--- title: "Kiambatisho cha Ziada v1.4" slug: "premium-annex-v1-4-swahili" status: "new" updated: 2026-11-20T10:41:51Z published: 2026-11-20T10:41:51Z canonical: "knowledge.rainforest-alliance.org/premium-annex-v1-4-swahili" --- > ## Documentation Index > Fetch the complete documentation index at: https://knowledge.rainforest-alliance.org/llms.txt > Use this file to discover all available pages before exploring further. # Kiambatisho cha Ziada v1.4 ### ![](https://cdn.document360.io/929f3fed-0f9d-454a-80e4-d7496bf45e88/Images/Documentation/indicator-guidance-image-g96v93xw.png?sv=2026-02-06&spr=https&st=2026-11-20T20%3A47%3A29Z&se=2026-11-20T21%3A47%3A29Z&sr=b&sp=r&sig=cn9Q%2FRuPMZjvmPO0im%2Bo6nuXRfXymbEIHj6hM5h7EZI%3D) | Kichwa: | Kiambatisho cha Ziada | | --- | --- | | Msimbo: | A-06-SRCL-B-CH | | Toleo: | 1.4 | | Inatumika kwa: | Wamiliki wa Vyeti vya Kilimo na Mnyororo wa Ugavi | | Utekelezaji: | Maudhui ya kuunganisha | | Kuanzia: | Machi 1, 2026 | | Inakamilika ifikapo: | Hadi itakapotangazwa vinginevyo | | Imechapishwa mnamo: | Septemba 8, 2025 | | Imeunganishwa na: | [A-1-S-B-F-V1.4 Kiwango cha Kilimo Endelevu cha shirika la Rainforest Alliance.](https://knowledge.rainforest-alliance.org/docs/rainforest-alliance-sustainable-agriculture-standard-farm-requirements-swahili) [A-33-R-B-FA-V1.0 Kiwango cha Kilimo Rejelevu cha shirika la Rainforest Alliance.](https://knowledge.rainforest-alliance.org/docs/rainforest-alliance-regenerative-agriculture-standard-swahili) [A-35-SRCL-B-SC_V1.5 Mahitaji ya Mnyororo wa Ugavi wa shirika la Rainforest Alliance.](https://knowledge.rainforest-alliance.org/docs/rainforest-alliance-sustainable-agriculture-standard-supply-chain-requirements-v15) | | Inachukua nafasi ya: | [A-06-SRCL-B-CH-V1.3 Kiambatisho cha Ziada](https://knowledge.rainforest-alliance.org/docs/premium-annex) | ### Hati hii inahusu nini? Kiambatisho hiki kinajumuisha maudhui ya ziada yenye masharti ya lazima kwa ajili ya mahitaji yaliyojumuishwa katika Sura ya Ada ya ziada ya Viwango vya shirika la Rainforest Alliance na Mahitaji ya Mnyororo wa Ugavi. Hati hii inajumuisha: - Maelezo ya ziada kuhusu ni wahusika wanaowajibika kulipa malipo ya ada ya ziada. - Maelezo ya ziada kuhusu masharti ya malipo ya ada ya ziada. - Maelezo ya ziada kuhusu utekelezaji wa mahitaji ya ada ya ziada katika hali maalum. - Maelezo ya ziada kuhusu utoaji wa taarifa za ada ya ziada kwenye mfumo wa la ufuatiliaji wa bidhaa. ### Lini na jinsi ya kutumia hati hii? Hati hii inawapa Wamiliki wa Vyeti na Mashirika ya Uthibitishaji maelezo ya ziada kuhusu utekelezaji wa mahitaji yaliyojumuishwa kutoka Viwango vya Rainforest Alliance na Mahitaji ya Mnyororo wa Ugavi ## Mabadiliko katika sasisho kutoka v1.2 hadi v1.3 | **Sehemu** | **Nini kimebadilika** | | --- | --- | | Hati