
Kichwa: | Kiambatisho cha Ufuatiliaji | |
Msimbo: | A-05-SRCL-B-CH | |
Toleo: | 1.4 | |
Inatumika kwa: | Wamiliki wa Vyeti vya Kilimo na Mnyororo wa Ugavi | |
Utekelezaji: | Maudhui ya kuunganisha | |
Kuanzia: | Machi 1, 2026 | |
Inakamilika ifikapo: | Hadi itakapotangazwa vinginevyo | |
Imechapishwa mnamo: | Septemba 8, 2025 | |
Imeunganishwa na: | A-1-S-B-F-V1.4 Kiwango cha Kilimo Endelevu cha shirika la Rainforest Alliance. A-33-R-B-FA-V1.0 Kiwango cha Kilimo Rejelevu cha shirika la Rainforest Alliance. A-35-SRCL-B-SC_V1.5EN_Mahitaji ya Mnyororo wa ugavi ya shirika la Rainforest Alliance | |
Inachukua nafasi ya: | ||
Hati hii inahusu nini?
Kiambatisho hiki kinajumuisha maudhui ya ziada yenye masharti ya lazima yanayohusiana na matakwa yaliyo katika Sura ya Ufuatiliaji wa viwango vya shirika la Rainforest Alliance na Mahitaji ya Mnyororo wa Ugavi ya shirika la Rainforest Alliance.
Hati hii inajumuisha:
Maelezo ya ziada kuhusu wahusika wanaowajibika kwa ufuatiliaji.
Maelezo ya ziada kuhusu ufafanuzi wa chaguo mbalimbali za ufuatiliaji.
Lini na jinsi ya kutumia hati hii?
Hati hii inawapa Wamiliki wa Vyeti na Mashirika ya Uidhinishaji taarifa ya ziada kuhusu mahitaji ya msingi yaliyo katika viwango vya Mashamba na Masharti ya Mnyororo wa Ugavi, pamoja na mwongozo wa utekelezaji.
Mabadiliko katika toleo lililosasishwa kutoka v1.3 hadi v1.4
Sehemu | Nini kimebadilika |
Katika Hati nzima | Kuongezwa kwa Kiwango cha Kilimo Rejelevu |
2.2.1 | Ufuatiliaji unahitajika kupitia mtengenezaji wa bidhaa iliyokamilika badala ya chapa/muuzaji wa rejareja. |
1. Utangulizi
Hati hii yenye masharti ya lazima inawapa Wamiliki wa Cheti (CHs) taarifa kuhusu utekelezaji wa masharti ya Ufuatiliaji ya Mahitaji ya Mnyororo wa Ugavi ya shirika la Rainforest Alliance kwa kiasi kinachohusiana na Kiwango cha Kilimo Endelevu cha shirika la Rainforest Alliance na Kiwango cha Kilimo Rejelevu.
Maelezo zaidi kuhusu utekelezaji wa kanuni na mahitaji yanaweza kupatikana katika Mwongozo wa Ufuatiliaji wa shirika la Rainforest Alliance.
Wigo na utumikaji wa mahitaji ya ufuatiliaji
Ufuatiliaji huhakikisha mtiririko na ukamilifu wa bidhaa zinazouzwa kama Zilizoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance, na kuthibitisha usahihi wa madai ya uidhinishaji. Wamiliki wote wa vyeti vya mashamba na wa mnyororo wa ugavi lazima wafuate mahitaji ya lazima yaliyo katika orodha ya uhakiki iliyowekwa kulingana na muktadha baada ya kujisajili katika Mfumo wa Uidhinishaji wa shirika la Rainforest Alliance (RACP).
Aina za ufuatiliaji
Aina zifuatazo za ufuatiliaji zinapatikana katika minyororo ya ugavi iliyoidhinishwa, zimeorodheshwa kutoka "ya juu zaidi" hadi "ya chini zaidi": Utambulisho Uliohifadhiwa (IP), Utenganishaji (SG), na Mizani ya Misa (MB).
