Swahili is the latest language to be added to the Knowledge Hub. Swahili versions of key documents (e.g. Certification Standard and Annexes) are now available!

Kiambatisho cha Mazingira v1.3

Prev Next

Kichwa:

Kiambatisho cha Mazingira

Msimbo:

A-09-SCRL-B-FA

Toleo:

1.3

Inatumika kwa:

Wamiliki wa Vyeti vya Shamba

Utekelezaji:

Maudhui ya kuunganisha

Kuanzia:

Machi 1, 2026

Inakamilika ifikapo:

Hadi itakapotangazwa vinginevyo

Imechapishwa mnamo:

Septemba 8, 2025

Imeunganishwa na:

A-1-S-B-F-V1.4 Kiwango cha Kilimo Endelevu cha shirika la Rainforest Alliance.

A-33-R-B-FA-V1.0 Kiwango cha Kilimo Rejelevu cha shirika la Rainforest Alliance.

Inachukua nafasi ya:

A-09-SCRL-B-FA-V1.2- Kiambatisho cha Mazingira

Hati hii inahusu nini?

Kiambatisho hiki kinajumuisha maudhui ya ziada ya kishia kuhusu mahitaji ya Mashamba yaliyojumuishwa katika Sura ya Mazingira ya viwango vya shirika la Rainforest Alliance.

Hati hii inajumuisha:

  • Taarifa za ziada zinazohusiana na mahitaji ya msingi kuhusu ulinzi wa misitu ya asili, mifumo ya ikolojia wa asili, na maeneo yaliyolindwa.

  • Maelezo ya ziada kuhusu maeneo ya uhifadhi na urejeshaji nje ya mipaka ya shamba kwa ajili ya Kiwango cha Kilimo Endelevu.

  • Maelezo ya ziada kuhusu uhifadhi na uboreshaji wa mifumo asilia ya ikolojia na uoto wa asili kwa ajili ya Kiwango cha Kilimo Rejelevu.

Lini na jinsi ya kutumia hati hii?

Hati hii inawapa Wamiliki wa Vyeti na Mashirika ya Uidhinishaji maelezo ya ziada kuhusu mahitaji yaliyomo na jinsi ya kuyatekeleza. Hati hii imegawanywa katika sehemu tatu:

  • Mahitaji ya Msingi kwa viwango vya Mashamba

  • Mahitaji kutoka kwa Kiwango cha Kilimo Endelevu

  • Mahitaji kutoka Kiwango cha Kilimo Rejelevu

Mahitaji ya msingi yanatumika kwa viwango vyote vya Mashamba. Mahitaji kutoka sehemu za Kiwango cha Kilimo Endelevu na Kiwango cha Kilimo Rejelevu yanajumuisha mahitaji maalum na/au ya maboresho ya kuendelea, yanayotumika kwa kiwango husika.

Mabadiliko katika sasisho kutoka v1.2 hadi v1.3

Sehemu

Nini kimebadilika

Katika hati nzima

Ujumuishaji wa sehemu kuu kwa ajili ya mahitaji ya msingi ya kawaida na mahitaji maalum kutoka kwa Kiwango cha Kilimo Endelevu na Kilimo Rejelevu.

Mahitaji ya msingi

Upangaji upya wa mahitaji ya ulinzi wa misitu asilia, mifumo mingine ya asilia ya ikolojia, na maeneo yaliyolindwa kwa ajili ya uwazi.

1.5 Ubadilishaji Mdogo Uliopangwa kwa ajili ya Miundombinu

Ufafanuzi kwamba huduma hii haipatikani kwa Wamiliki wa Vyeti (CHs) wa kakao na kahawa wanaotaka kuoanishwa na EUDR.

Mahitaji kutoka kwa Kiwango cha Kilimo Endelevu

Mahitaji ya uboreshaji endelevu 6.2.3 na 6.2.4 yamehamishiwa kwenye sehemu hii.

Kiwango cha Kilimo Rejelevu

Ujumuishaji wa maelezo ya ziada ya mahitaji maalum ya Kiwango kipya cha Kilimo Rejelevu.

Mahitaji ya Msingi kwa ajili ya viwango vya Mashamba

Sehemu hii inatoa maelezo zaidi kwa ajili ya utekelezaji wa mahitaji husika ya msingi ya Kiwango cha Kilimo Endelevu (SAS) cha shirika la Rainforest Alliance na Kiwango cha Kilimo Rejelevu (RAS).