Nzima | Lugha imesasishwa ili kuakisi Uidhinishaji wa Kilimo Rejelevu. | | Sehemu ya 2 | Ufafanuzi kuhusu matunda yaliyosindikwa na majukumu ya ada ya ziada. | | Sehemu ya 2.3, Sharti la 3.1.1 | Marekebisho ya Februari 25, 2026: Sasisho la kiwango cha ubadilishaji fedha kuwa sawa na thamani ya Euro, litakalotumika kwa kakao iliyoidhinishwa inayozalishwa katika msimu wa mavuno wa 2026-2027 na baadaye. | ## 1. Utangulizi **Utangulizi na Matarajio ya Uidhinishaji wa mara Mbili** Utekelezaji wa mahitaji ya ada ya ziada hutofautiana kulingana na sekta, ukizingatia mienendo ya kipekee ya mnyororo wa ugavi wa kila bidhaa iliyoidhinishwa katika soko la kimataifa. Kiambatisho hiki kinatoa mahitaji mahususi kwa sekta ili kuhakikisha kuwa ada ya ziada inatumika kwa haki na kwa uthabiti katika mazingira mbalimbali. Malipo ya ziada yanafafanuliwa kama malipo ya kifedha yanayofanywa na taasisi inayowajibika, pamoja na bei ya soko, ada ya ziada kutokana na ubora au tofauti nyingine za bei. Mahitaji ya malipo ya ziada yanatumika kwa kiasi cha bidhaa zinazouzwa zikiwa na uidhinishaji wa shirika la Rainforest Alliance (SAS), uidhinishaji wa Kilimo Rejelevu wa shirika la Rainforest Alliance (RAS), na uidhinishaji mara mbili wa shirika la Rainforest Alliance (SAS+RAS). Malipo haya ni muhimu ili kuwatuza wakulima kwa juhudi zao za kuzingatia uendelevu na kuimarisha thamani ya muda mrefu ya uidhinishaji. Pale ambapo kiasi cha bidhaa kimeidhinishwa chini ya Kiwango cha Kilimo Endelevu na Kiwango cha Kilimo Rejelevu cha shirika la Rainforest Alliance, malipo ya ziada hulipwa mara moja tu. Hata hivyo, inatarajiwa kuwa malipo haya ya ziada yatakuwa ya juu zaidi kuliko yale yanayolipwa kwa kiasi cha bidhaa kilichoidhinishwa chini ya kiwango kimoja pekee. Shirika la Rainforest Alliance linaamini kuwa juhudi kubwa zaidi zinapaswa kuambatana na malipo makubwa zaidi, na inahimiza kwa dhati kampuni kuzingatia kanuni hii katika taratibu zao za ununuzi wa bidhaa. Ili kuwezesha mabadiliko haya, tutaendelea kufuatilia kwa karibu data inayohusiana na malipo ya ziada. ## 2. Utekelezaji wa mahitaji ### 2.1 Majukumu kuhusu Makubaliano na Malipo Utekelezaji wa mahitaji ya malipo ya ziada hutofautiana kulingana na sekta (na eneo katika baadhi ya matukio). Jedwali lililo hapa chini linaonyesha Mmiliki wa Cheti (CH) wa Mnyororo wa Ugavi anayewajibika kutekeleza mahitaji haya: **Jedwali la 1.** Muhtasari wa taasisi zinazowajibika kutekeleza mahitaji ya malipo ya ziada. | **Zao/Sekta** | **Taasisi inayowajibika kulipia Malipo ya ziada** | **Wajibu:** | | --- | --- | --- | | Kahawa | **Mnunuzi wa Kwanza** *Taasisi ya kwanza inayopokea muamala kwenye mfumo wa ufuatiliaji bidhaa wa shirika la Rainforest Alliance baada ya mmiliki wa cheti wa shamba linalozalisha.