Utambulisho Uliohifadhiwa (IP)
Hii ndiyo aina ya ufuatiliaji yenye masharti makali zaidi, ambapo bidhaa iliyoidhinishwa inaweza kufuatiliwa hadi kwa Mmiliki wa Cheti wa shamba. Hakuna kuchanganya bidhaa iliyoidhinishwa na bidhaa isiyoidhinishwa, au na bidhaa iliyoidhinishwa kutoka vyanzo tofauti.
Ikiwa bidhaa iliyoidhinishwa inatoka katika vyanzo/mashamba mbalimbali yaliyoidhinishwa, lakini utambulisho wake umehifadhiwa, aina ndogo ya Utambulisho Mseto Uliohifadhiwa (Mixed IP) inaweza kutumika.
Kwa aina hii ya ufuatiliaji wa bidhaa, bidhaa zilizoidhinishwa hutenganishwa na bidhaa zisizoidhinishwa, kimwili na katika nyaraka. Utenganishaji hufanyika katika hatua zote za mnyororo wa ugavi (upokeaji, uchakataji, ufungashaji, uhifadhi, na usafirishaji). Hii inamaanisha kuwa bidhaa imeidhinishwa kikamilifu, ingawa utambulisho wa chanzo au vyanzo vyake haujulikani.
Mizani ya Misa (MB)
Mizani ya Misa ni aina ya ufuatiliaji wa kiutawala ambapo bidhaa zilizoidhinishwa na zisizoidhinishwa zinaweza kuchanganywa. Hata hivyo, kiasi kinachouzwa kama kilichoidhinishwa hakiwezi kuzidi kiasi kilichonunuliwa awali kama kilichoidhinishwa. Mmiliki wa Cheti (CH) wa mnyororo wa ugavi lazima aandike kumbukumbu ya pembejeo na matokeo yote yaliyoidhinishwa na yasiyoidhinishwa na kuhakikisha kuwa mauzo ya kiasi kilichoidhinishwa yanaakisiwa kwa usahihi katika jukwaa la ufuatiliaji bidhaa.
Maboresho kutoka aina moja ya ufuatiliaji wa bidhaa hadi nyingine hayawezekani. Kwa mfano, bidhaa iliyonunuliwa kwa mfumo wa Utenganishaji haiwezi kuuzwa kama bidhaa yenye Utambulisho Uliohifadhiwa. Hata hivyo, kushusha kutoka aina ya juu ya ufuatiliaji hadi ya chini, kama vile kutoka Utenganishaji hadi Mizani ya Misa, kunaruhusiwa.
Wigo wa aina za ufuatiliaji
Utambulisho Uliohifadhiwa unaweza kutumika kwa zao lolote lililo ndani ya wigo wa uidhinishaji wa shirika la Rainforest Alliance.
Utenganishaji unaweza pia kutumika kwa zao lolote lililo ndani ya wigo wa uidhinishaji, lakini sio kwa Wamiliki wa Vyeti (CHs) wa mashamba.
Mizani ya Misa inaweza kutumika kwa mazao yafuatayo na Wamiliki wa Vyeti (CHs) wa mnyororo wa ugavi: kakao, matunda yaliyosindikwa (ikiwemo juisi ya machungwa), hazelnati, korosho, lozi, mafuta ya nazi, maua[1], pamoja na mimea na viungo muhimu[2]. Wamiliki wa Vyeti wa mashamba wanaweza kutumia aina ya ufuatiliaji ya Mizani ya Misa kwa hazelnati, korosho, lozi, mafuta ya nazi na maua pekee.
2. Ufuatiliaji wa bidhaa
Sharti 2.1.1 Mnyororo wa Ugavi, 2.1.3 Shamba – Utenganishaji
Shirika la Rainforest Alliance limeanzisha vigezo tofauti katika kiwango cha Shamba. Mashamba na vikundi vya Mnyororo wa Ugavi vilivyoidhinishwa na kushughulikia kiasi cha mazao kutoka katika Viwango tofauti vya shirika la Rainforest Alliance lazima vitenganishe kimwili kiasi hicho cha mazao katika hatua zote, ikiwemo uvunaji, uhifadhi, usafirishaji, uchakataji na ufungashaji.
