--- title: "Kiwango Cha Kilimo Rejelevu Cha Shirika La Rainforest Alliance - Mahitaji Ya Shamba v1.0" slug: "rainforest-alliance-regenerative-agriculture-standard-swahili" status: "new" updated: 2026-11-16T08:28:53Z published: 2026-11-16T08:28:53Z canonical: "knowledge.rainforest-alliance.org/rainforest-alliance-regenerative-agriculture-standard-swahili" --- > ## Documentation Index > Fetch the complete documentation index at: https://knowledge.rainforest-alliance.org/llms.txt > Use this file to discover all available pages before exploring further. # Kiwango Cha Kilimo Rejelevu Cha Shirika La Rainforest Alliance - Mahitaji Ya Shamba v1.0 Kwa kuzingatia uzoefu wa miongo kadhaa, kiwango hiki kinaongeza kina katika maeneo matatu ya athari yanayolenga mazingira asilia: afya na rutuba ya udongo, bioanuwai na ustahimilivu wa mabadiliko ya tabianchi. Wakati huo huo, inaendelea kuwa na mahitaji madhubuti ya kijamii. Kwa kulinda haki za binadamu na kuboresha maisha, utanzaji wa mazingira unaimarishwa, kwani wakulima na wafanyakazi walio salama na wenye afya bora wana uwezo zaidi wa kutunza mazingira. Kiwango cha Kilimo Rejelevu katika muundo wa kujitegemea kinajumuisha mahitaji mapya ya kilimo rejelevu, mahitaji ya msingi yanayoshirikiwa na Kiwango cha Kilimo Endelevu, na baadhi ya mahitaji mengine ya pamoja ya kilimo endelevu katika mada muhimu. Kwa pamoja, mahitaji haya yanalenga maeneo makuu matano: ustahimilivu wa mazao, afya ya udongo, bioanuwai, usimamizi wa maji na maisha bora. Muundo wa nyongeza unajumuisha mahitaji mapya ya kilimo rejelevu ambayo yanapaswa kutekelezwa pamoja na Mahitaji ya Kiwango cha Kilimo Endelevu. [PDF document](https://cdn.document360.io/929f3fed-0f9d-454a-80e4-d7496bf45e88/Images/Documentation/A-33-R-B-FA_V1.0SW_Rainforest-Alliance-Regenerative-Agriculture-Standard-Farm-Requirements.pdf?sv=2026-02-06&spr=https&st=2026-11-16T18%3A00%3A38Z&se=2026-11-16T19%3A00%3A38Z&sr=b&sp=r&sig=Vfj6R0jbfS5K9ZJFUFbuAyp5vdTd1g4NZ%2F3kEAvUcfI%3D)