 1. Ulinzi wa misitu ya asili, mifumo mingine asilia ya ikolojia na maeneo yaliyohifadhiwa

Sehemu hii inatoa maelezo ya ziada kuhusu ubadilishaji wa hitaji 6.1.1 na uvamizi katika maeneo yaliyolindwa ya hitaji 6.1.2 kutoka kwa Kiwango cha Kilimo Endelevu.

1.1 Tathmini ya Hatari ya Data ya Kijiografia inayohusishwa na mahitaji 6.1.1 na 6.1.2

Tathmini ya hatari ya Data ya kijiografia ya shirika la Rainforest Alliance inawapatia Wamiliki wa Vyeti taarifa zifuatazo:

  • Ramani ya hatari ya ukataji misitu.

  • Ramani ya hatari ya uvamizi katika maeneo yaliyolindwa.

  • Jedwali la hatari ya data ya kijiografia ya kila kitengo cha shamba lenye kiwango cha ukataji misitu na uvamizi wa maeneo yaliyohifadhiwa.

Matokeo haya yanatoa muhtasari wa uwezekano wa kutofuata ipasavyo mahitaji ya 6.1.1 na 6.1.2 ya shirika la Rainforest Alliance. Tathmini ya hatari inapatikana kwa Wamiliki wa Vyeti na Mashirika ya Uidhinishaji kwenye jukwaa la uidhinishaji la shirika la Rainforest Alliance na husasishwa kila mara data ya eneo la kijiografia inapoboreshwa.

1.2 Kutobadilisha misitu ya asili na mifumo asili ya ikolojia inayohusishwa na hitaji la 6.1.1  

Hitaji la msingi la 6.1.1 linaweka Januari 1, 2014 kama tarehe ya mwisho ambayo baada ya hapo hakuna ukataji misitu au ubadilishaji wowote unaoruhusiwa kufanyika. Ukataji misitu au ubadilishaji wowote unaotokea baada ya tarehe hii, unafanya eneo husika au kitengo cha uzalishaji kutofikia Viwango vya shirika la Rainforest Alliance, na inaweza kuwa sababu ya kutosajiliwa au kufutiliwa mbali kwa cheti.

Hata hivyo, unyumbulifu fulani unatolewa kwa ajili ya matukio madogo ya ukataji misitu au ubadilishaji ambayo yanaweza kurekebishwa kama ilivyofafanuliwa katika sehemu ya 1.4 hapa chini. Zaidi ya hayo, ubadilishaji mdogo kwa ajili ya usimamizi wa miundombinu unaweza kuruhusiwa na shirika la Rainforest Alliance kufuatia utaratibu wa maombi uliofafanuliwa katika sehemu ya 1.5.

1.3 Utambuzi wa ubadilishaji unaohusishwa na hitaji la 6.1.1

Tathmini ya hatari ya ukataji misitu ya shirika la Rainforest Alliance inatathmini data ya kijiografia iliyopakiwa kutoka kwa Wamiliki wa Vyeti ili kubaini ikiwa kitengo cha shamba kina hatari ya ukataji misitu kuanzia mwaka wa 2014 na kuendelea. Kulingana na asilimia ya eneo la kipande cha shamba linaloingiliana na eneo lililokatwa misitu, viwango vitatu vya hatari vinatengwa: hatari ndogo (kijani) 0%, hatari ya wastani (machungwa) hadi 1.2%, na hatari kubwa (nyekundu) zaidi ya 1.2% ya mwingiliano. Hatari ndogo inachukuliwa kuwa hatari isiyo kubwa saba, ilhali hatari ya wastani na hatari kubwa zinachukuliwa kuwa hatari kubwa.

Tathmini ya hatari ya ukataji misitu inaweza isitofautishe kila wakati kati ya ubadilishaji na mabadiliko yanayokubalika ya matumizi ya ardhi kama yalivyofafanuliwa na shirika la Rainforest Alliance, kama vile:

  • Mashamba ya miti ya kupandwa yanayovunwa na kubadilishwa kwa matumizi ya kilimo lakini hayahusishi ubadilishaji wa mifumo asilia ya ikolojia.

  • Uvunaji wa mti wa kivuli hauhusishi ubadilishaji wa misitu ya asilia.