Kiasi cha bidhaa kilichoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance lazima pia kitenganishwe na kiasi kilichoidhinishwa chini ya mfumo mwingine au kiasi cha bidhaa ambacho hakijaidhinishwa.
Sharti 2.1.4 Mnyororo wa Ugavi, 2.1.5 Nyaraka za Shamba
Nyaraka za bidhaa zinazoingia na zinazotoka lazima zijumuishe marejeleo ya kiasi cha bidhaa kilichoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance, pamoja na Kiwango cha shirika la Rainforest Alliance ambacho kiasi hicho kinahusishwa nacho. Kwa mfano, Kiwango cha Kilimo Endelevu au Kiwango cha Kilimo Rejelevu.
Sharti la 2.1.6 Mnyororo wa Ugavi, Sharti la 2.1.7 Shamba - Uuzaji maradufu
Uuzaji Maradufu unamaanisha kitendo cha kuuza kiasi kilekile cha bidhaa iliyoidhinishwa mara mbili. Mara moja chini ya Kiwango cha shirika la Rainforest Alliance, na tena chini ya Kiwango kingine cha shirika la Rainforest Alliance, mfumo mwingine wa uidhinishaji, au kama bidhaa ya kawaida. Uuzaji maradufu hauruhusiwi.
Kwa mfano, tani 100 za kahawa zilizozalishwa na shamba zinaweza kuthibitishwa kuwa za kilimo hai (organic) na pia chini ya Kiwango cha Kilimo Endelevu cha shirika la Rainforest Alliance na kuuzwa kama:
Tani 100 za kahawa zilizothibitishwa tu chini ya Kiwango cha Kilimo Endelevu cha shirika la Rainforest Alliance, au
Tani 100 za zao ya kilimo hai pekee, au
Tani 100 za mazao yaliyothibitishwa kuambatana na Kiwango cha Kilimo Endelevu cha shirika la Rainforest Alliance na kilimo hai (mara moja kwa kundi moja) kwa mnunuzi mmoja.
Hata hivyo, kiasi hicho hicho cha kahawa hakiwezi kuuzwa kama tani 100 za kahawa ya kilimo hai, pamoja na pia tani 100 za kahawa iliyothibitishwa chini ya Kiwango cha Kilimo Endelevu cha shirika la Rainforest Alliance au Kilimo Rejelevu.
3. Ufuatiliaji katika jukwaa la mtandaoni
Jukwaa la Ufuatiliaji bidhaa la shirika la Rainforest Alliance linaonyesha mzunguko wa bidhaa iliyoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance katika mnyororo mzima wa ugavi na linatekelezwa katika kiwango cha Mmiliki wa cheti (CH). Kiasi cha bidhaa katika jukwaa la ufuatiliaji kitaonyesha kiasi cha bidhaa kilicho chini ya Kiwango cha Kilimo Endelevu au cha Kilimo Rejelevu cha shirika la Rainforest Alliance, au vyote viwili. Kwa Wamiliki wa Vyeti (CH) wanaomiliki sehemu nyingi, eneo la usimamizi mkuu ndilo linalowajibikia mahitaji ya ufuatiliaji. Kwa ujumla, ufuatiliaji hufuata umiliki wa kisheria. Ufuatiliaji hauhitajiki kwa usafirishaji wa bidhaa zilizoidhinishwa kati ya maeneo yaliyojumuishwa kwenye cheti kimoja.
Shughuli za kuripoti katika jukwaa zinajumuisha mauzo, ubadilishaji, uthibitishaji, uchanganyaji, ukomboaji, uondoaji na kushusha daraja kwa bidhaa iliyoidhinishwa.