* | - bainisha kiasi na masharti ya malipo ya ziada katika mikataba au makubaliano yaliyotiwa saini na Wamiliki wa Vyeti vya Mashamba (CHs) - fanya malipo kwa kiasi cha bidhaa zilizonunuliwa zikiwa zimeidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance (SAS), zimeidhinishwa kama zinazozalishwa kupitia Kilimo Rejelevu na shirika la Rainforest Alliance (RAS), au zimeidhinishwa chini ya mifumo yote miwili ya uidhinishaji ya shirika la Rainforest Alliance (SAS+RAS) | | Kakao | | Matunda yaliyosindikwa na Mafuta ya Nazi | | Karanga | | Mimea ya viungo na Viungo vya chakula | | Mazao mengine | | Chai | **Mmiliki** **wa chapa** Dokezo kwa wamiliki wa chapa za huduma za chakula na rejareja: mtengenezaji wa bidhaa zenye chapa binafsi (mpakiaji) lazima akubali kulipa, athibitishe, na alipe malipo ya ziada kwa niaba ya mmiliki wa chapa ya rejareja. Chapa za rejareja zinatakiwa kumfidia mtengenezaji wa bidhaa zenye chapa binafsi (mpakiaji) kwa malipo haya ya ziada. | (Iwapo hakuna mkataba au makubaliano yaliyotiwa saini kati ya mmiliki wa cheti (CH) cha shamba na mmiliki wa chapa) - toa ahadi rasmi katika mfumo wa ufuatiliaji bidhaa wa shirika la Rainforest Alliance - bainisha kiasi cha malipo ya ziada kwa kila kiasi cha bidhaa - fanya malipo kwa kiasi cha bidhaa zilizouzwa zikiwa zimeidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance (SAS), zimeidhinishwa kama zinazozalishwa kupitia kilimo Rejelevu na shirika la Rainforest Alliance (RAS), au zimeidhinishwa chini ya mifumo yote miwili ya uidhinishaji ya shirika la Rainforest Alliance (SAS+RAS). Uhamishaji wa malipo ya ziada kwa Wamiliki wa Vyeti (CHs) vya mashamba utawezeshwa na kituo cha malipo cha shirika la Rainforest Alliance. | | Ndizi na Matunda Mabichi[[1]](/docs/premium-annex-v1-4-swahili#footnote-2) | **Mwagizaji bidhaa kutoka nje ya nchi** *shirika lililo nje ya nchi ya asili ya bidhaa, ambalo huagiza moja kwa moja kutoka nchi hiyo kiasi cha bidhaa zilizoidhinishwa, ikiwemo wauzaji wa rejareja, wamiliki wa chapa au shirika lingine lolote linalotekeleza kazi hii.* | - bainisha masharti ya malipo katika mikataba na wasambazaji wao wa moja kwa moja Kumbuka: - Wasafirishaji wa bidhaa nje ya nchi lazima wawasilishe malipo ya ziada kwa Mmiliki wa Cheti (CH) wa shamba. | | Maua | *TBD* | *TBD* | > [!WARNING] > **KUMBUKA:** Mashirika yanayoshughulikia mazao mbalimbali yanaweza kuwa na majukumu tofauti kuhusu malipo ya ziada, kulingana na jukumu lao katika kila mnyororo wa ugavi na wajibu wa malipo uliowekwa kwa sekta husika. ### 2.2 Sharti la 3.1.1: Kuripoti Malipo ya ziada **- Mbinu ya mnunuzi na mwagizaji wa kwanza** - Wakati wa kuingiza muamala wa mauzo, Wamiliki wa Vyeti (CHs) vya mashamba lazima waweke kiasi cha malipo ya ziada kilichokubaliwa katika mkataba au makubaliano yaliyotiwa saini katika sehemu ya “malipo ya ziada yaliyokubaliwa” ya maelezo ya muamala. Kiasi cha malipo ya ziada kilichokubaliwa katika sarafu za ndani hubadilishwa na kurekodiwa kwa Euro (€) au Dola za Marekani (US$). - Mnunuzi wa kwanza lazima athibitishe kiasi cha malipo ya ziada kilichokubaliwa kwa kuthibitisha muamala mzima. Ikiwa kiasi kilichoingizwa na Mmiliki wa Cheti (CH) cha shamba kinatofautiana na kile kilichokubaliwa, mnunuzi wa kwanza anaweza kukataa muamala wa mauzo na kumwomba Mmiliki wa Cheti cha shamba arekebishe kiasi hicho. Kwa ndizi na matunda mengine mabichi: Malipo ya ziada yaliyokubaliwa kati ya Mmiliki wa Cheti (CH) cha shamba na mnunuzi wa kwanza hurekodiwa kwenye mfumo. Ikiwa mwagizaji sio mnunuzi wa kwanza, malipo ya ziada yaliyokubaliwa na wasambazaji hurekodiwa nje ya mfumo wa ufuatiliaji wa bidhaa wa Rainforest Alliance. **- Mbinu ya mmiliki wa chapa** - Wakati wa kukomboa kiasi cha bidhaa zilizoidhinishwa kutoka kwenye mfumo wa ufuatiliaji wa bidhaa wa shirika la Rainforest Alliance, mmiliki wa chapa huweka kiasi cha malipo ya ziada alichoahidi kulipa na kuthibitisha kulipa kwenye mfumo huo. Kwa chapa za huduma za chakula na rejareja, hatua hizi hutekelezwa na mtengenezaji wa bidhaa zenye chapa binafsi (mpakiaji), isipokuwa pale ambapo chapa ya huduma za chakula au rejareja inapochukua jukumu la kutimiza ahadi hiyo, malipo ya ziada, na ukombozi wa bidhaa zilizoidhinishwa. ### 2.3 Sharti la 3.1.1: Kiasi cha Chini kabisa Shirika la Rainforest Alliance limeweka kiwango cha chini kabisa cha malipo ya ziada ya kifedha kwa kakao. Hii inamaanisha kuwa malipo ya ziada yaliyokubaliwa kati ya mnunuzi wa kwanza na Mmiliki wa Cheti (CH) cha shamba lazima angalau yafikie kiwango hiki. **Jedwali la 2.** Kiwango cha chini zaidi cha malipo ya ziada kwa kakao | **Kakao** | **Kanda** | | --- | --- | | **Nchi za Afrika zinazotumia XOF au XAF** | **Sehemu zingine za Dunia** | | **Kiwango cha chini cha malipo ya ziada*** | Euro 63 kwa kila tani ya kokwa za kakao** | Euro 64 kwa kila tani ya kokwa za kakao | Dola 70 za Marekani kwa kila tani ya kokwa za kakao | | **Tarehe inayotumika** | Kakao yote iliyoidhinishwa iliyozalishwa katika msimu wa mavuno wa 2023-2024, 2024-2025, 2025-2026 na kuuzwa ikiwa imeidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance | Kakao yote iliyoidhinishwa iliyozalishwa inayozalishwa katika msimu wa mavuno wa 2026-2027 (na misimu iliyofuata) inayouzwa kama Iliyoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance | Julai 1, 2022 | > [!WARNING] > **Kumbuka:** Kwa kakao, angalau Dola za Marekani ($70USD) kwa kila tani (sawa na Euro 64 kwa nchi za Afrika zinazotumia XOF au XAF), au 40% ya jumla ya malipo ya ziada ya fedha yaliyopokelewa na Mmiliki wa Cheti (CH) cha shamba, kulingana na kiasi kikubwa zaidi, lazima kigawiwe kwa wanachama wa kikundi. Tazama Sehemu ya 3 kwa maelezo zaidi. **Tafadhali rejelea Sera ya Uidhinishaji wa Mashamba na Mnyororo wa Ugavi wa Kakao kwa maelezo ya ziada yanayohusiana na nchi ya Côte d’Ivoire.