  • Kupotea kwa uoto wa miti kulikotokea kabla ya tarehe ya kikomo ya mwaka wa 2014.

Wamiliki wa Vyeti lazima watumie matokeo ya tathmini ya hatari ya shirika la Rainforest Alliance ili kubaini maeneo na wanachama wa kikundi walio katika hatari ya kutofikia vigezo, kutathmini hatari hizo, na kuchukua hatua za kuzidhibiti ipasavyo.

Kwa vitengo vya mashamba vinavyokumbwa na hatari kubwa ya ukataji miti (vilivyowekwa katika kundi la hatari ya kati au ya juu), Mmliki wa Cheti anahitajika kufanya ukaguzi wa ndani wa maeneo haya. Ukaguzi huu lazima uthibitishe ikiwa ubadilishaji wowote wa ardhi umetokea kwa kukusanya ushahidi kupitia mahojiano ya wakulima na uchunguzi wa nyanjani. Ushahidi uliokusanywa lazima uhifadhiwe wakati wote na baada ya mchakato wa ukaguzi, na lazima upatikane pindi utakapohitajika na wakaguzi au shirika la Rainforest Alliance. Ushahidi wa kuthibitisha ikiwa ubadilishaji huo ulitokea unaweza kujumuisha:

  • Poligoni za mipaka ya shamba zilizosasishwa, ikiwa zinafaa.

  • Nyaraka zinazoonyesha haki za matumizi ya ardhi au umiliki wa kisheria wa ardhi kwa mujibu wa sheria za kitaifa (k.v., hati miliki za ardhi, haki za kiasili, vibali vya serikali, vyeti, au mbinu za kimila zinazoweza kuthibitishwa).

  • Picha zilizowekwa alama za kijiografia, ramani, au ushahidi mwingine wa kuona.

  • Kumbukumbu za mahojiano ya mkulima, wanajamii, na wadau wengine.

  • Taarifa kutoka kwa mashirika ya serikali za mitaa (k.v., Mashirika ya misitu, Hifadhi za Taifa n.k.).

1.4 Ubadilishaji Mdogo ambao tayari umetokea unaohusishwa na hitaji la 6.1.1

Ikiwa ukaguzi wa ndani kabla ya ukaguzi wa kwanza wa uidhinishaji utabadilishwa, mmiliki wa cheti lazima aangalie ikiwa vimo chini ya viwango vya ubadilishaji mdogo vilivyofafanuliwa hapa na kutekeleza mpango wa urejeshaji kulingana na sehemu ya 1.4.1. Wakati ubadilishaji unapozidi viwango vilivyowekwa, mmiliki wa cheti atamwondoa mwanachama wa kikundi asiyetii, shamba, au kitengo cha shamba kisichofikia vigezo vinavyohitajika, kutoka kwenye mpango wa uidhinishaji. Kwa mashamba yote, ikijumuisha chaguo la EUDR, ubadilishaji lazima uwe umetokea kati ya Januari 1, 2014, na Desemba 31, 2020. Wamiliki wa Vyeti na/au wanachama wa kikundi lazima watimize vigezo hivi vya ziada:

a) Mashamba makubwa na mashamba ya watu binafsi:

Kwa mashamba makubwa (ikijumuisha yale yaliyoidhinishwa kama sehemu ya kikundi) na mashamba ya watu binafsi, ubadilishaji haupaswi kuzidi 1% ya ardhi ya shamba au zaidi ya hekta 10 (popote palipo padogo zaidi).

b) Uidhinishaji wa kikundi

Kwa mashamba madogo katika uidhinishaji wa kikundi, ubadilishaji haupaswi kuzidi 1% ya jumla ya ardhi ya eneo la kipande cha shamba.

Shirika la Rainforest Alliance linahifadhi haki ya kukagua, kuidhinisha, kukataa, au kubatilisha ruhusa hizi kwa Wamiliki wa Vyeti mahususi na kwa msingi wa kila tukio.