Sharti 2.1.2 Mnyororo wa Ugavi, 2.1.9 Shamba– ubadilishaji wa bidhaa iliyoidhinishwa
Kwa shughuli kama vile uchakataji zinazobadilisha kiasi cha bidhaa iliyoidhinishwa (kwa mfano kutoka kahawa mbichi hadi iliyokaangwa), Mumiliki wa Cheti (CH) mwenye mnyororo wa ugavi lazima atekeleze kazi ya ‘ubadilishaji’ katika jukwaa la ufuatiliaji kabla ya kuuza bidhaa hiyo mbele. Kwa shughuli kama vile utengenezaji zinazosababisha bidhaa tofauti (kwa mfano bidhaa yenye viambato vingi), lakini bila kubadilisha kiasi cha bidhaa, Mumiliki wa Cheti (CH) wa mnyororo wa ugavi lazima atekeleze ‘taarifa ya utengenezaji’ katika jukwaa la ufuatiliaji kabla ya kuuza bidhaa hiyo kwa mhusika anayefuata katika mnyororo wa ugavi.
Kwa kiasi cha bidhaa ambacho hakihitaji kuuzwa kwa mhusika anayefuata kupitia jukwaa la ufuatiliaji na ambacho kinahitaji kukombolewa na Mumiliki wa Cheti (CH) wa mnyororo wa ugavi, shughuli hizi hazihitaji kufanywa kabla ya kukomboa kiasi hicho, (angalia viwango vya ubadilishaji katika Sehemu ya 5). Kwa ufuatiliaji wa hiari mwishoni mwa mnyororo wa ugavi (yaani, ufuatiliaji hadi kwenye maduka ya rejareja), shughuli hizi pia hazihitaji kufanywa kabla ya kuuza.
Sharti la 2.1.4 Mnyororo wa Ugavi, Sharti la 2.1.5 Shamba – kusimamia miamala inayoingia ya bidhaa iliyoidhinishwa
Miamala ya bidhaa zilizoidhinishwa zinazouzwa na wasambazaji lazima ikaguliwe na kuthibitishwa[3] na Mumiliki wa Cheti (CH) anayenunua bidhaa hiyo iliyoidhinishwa.
Sharti la 2.2.1 Mnyororo wa Ugavi na Shamba – kusimamia miamala inayotoka ya bidhaa iliyoidhinishwa
Miamala yote ya bidhaa zilizoidhinishwa lazima iripotiwe kwenye jukwaa la ufuatiliaji la shirika la Rainforest Alliance, kuanzia kwa Mumiliki wa Cheti (CH) wa shamba hadi kwa mtengenezaji wa mwisho wa bidhaa tayari kwa matumizi ya mtumiaji (au mwagizaji wa matunda na mboga mboga)). Kiasi kinachouzwa kama bidhaa za mwisho kwa mtumiaji lazima zikombolewe4 kutoka kwenye jukwaa la ufuatiliaji.
Kuondoa Kiasi cha bidhaa Iliyoidhinishwa
Kiasi cha bidhaa kilichoidhinishwa ambacho hakijauzwa kama bidhaa iliyoidhinishwa (iwe kama cha kawaida, kama bidhaa iliyoidhinishwa na mfumo mwingine wa uidhinishaji, au bidhaa iliyoharibika au kupotea) lazima kiondolewe kutoka kwenye jukwaa la ufuatiliaji. Kiasi cha bidhaa kinachohusishwa na mfumo wa mizani ya misa hakihitajiki kuondolewa kwenye jukwaa la ufuatiliaji bidhaa, na muamala wa mauzo unapaswa kutolewa kwa mnunuzi (ikiwa inatumika) pindi kiasi husika cha bidhaa iliyoidhinishwa, chenye thamani sawa, kitakapokuwa kimeuzwa.
Wakati wa Kuripoti
Shughuli zote lazima ziripotiwe katika jukwaa la ufuatiliaji ndani ya wiki 2 kuanzia mwisho wa robo ya kalenda (Januari – Machi, Aprili – Juni, Julai – Septemba, Oktoba – Desemba) ambapo shughuli hizo zilifanyika.
Mfano 1: Mauzo ya kimwili yanafanyika mwezi Mei - Mumiliki wa Cheti (CH) lazima aripoti muamala wa mauzo kufikia tarehe Julai 14.
Mfano 2: Kiasi cha bidhaa kilichoidhinishwa kinachouzwa kama bidhaa ya kawaida mwezi Desemba lazima kiondolewe kwenye jukwaa la ufuatiliaji ifikapo Januari 14 ya mwaka unaofuata.