** ### 2.4 Sharti la 3.1.2: Mikataba au Makubaliano yaliyotiwa Saini kuhusu Malipo ya ziada Katika mazao yote isipokuwa chai, vikundi na mashamba yaliyoidhinishwa kibinafsi lazima viwe na mikataba iliyo wazi inayobainisha kiasi cha malipo ya ziada na masharti mengine. **Mbinu ya Mnunuzi wa Kwanza (kahawa, kakao, matunda yaliyosindikwa na mafuta ya nazi, karanga, mimea ya viungo na viungo vya chakula, mazao mengine)** Wanunuzi wa kwanza lazima wajadiliane na Wamiliki wa Vyeti vya mashamba kuhusu kiasi cha malipo ya ziada. Mmiliki wa Cheti (CH) cha mnyororo wa ugavi atajumuisha kiasi cha malipo ya ziada kilichokubaliwa katika mikataba au makubaliano yaliyotiwa saini na Wamiliki wa Vyeti vya mashamba. **Mbinu ya Mwagizaji wa bidhaa (ndizi na matunda mabichi)** Waagizaji wa bidhaa lazima wajadiliane na kukubaliana na msambazaji bidhaa kuhusu kiasi cha malipo ya ziada. Kiasi cha malipo ya ziada kilichokubaliwa kinajumuishwa katika mikataba. Ikiwa mwagizaji haununui moja kwa moja kiasi cha bidhaa zilizoidhinishwa kutoka kwa Mmiliki wa Cheti (CH) cha shamba, Mmiliki wa Cheti cha mnyororo wa ugavi katika nchi ya asili (wanunuzi wa kwanza/wasafirishaji wa bidhaa nje ya nchi, n.k.) lazima ajumuishe kiasi cha malipo ya ziada kilichojadiliwa katika mikataba au makubaliano yaliyotiwa saini na Mmiliki wa Cheti (CH) cha shamba. Mmiliki wa cheti cha mnyororo wa ugavi anayeingia katika mkataba moja kwa moja na Mmiliki wa Cheti (CH) cha shamba lazima amlipe kiasi cha malipo ya ziada kilichokubaliwa. **Mbinu ya Mmiliki wa chapa (chai)** Wamiliki wa chapa lazima waweke ahadi ya kiasi cha malipo ya ziada watakacholipa kwa kila kipimo cha kiasi cha bidhaa. Malipo kwa Wamiliki wa Vyeti (CH) vya mashamba yatafanywa kupitia mfumo wa malipo ya shirika la Rainforest Alliance, huku ankara ikitumwa kwa mmiliki wa chapa. Kwa chapa za huduma za chakula na za rejareja, mahitaji haya yanawezeshwa na mtengenezaji wao wa chapa binafsi (mpakiaji) ambaye atakomboa kiasi cha bidhaa na kuweka ahadi ya kulipa malipo ya ziada. **Wamiliki wa Vyeti (CH) vya mashamba wanaonunua bidhaa zilizoidhinishwa kutoka kwa mashamba mengine** Mmiliki wa Chati (CH) cha shamba anayenunua bidhaa zilizoidhinishwa kutoka kwa Wamiliki wa Vyeti (CHs) vya mashamba wengine huchukuliwa kuwa mnunuzi wa kwanza wa kiasi cha bidhaa alizonunua. Kwa mazao ambayo mnunuzi wa kwanza anawajibika kulipia malipo ya ziada (tazama jedwali la 1), Wamiliki hawa wa Vyeti (CH) vya mashamba lazima walipe malipo ya ziada kwa kiasi cha bidhaa walizonunua zikiwa zimeidhinishwa. ### 2.5 Muda wa kulipa Malipo ya ziada Shirika la Rainforest Alliance limeweka muda maalum wa kulipa malipo ya ziada kwa kila sekta, kama ilivyoonyeshwa katika jedwali hapa chini: **Jedwali la 3.