1.4.1 Urejeshaji wa Ubadilishaji Mdogo ambao tayari umetokea

Kwa ubadilishaji ulio ndani ya viwango hivi, usimamizi wa shamba lazima uandae mpango wa urejeshaji kwa kushirikiana na mtaalamu wa ikolojia ili kurekebisha msitu au mfumo wa ikolojia uliogeuzwa. Urejeshaji uliopangwa lazima uwe:

  • Uwe na uwiano: Eneo linalotakiwa kurejeshwa lazima liwe na ukubwa unaolingana au zaidi ya eneo lililogeuzwa. Sharti hili linaweza kutimizwa kwa kuondoa eneo lililogeuzwa kwenye uzalishaji na kulirejesha, au kwa kurejesha na/au kutoa manufaa ya fidia ya uhifadhi kwenye eneo lililo karibu.

  • Sawa na: Mfumo wa ikolojia unaotakiwa kurejeshwa lazima uwe sawa na mfumo wa ikolojia wa asili uliopotea katika thamani ya kiikolojia. Ikiwa thamani ya eneo lililorejeshwa ni ndogo au itakuwa ndogo kuliko ile ya eneo lililobadilishwa, basi eneo kubwa zaidi lazima lirejeshwe.

  • Ziada: Shughuli za urejeshaji lazima ziwe za ziada kwa shughuli zilizopangwa kwa sababu zingine, ikiwa ni pamoja na uzingatiaji wa mahitaji ya shirika la Rainforest Alliance kuhusu uoto wa asili.

  • Kudumu: Shughuli za urejeshaji lazima zisanifiwe kwa njia itakayohakikisha uendelevu wa muda mrefu, ikijumuisha ufadhili, majukumu ya usimamizi, na ugawaji wazi wa ardhi pamoja na haki za ardhi.

Zaidi ya hayo, kwa uidhinishaji wa kikundi, yafuatayo lazima yatekelezwe ili kuepuka ubadilishaji zaidi:

  • Uanzishwaji wa mfumo wa adhabu kwa wanachama wa kikundi ili kuzuia ukataji miti zaidi.

  • Utekelezaji wa hatua za kuongeza uelewa au mafunzo kwa wanachama wa kikundi.

  • Ukusanyaji wa poligoni za vipande vya mashamba kwa wanachama wote wa kikundi waliobainika katika tathmini ya hatari kuwa wamo katika hatari kubwa ya ukataji miti.

Uongozi lazima uwasilishe mpango wa urejeshaji kwa shirika la Rainforest Alliance kupitia farmcert@ra.org. Mpango huo lazima ujumuishe:

  • Ufafanuzi wa shughuli zitakazotekelezwa na malengo na majukumu yaliyoainishwa kwa muda maalum.

  • Mpango wa ufuatiliaji wa eneo lililorejeshwa utakaotekelezwa angalau kila baada ya miaka mitatu.

  • Poligoni za eneo/maeneo yanayotakiwa kurejeshwa.

  • Orodha ya spishi za miti itakayopandwa.

  • Wasilisha ripoti za maendeleo kila baada ya miaka mitatu kwa wachunguzi na wakaguzi wa ndani ili kupitia na kuthibitisha ikiwa ziko sawiya na hali halisi ya eneo linalorejeshwa.

Kumbuka: Utekelezaji, ufuatiliaji, na utoaji wa taarifa za michakato ya urejeshaji kwa wakulima wadogo ndani ya kikundi, lazima uwezeshwe na usimamizi wa kikundi. Usimamizi wa kikundi utawajibika ikiwa hatua hizi hazitatekelezwa kwa wanachama wowote wa kikundi walioathirika, jambo ambalo linaweza kusababisha kutoidhinishwa au kufutiliwa mbali kwa cheti.

1.5 Ubadilishaji Mdogo Uliopangwa kwa ajili ya Miundombinu unaounganishwa na hitaji la 6.1.1

Ubadilishaji wa mifumo ya ikolojia ya asili, kufikia 1% ya jumla ya eneo la ardhi lililoidhinishwa, kwa madhumuni ya kudumisha au kupanua miundombinu muhimu kwa shughuli za shamba au usindikaji, unaweza kuruhusiwa chini ya masharti yafuatayo:

  1. Ubadilishaji unaweza kufanyika tu kwa madhumuni ya kuweka miundombinu mipya ya shamba au kukarabati au kuboresha miundombinu iliyopo ya shamba (k.v, barabara au miundombinu ya umwagiliaji, ikijumuisha miundombinu ya umwagiliaji maji, mifereji, mabwawa, hifadhi za maji, na vizuizi vya maji), mitambo ya kudumu, au vifaa vya kuosha, kusindika, au kufungasha.