Iwapo Mmiliki wa Cheti (CH) wa mnyororo wa ugavi hawezi kutangaza mauzo ya bidhaa iliyoidhinishwa kwa mnunuzi wake ndani ya muda unaohitajika kwa sababu msambazaji wa CH bado hajatangaza mauzo hayo kwake, CH anahitaji kuonyesha kwamba amechukua hatua stahiki za kumfuatilia na kuwasiliana na msambazaji wake.
Sharti la 2.2.2 Mnyororo wa Ugavi, Sharti la 2.2.4 Shamba – Ada ya Mrabaha
Kwa mujibu wa Sheria na Masharti ya Jumla ya Mkataba wetu wa Leseni wa shirika la Rainforest Alliance, Wamiliki wa Vyeti (CHs) lazima walipe ada ya Mrabaha kulingana na Ratiba ya Mrabaha, kwa kila zao na kiwango kinachohusika.
4. Usawa wa kiasi cha bidhaa
Sharti la 2.3.1 Mnyororo wa Ugavi na Shamba – ubadilishaji wa kiasi cha bidhaa
Kulingana na kanuni zetu za Mizani ya Misa, kubadilisha kiasi cha bidhaa iliyoidhinishwa kuwa kiasi cha bidhaa ya kawaida, kunaruhusiwa tu kwa bidhaa zilezile au kwa kufuata mwelekeo wa uchakataji wa kimwili, kwa mfano:
Siagi ya kakao iliyoidhinishwa kuwa siagi ya kakao ya kawaida
Kokwa za kakao zilizoidhinishwa kuwa siagi ya kakao ya kawaida
Karanga za hazelnati zilizoidhinishwa zikiwa ziko kwenye ganda kuwa punje za hazelnati zilizokaangwa za kawaida
Mafuta ghafi ya nazi yaliyothibitishwa kuwa mafuta yaliyosafishwa ya nazi ya kawaida
Ubadilishaji wa kurudi nyuma hauruhusiwi, kwa mfano:
Kakao iliyosagwa kuwa vipande vya kakao vya kawaida vilivyoidhinishwa
Chokoleti iliyoidhinishwa kuwa siagi ya kakao ya kawaida
Siagi ya kakao iliyoidhinishwa kuwa unga wa kakao wa kawaida
Punje za hazelnati zilizochakatwa kuwa hazelnati zilizo ndani ya maganda
Mahitaji 2.3.4 na 2.3.5: Mnyororo wa Ugavi na Shamba – ulinganishaji wa asili
Kwa sekta ya kakao, mahitaji na ufafanuzi ufuatao kuhusu ulinganifu wa asili hutumika:
Ufafanuzi
Kiasi cha kila mwaka | Jumla ya kiasi mauzo halisi ya kakao iliyosagwa iliyoidhinishwa, kwa kuzingatia asili yake, katika kipindi cha miezi 12. |
Asili | Nchi ambako kokwa za kakao zilizoidhinishwa zilizalishwa. |
Alama ya asili | Nchi ya asili ya Mumiliki wa Cheti (CH) wa shamba kwa kiasi cha kakao kilichoidhinishwa katika jukwaa la ufuatiliaji. |
Ulinganifu wa asili | Wakati kiasi cha kakao kilichoidhinishwa kinaponunuliwa, ili kuuza kiasi kinacholingana cha kakao ya kawaida kama iliyoidhinishwa, asili ya kiasi hicho cha bidhaa zote mbili lazima iwe sawa (kwa kila muamala au kwa msingi wa jumla). |
Mpango wa upatikanaji | Mpango wa kutekeleza mabadiliko katika upatikanaji wa bidhaa zilizoidhinishwa ili kutimiza mahitaji ya ulinganifu wa asili. Mpango huu lazima uwasilishwe kwa shirika la Rainforest Alliance na kuidhinishwa nao. |
Wigo
Ulinganifu wa asili unahitajika kwa miamala yote iliyokamilishwa katika jukwaa la ufuatiliaji mfumo wa ufuatiliaji kwa mikataba iliyotiwa saini kuanzia Aprili 1, 2021, kwa mahitaji ya awamu ya 1, na kuanzia Oktoba 1, 2023 kwa mahitaji ya awamu ya 2.