** Muda wa kulipa malipo ya ziada | **Zao/Sekta** | **Muda wa malipo unaotumika** | | --- | --- | | Kahawa | Malipo hufanywa sio zaidi ya miezi 12 baada ya bidhaa kusafirishwa kutoka kwa mmiliki wa cheti (CH) kwenda kwa mnunuzi wa kwanza. | | Matunda Yaliyosindikwa na Mafuta ya Nazi | | Karanga | | Mimea ya viungo na Viungo vya chakula | | Mazao mengine | | Kakao | Malipo hufanywa sio zaidi ya miezi 6 baada ya bidhaa kusafirishwa kutoka kwa Mmiliki wa Cheti (CH) cha shamba kwenda kwa mnunuzi wa kwanza, isipokuwa pale ambapo kanuni za eneo husika zinahitaji muda tofauti. | | Chai | Malipo hufanywa kila baada ya miezi mitatu. Jumla ya malipo ya kila robo mwaka hulipwa ndani ya muda uliowekwa kwenye ankara ya malipo ya ziada kutoka kwenye mfumo wa malipo wa shirika la Rainforest Alliance, na sio zaidi ya mwisho wa robo inayofuata. | | Ndizi na matunda mengine mabichi | Malipo yamefunganishwa na malipo ya kawaida kwa bidhaa iliyoidhinishwa. | ## 3. Majukumu ya Shamba Kuhusu Malipo ya Ziada ### Sharti la 3.1.3: Usambazaji wa Malipo ya Ziada kwa Wanachama wa Kikundi Wamiliki wa Vyeti (CH) vya mashamba lazima wahifadhi ushahidi kamili na sahihi wa malipo yote ya kifedha ya malipo ya ziada yaliyofanywa kwa kila mwanachama wa kikundi, ikiwemo kiasi cha fedha kilichopokelewa. Kumbukumbu hizi lazima zisasishwe angalau kila mwaka. Ushahidi huo lazima uonyeshe kuwa jumla ya malipo ya ziada ya fedha kwa wanachama wa kikundi ni sawa na asilimia ya malipo ya ziada ya fedha yaliyopokelewa kutoka kwa mnunuzi/wanunuzi, iliyotengwa kwa ajili ya usambazaji. Kwa kiwango cha chini kabisa, kiasi hiki kinapaswa kuwa 40% ya jumla ya malipo ya ziada ya fedha ambayo kikundi kilichoidhinishwa kilipokea kutoka kwa mnunuzi/wanunuzi*. Gharama zinazohusiana na miamala na kodi pekee ndizo zinazoweza kukatwa kutoka kwa jumla ya malipo ya ziada ya fedha yaliyopokelewa, na ushahidi wa makato hayo lazima utolewe. Hii inamaanisha kuwa Wamiliki wa Vyeti (CH) vya mashamba lazima wawe na mfumo wa uhasibu unaofaa ili: - Kurekodi malipo ya ziada kando na bei ya bidhaa na ada ya ziada ya ubora au malipo mengine ya ziada. - Kurekodi kiasi na tarehe za malipo yaliyofanywa kwa kila mwanachama wa kikundi yakihusishwa na kiasi cha bidhaa iliyowasilishwa kwa kikundi. - Kuwapa wanachama wa kikundi taarifa kuhusu kiasi kilichokubaliwa cha malipo ya ziada (kwa kiasi), na muda na mbinu za malipo. - Kumpa kila mwanachama wa kikundi taarifa kuhusu kiasi cha malipo ya ziada ilicholipwa. > [!WARNING] > ***Kumbuka:** Kwa kakao, angalau Dola za Marekani ($70USD) kwa kila tani (sawa na Euro 64 kwa nchi za Afrika zinazotumia XOF au XAF), au 40% ya jumla ya malipo ya ziada ya