindikaji.
Data inayowasilishwa ni ya mwaka uliotangulia.
*Ikiwa Mmiliki wa Cheti ameidhinishwa chini ya Kiwango cha Kilimo Endelevu, Kiashiria hiki huripotiwa mara moja tu.
Utekelezwaji:
Uidhinishaji wa kikundi | Uidhinishaji binafsi | ||
Mashamba madogo | Mashamba makubwa | Usimamizi wa kikundi | Dogo/Kubwa |
|
|
| |
Taarifa nyinginezo
Tarehe ya kwanza ya kuchapishwa kwa hati hii (v 1.0): Machi 3, 2025
Nyaraka zilizotajwa kuwa "za lazima" lazima zizingatiwe ili kupata uidhinishaji. Nyaraka zinazotajwa kama "zisizo funganisha" hutoa taarifa zisizo za lazima ili kuwasaidia wasomaji kuelewa na kutekeleza masharti pamoja na maudhui mengine yanayolazimisha.
Kanusho la Tafsiri
Kwa swali lolote linalohusiana na maana kamili ya taarifa katika tafsiri, rejelea toleo rasmi la Kiingereza kwa ufafanuzi. Makosa yoyote au tofauti za maana zinazotokana na tafsiri, hazilazishi na hazina athari kwa madhumuni ya ukaguzi au uthibitisho.
Unakili, urekebishaji, usambazaji, au uchapishaji upya wa maudhui haya ni marufuku kabisa bila idhini ya maandishi ya awali kutoka kwa shirika la Rainforest Alliance.
Taarifa zaidi?
Kwa msaada wa kupata cheti cha shirika la Rainforest Alliance, wasiliana na timu yetu ya Mafanikio ya Wateja kupitia customersuccess@ra.org.
Kwa taarifa zaidi kuhusu shirika la Rainforest Alliance, tembelea http://www.rainforest-alliance.org wasiliana kupitia info@ra.org au Ofisi ya shirika la Rainforest Alliance Amsterdam, De Ruijterkade 6, 1013AA Amsterdam, Uholanzi.























































































