  2. Usimamizi wa shamba au wa kikundi lazima uandikishe mpango wa usakinishaji mapema, ikijumuisha sababu kwa nini usakinishaji au ukarabati wa miundombinu uliopendekezwa hauwezi kutekelezwa bila kubadilisha eneo husika.

  3. Poligoni za jumla ya ardhi iliyoidhinishwa pamoja na eneo lililobadilishwa hukusanywa ili kuonyesha kuwa eneo la ardhi litakalobadilishwa liko chini ya kiwango kinachoruhusiwa cha 1% ya jumla ya ardhi iliyoidhinishwa. Zingatia: Kiwango cha 1% ni jumla ya eneo lote linaloruhusiwa kuanzia tarehe ya kwanza ya kutuma maombi ya uidhinishaji.

  4. Kabla ya kubadilisha, usimamizi wa shamba au wa kikundi lazima upate idhini kutoka kwa shirika la Rainforest Alliance. Ili kupata idhini, usimamizi utawasilisha mpango kwa farmcert@ra.org ikijumuisha sababu, mpango, na poligoni za eneo linalotakiwa kubadilishwa.

  5. Ubadilishaji huo unatii kikamilifu hitaji la 6.1.2 la Viwango vya shirika la Rainforest Alliance.

  6. Ubadilishaji huo unatii kikamilifu sheria inayotumika.

  7. Ubadilishaji huo unaambatana na sifa au mapendekezo yoyote kuhusu Thamani ya Juu ya Uhifadhi (HCV) yaliyomo kwenye tathmini yoyote ya HCV ya eneo au sehemu hiyo.

  8. Shirika la Rainforest Alliance linahifadhi haki ya kumwomba Mmiliki wa Cheti kutekeleza mpango wa urejeshaji kama ilivyofafanuliwa katika sehemu ya 1.4.1 kwa msingi wa tukio moja baada ya lingine, baada ya kutathmini mpango wa ubadilishaji.

  9. Ruhusa hii haipatikani kwa Wamiliki wa Vyeti wa kakao na kahawa wanaofuata Kanuni ya Umoja wa Ulaya ya Ukataji Misitu (EUDR).

1.6 Kutovamia Maeneo Yaliyohifadhiwa kumeunganishwa na hitaji la 6.1.2

Ili kutathmini hatari ya kutotii hitaji la 6.1.2 la viwango, tathmini ya hatari ya shirika la Rainforest Alliance huamua uwezekano wa kitengo cha shamba kuwa ndani ya eneo lililohifadhiwa au katika maeneo yake maalum ya ulinzi, na ikiwa uzalishaji wa kilimo ndani ya maeneo hayo unaruhusiwa chini ya sheria zinazotumika.

Shirika la Rainforest Alliance, likitumia mfumo wa uainishaji wa maeneo yaliyohifadhiwa wa IUCN, limetenga maeneo ya kwenda na kutoenda. Katika maeneo yaliyohifadhiwa ya “kutoenda”, uzalishaji wa kilimo ni marufuku, ilhali katika maeneo yaliyohifadhiwa ya "kwenda", shughuli za kilimo zinaruhusiwa chini ya masharti maalum na kudhibitiwa na sheria. Kulingana na hili, viwango vitatu vya hatari vimeainishwa: Hatari ya chini (kijani) hakuna mwingiliano na maeneo yaliyohifadhiwa, hatari ya kati (machungwa) mwingiliano na maeneo yaliyohifadhiwa ya "kwenda", na hatari kubwa (nyekundu) mwingiliano na maeneo yaliyohifadhiwa ya "kutoenda".

Ikiwa vitengo vya mashamba vitatambuliwa kuwa na hatari kubwa wakati wa tathmini ya hatari, Wamiliki wa Vyeti lazima watembelee mashamba yote hayo wakati wa ukaguzi wa ndani na kukusanya ushahidi unaoonyesha kwamba uzalishaji haukufanyika ndani ya eneo lililohifadhiwa la 'kutoenda'. Ushahidi huo lazima uhifadhiwe wakati na baada ya ukaguzi, na kupatikana kila unapohitajika na wakaguzi au shirika la Rainforest Alliance. Ushahidi wa kuthibitisha ikiwa uvamizi katika eneo lililohifadhiwa au eneo la kinga umefanyika unaweza kujumuisha:

  • Poligoni zilizorekebishwa za mipaka ya shamba, ikiwa ni muhimu.