Hii inajumuisha bidhaa zote za kakao zilizoidhinishwa chini ya mfumo wa mizani ya misa ambazo zina alama ya asili iliyoonyeshwa katika jukwaa la ufuatiliaji.
Mahitaji ya awamu ya 1
Kokwa za kakao na vipande vyake
Ulinganifu wa asili unahitajika kwa 100% ya kila muamala wa ununuzi na mauzo ya kokwa na vipande vya kakao vilivyoidhinishwa kati ya Wamiliki wa Vyeti (CHs) wa mnyororo wa ugavi. Nyaraka za ununuzi na mauzo za kokwa na vipande vya kakao vinavyouzwa kama vilivyoidhinishwa lazima zijumuishe taarifa za asili hadi kiwango cha nchi kwa kokwa na vipande vya kakao vilivyoidhinishwa na vya kawaida.
Kakao iliyosagwa
Ulinganifu wa asili unahitajika kwa mauzo ya kwanza ya kakao iliyosagwa iliyoidhinishwa katika mnyororo wa ugavi, kwa msingi wa jumla kwa kila kipindi cha miezi 12. Kampuni lazima zihesabu kiasi chao cha mwaka kwa ajili ya ulinganifu wa asili wa kakao iliyosagwa iliyoidhinishwa chini ya Mizani ya Misa na zijumuishe uthibitisho wa hesabu hiyo. Nyaraka katika mnyororo wa ugavi wa kiwango cha Mmiliki wa Cheti lazima zijumuishe taarifa za asili hadi kiwango cha nchi kwa pembejeo za kakao zilizoidhinishwa na zisizoidhinishwa.
Asili za mauzo ya jumla ya kakao iliyosagwa iliyoidhinishwa na kiasi cha kila mwaka hulinganishwa, huku ulinganifu wa asili ukihitajika kwa angalau 80% ya kiasi cha bidhaa.
Iwapo ulinganifu wa asili ni chini ya 80% katika kipindi cha miezi 12, pengo la kiasi cha bidhaa lazima lijazwe ndani ya miezi 3 inayofuata.
Mahitaji ya awamu ya 2
Mauzo ya nje kutoka Côte d’Ivoire, Ghana, Ecuador
Mbali na mahitaji yote ya awamu ya 1, ulinganifu wa asili unahitajika kwa 100% ya kila mauzo ya nje ya kakao iliyosagwa, siagi ya kakao au unga wa kakao ulioidhinishwa, kutoka nchi ya asili (kwa Côte d’Ivoire, Ghana na Ecuador). Ulinganifu wa asili kwa Mumiliki wa Cheti (CH) yeyote wa mnyororo wa ugavi aliye katika kiwango zaidi ya kile cha mwagizaji, hauhitajiki.
Mbinu ya kikanda ya asili
Ulinganifu wa asili unaweza kufanywa kwa kiwango cha kikanda kwa bidhaa zote isipokuwa kokwa na vipande vya kakao, kwa kuunganisha nchi mahususi ndogo za asili, kama ilivyoainishwa katika jedwali hapa chini:
Kanda | Nchi | Vighairi |
Afrika Magharibi | Guinea, Liberia, Togo, Sierra Leone, au nchi nyingine za Afrika Magharibi | Haijajumuishwa: Kameruni, Côte d’Ivoire, Ghana, Nigeria, Madagaska, au nchi zilizoorodheshwa chini ya Afrika ya Kati na Mashariki |
Afrika ya Kati na Mashariki | Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Guinea ya Ikweta, Gaboni, Sao Tome na Principe, Tanzania, Uganda | Haijajumuishwa: Kameruni, Madagaska |
Amerika ya Kusini na Kati | Belize, Bolivia, Kosta Rika, Kuba, Dominika, Grenada, Guatemala, Haiti, Hondurasi, Jamaika, Meksiko, Nikaragua, Panama, Santa Lucia, Trinidad na Tobago, Venezuela, au nchi nyingine za Amerika ya Kusini na Kati | Haijajumuishwa: Brazili, Kolombia, Jamhuri ya Dominika, Ekuado, Peru |
Asia na Oceania | Fiji, India, Malaysia, Papua Guinea Mpya, Ufilipino, Visiwa vya Solomon, Sri Lanka, Thailand, Vanuatu, Vietnam, au nchi nyingine za Asia na Oceania | Haijajumuishwa: Indonesia |
5. Viwango vya ubadilishaji kwa bidhaa za Mizani ya Misa
Jedwali hapa chini linaonyesha viwango vya ubadilishaji kwa Mizani ya Misa katika sekta ambazo mfumo huu unaruhusiwa. Viwango vinavyoruhusiwa vya ubadilishaji kwa Kutenganisha na Kuhifadhi Utambulisho vimewekwa awali katika Jukwaa la ufuatiliaji.