fedha yaliyopokelewa na Mmiliki wa Cheti (CH) cha shamba, kulingana na kiasi kikubwa zaidi, lazima kigawiwe kwa wanachama wa kikundi. ### Sharti la 3.1.4: Malipo ya Ziada kwa Wamiliki wa Vyeti (CH) wa Mashamba Makubwa na Mashamba ya Binafsi Wamiliki wa Vyeti (CHs) wa mashamba makubwa na mashamba ya Binafsi lazima wahifadhi kumbukumbu sahihi za jinsi walivyotumia malipo ya ziada yaliyopokelewa. Hii inapaswa kujumuisha: - Jumla ya kiasi cha fedha kilichopokelewa kulingana na jumla ya kiasi cha bidhaa zilizouzwa. - Asilimia ya jumla ya malipo ya ziada yaliyopokelewa ambayo ilitumika kuwanufaisha wazalishaji au wafanyakazi. Wamiliki wa Vyeti hawatakiwi kuwasilisha taarifa hizi, lakini wanapaswa kuwa na kumbukumbu hizo tayari pindi zitakapohitajika na Mashirika ya Uidhinishaji, mawakala wao na/au shirika la Rainforest Alliance. ## 4. Uwazi Shirika la Rainforest Alliance limejizatiti kuimarisha uwazi katika mnyororo wa ugavi. Wamiliki wa vyeti vya mashamba ya chai hujulishwa kuhusu mmiliki wa chapa au mfungashaji aliyeahidi kulipa na kulipa kiasi cha malipo ya ziada kwa kila malipo yaliyofanyika. ## Taarifa nyinginezo Tarehe ya kwanza ya kuchapishwa kwa hati hii (v 1.0): Julai 1, 2022. Shirika la Rainforest Alliance linahifadhi haki ya kukagua, kuidhinisha, kukataa, au kubatilisha ruhusa hizi kwa Wamiliki wa Vyeti (CHs) mahususi na kwa kuzingatia kila kesi kivyake. Nyaraka zilizotajwa kuwa *"zinazofunganisha"* lazima zizingatiwe ili kupata uthibitisho. Nyaraka zinazotajwa kama *"zisizo funganisha"* hutoa taarifa zisizo za lazima ili kuwasaidia wasomaji kuelewa na kutekeleza masharti pamoja na maudhui mengine yanayolazimisha. **Kanusho la Tafsiri** Kwa swali lolote linalohusu na maana sahihi ya taarifa katika tafsiri, wasiliana na toleo rasmi la Kiingereza kwa ufafanuzi. Makosa yoyote au tofauti za maana zinazotokana na tafsiri, hazilazishi na hazina athari kwa madhumuni ya ukaguzi au uthibitisho. Unakili, urekebishaji, usambazaji, au uchapishaji upya wa maudhui haya ni marufuku kabisa bila idhini ya maandishi ya awali kutoka kwa shirika la Rainforest Alliance. **Taarifa zaidi?** Kwa msaada wa kupata cheti cha shirika la Rainforest Alliance, wasiliana na timu yetu ya Huduma kwa Wateja kupitia [customersuccess@ra.org](mailto:customersuccess@ra.org). Kwa taarifa zaidi kuhusu shirika la Rainforest Alliance, tembelea [http://www.rainforest-alliance.org](http://www.rainforest-alliance.org) wasiliana kupitia [info@ra.org](mailto:info@ra.org) au Ofisi ya shirika la Rainforest Alliance Amsterdam, De Ruijterkade 6, 1013AA Amsterdam, Uholanzi. **Futnodi** 1. Kwa matunda mabichi ambayo yatachakatwa zaidi, sehemu ya matunda yaliyosindikwa na mafuta ya nazi inapaswa kutumika kubainisha wajibu wa malipo ya ziada. [↑](/docs/premium-annex-v1-4-swahili#footnote-ref-2)