  • Nyaraka zinazoonyesha matumizi ya ardhi na/au haki za kisheria kwa mujibu wa sheria za kitaifa.

  • Picha zenye viunganishi vya kijiografia, ramani,au ushahidi mwingine wa picha.

  • Kumbukumbu za mahojiano ya wakulima na wadau wengine.

Vitengo vya mashamba vilivyotambuliwa kuwa na hatari ya kati vitatembelewa na Wamiliki wa Vyeti ili kutathmini ikiwa shughuli za uzalishaji au usindikizaji zilifanyika ndani ya eneo lililohifadhiwa, na ikiwa zinazingatia sheria inayotumika. Angalau, wazalishaji kama hao lazima wawasilishe yafuatayo:

  • Nyaraka zinazoonyesha matumizi ya ardhi na/au haki za kisheria kwa mujibu wa sheria za kitaifa.

Mahitaji kutoka kwa Kiwango cha Kilimo Endelevu

Sehemu hii inatoa maelezo ya ziada kuhusu utekelezaji wa mahitaji mahususi na/au ya uboreshaji endelevu yanayotumika katika Kiwango cha Kilimo Endelevu (SAS) cha shirika la Rainforest Alliance.

2. Maeneo ya uhifadhi na urejeshaji yaliyo nje ya mipaka ya shamba

Sehemu hii inatoa masharti ya kudumisha maeneo ya uhifadhi na/au urejeshaji yaliyo nje ya shamba lililoidhinishwa, yanayohusiana na mahitaji ya maboresho endelevu ya 6.2.3 na 6.2.4 ya Kiwango cha Kilimo Endelevu.

2.1 Masharti ya maeneo ya uhifadhi na urejeshaji yaliyo nje ya shamba lililoidhinishwa yanayohusiana na mahitaji ya 6.2.3 na 6.2.4

Iwapo kufikia asilimia inayohitajika ya uoto wa asili shambani hautawezekana pasipo kupunguza eneo la uzalishaji wa kilimo. Wazalishaji wana fursa ya kuongeza eneo la uoto wa asili wa shambani kwa kutumia maeneo ya uhifadhi au urejeshaji yaliyo nje ya mipaka ya shamba chini ya masharti haya:

  1. Wazalishaji wanaweza kuwa na maeneo ya uhifadhi au urejeshaji nje ya mipaka ya shamba pale tu wanapokuwa hawawezi kufikia asilimia inayohitajika ya uoto wa asili kwenye mashamba yao.

  2. Wazalishaji hawabadilishi uoto wa asili uliopo shambani kuwa matumizi mengine ya ardhi. Maeneo ya uhifadhi yaliyo nje ya mipaka ya shamba yanaweza tu kutumika kukamilisha uoto wa asili uliopo na ule wa ziada wa shambani. Maeneo ya kudumu ya uhifadhi hayawezi kutumika kuchukua nafasi ya uoto wa asili wa shambani.

  3. Wazalishaji wanaweza kuwa na sehemu ya asilimia inayohitajika ya uoto wa asili kwenye mashamba yao, na asilimia ya uoto wa asili kama eneo la uhifadhi nje ya mipaka ya shamba. Kwa mfano, mzalishaji anaweza kuwa na 5% ya uoto wa asili shambani na 5% nje ya shamba.

  4. Eneo la uhifadhi au urejeshaji lililo nje ya mipaka ya shamba lililoidhinishwa linatoa ulinzi thabiti wa muda mrefu wa eneo hilo kwa angalau miaka 25.

  5. Eneo la uhifadhi au urejeshaji nje ya mipaka ya shamba lililoidhinishwa linaleta thamani ya ziada ya uhifadhi na hali ya ulinzi ikilinganishwa na hali iliyopo sasa: eneo hilo linadumishwa au kuboreshwa kulingana na thamani ya bioanuwai.

  6. Eneo la uhifadhi au urejeshaji lililo nje ya mipaka ya shamba lililoidhinishwa lipo katika mfumo wa ikolojia unaofanana na ule wa shamba lililoidhinishwa. Kwa mfano, ikiwa shamba lililoidhinishwa liko katika eneo ambalo msitu wa mvua ndio mfumo mkuu wa ikolojia, eneo la uhifadhi nalo linakuwa katika eneo ambalo msitu wa mvua ndio mkuu.

  7. Wamiliki wa Vyeti watatuma mpango wa uhifadhi au urejeshaji ikijumuisha mahitaji yote kwa shirika la Rainforest Alliance kupitia farmcert@ra.org.

2.2 Masharti ya uwezo wa kukaguliwa kwa maeneo ya uhifadhi na urejeshaji yaliyo nje ya shamba lililoidhinishwa yanayohusiana na mahitaji ya 6.2.3 na 6.2.4

  1. Wamiliki wa Vyeti hutoa data ya poligoni ya eneo au maeneo ya uhifadhi au urejeshaji yaliyo nje ya mipaka ya shamba.

  2. Wamiliki wa Vyeti huonyesha ukubwa (ha) wa eneo/maeneo ya uhifadhi au urejeshaji, pamoja na asilimia ambayo eneo hili linawakilisha kwa kulinganisha na ukubwa wa shamba lililoidhinishwa.

  3. Wamiliki wa Vyeti huonyesha nyaraka zinazothibitisha kwamba eneo/maeneo ya uhifadhi au urejeshaji yanaweza kupewa ulinzi madhubuti wa muda mrefu kwa angalau miaka 25.

  4. Mkaguzi atatembelea eneo la uhifadhi au urejeshaji lililo nje ya mipaka ya shamba angalau mara moja kila baada ya miaka mitatu. Wamiliki wa Vyeti hulipa gharama zozote za ziada za kukagua eneo la uhifadhi au urejeshaji lililo nje ya mipaka ya shamba lililoidhinishwa, kwa mfano, kwa wakaguzi kusafiri hadi eneo/maeneo ya uhifadhi au urejeshaji kwa ajili ya uthibitishaji.

Mahitaji kutoka Kiwango cha Kilimo Rejelevu

Sehemu hii inatoa maelezo ya ziada kuhusu utekelezaji wa mahitaji mahususi na/au ya uboreshaji endelevu yanayotumika tu kwa Kiwango cha Kilimo Rejelevu (RAS) cha shirika la Rainforest Alliance.

3. Uhifadhi na uboreshaji wa mifumo ya asili ya ikolojia na uoto wa asili.

Sehemu hii inawasilisha taarifa muhimu zinazohusiana na utiifu wa hitaji maalum la 6.2.5.

3.1 Udumishaji wa uoto wa miti ya asili unahusiana na hitaji maalum la 6.2.5

Mahitaji yafuatayo ya ziada lazima yatimizwe.

Mahitaji mahususi kwa mazao

Chai

Wazalishaji hudumisha angalau spishi tatu za miti ya asili, na wazalishaji hufuata mapendekezo ya kitaifa kuhusu spishi za miti na msongamano wake..

Taarifa nyinginezo

Tarehe ya kwanza ya kuchapishwa kwa hati hii (v 1.0): Julai 1, 2022.

Nyaraka zilizotajwa kuwa "zinazofunganisha" lazima zizingatiwe ili kupata uthibitisho. Nyaraka zinazotajwa kama "zisizo funganisha" hutoa taarifa zisizo za lazima ili kuwasaidia wasomaji kuelewa na kutekeleza masharti pamoja na maudhui mengine yanayolazimisha.

Kanusho la Tafsiri

Kwa swali lolote linalohusiana na maana sahili ya taarifa katika tafsiri, rejelea toleo rasmi la Kiingereza kwa ajili ya ufafanuzi. Makosa yoyote au tofauti za maana zinazotokana na tafsiri hii, hazina nguvu ya kisheria na hazitakuwa na athari yoyote kwa madhumuni ya ukaguzi au uthibitishaji.

Unakili, urekebishaji, usambazaji, au uchapishaji upya wa maudhui haya ni marufuku kabisa bila idhini ya maandishi ya awali kutoka kwa shirika la Rainforest Alliance.

Taarifa zaidi?

Kwa msaada wa kupata cheti cha shirika la Rainforest Alliance, wasiliana na timu yetu ya Mafanikio ya Wateja kupitia customersuccess@ra.org

Kwa taarifa zaidi kuhusu shirika la Rainforest Alliance, tembelea http://www.rainforest-alliance.org wasiliana kupitia info@ra.org au Ofisi ya shirika la Rainforest Alliance Amsterdam, De Ruijterkade 6, 1013AA Amsterdam, Uholanzi.