Zao/Sekta | Kigezo cha ubadilishaji |
Kakao | |
Kokwa hadi kakao iliyosagwa | 1:0.82 |
Kokwa hadi vipande vya kakao | 1:0.82 |
Vipande vya kakao hadi kakao iliyosagwa | 1:1 |
Kakao iliyosagwa hadi siagi na unga wa kakao Bidhaa ya kakao yenye viambato vingi (kiwango cha kakao) hadi bidhaa ya kakao yenye viambato vingi (kiwango cha kakao) | 1:0.5:0.5 1:1 |
Hazelnati | |
Zikiwa na punje hadi kokwa | 1:0.5 |
Punje hadi punje zilizokaangwa | 1:0.94 |
Punje hadi punje zilizosindikwa (k.m. zilizokaushwa kwa maji ya moto, zilizokatwa vipande, zilizokatwa vipande vyembamba, n.k.) | 1:1 |
Kokwa zilizokaangwa hadi punje zilizokaangwa na kusindikwa | 1:1 |
Nazi | |
Matunda mabichi hadi kopra | 1:0.25 |
Kopra hadi mafuta ghafi ya nazi | 1:0.62 |
Mafuta ghafi ya nazi hadi mafuta yaliyosafishwa ya nazi (RBD) | 1:0.96 |
Mafuta ghafi ya nazi hadi mafuta yaliyosafishwa ya nazi (yaliyotiwa hidrojeni) | 1:0.96 |
Korosho & Lozi | |
Zikiwa na punje hadi kokwa | 1:0.25 |
Punje hadi punje zilizosindikwa | 1:0.95 |
Punje hadi punje zilizokaangwa | 1:0.95 |
Kokwa hadi rojo ya punje | 1:1 |
Kokwa zilizokaangwa hadi punje zilizokaangwa na kusindikwa | 1:0.95 |
Punje zilizokaanngwa hadi rojo ya punje | 1:1 |
Taarifa nyinginezo
Tarehe ya kwanza ya kuchapishwa kwa hati hii (v 1.0): Julai 1, 2022.
Shirika la Rainforest Alliance linahifadhi haki ya kukagua, kuidhinisha, kukataa, au kubatilisha ruhusa hizi kwa Wamiliki wa Vyeti (CHs) mahususi na kwa kuzingatia kila kesi kivyake.
Nyaraka zilizotajwa kuwa "zinazofunganisha" lazima zizingatiwe ili kupata uthibitisho. Nyaraka zinazotajwa kama "zisizo funganisha" hutoa taarifa zisizo za lazima ili kuwasaidia wasomaji kuelewa na kutekeleza masharti pamoja na maudhui mengine yanayolazimisha.
Kanusho la Tafsiri
Kwa swali lolote linalohusiana na maana kamili ya taarifa katika tafsiri, tafadhali rejelea toleo rasmi la Kiingereza kwa ufafanuzi. Makosa yoyote au tofauti za maana zinazotokana na tafsiri, hazilazishi na hazina athari kwa madhumuni ya ukaguzi au uthibitisho.
Unakili, urekebishaji, usambazaji, au uchapishaji upya wa maudhui haya ni marufuku kabisa bila idhini ya maandishi ya awali kutoka kwa shirika la Rainforest Alliance.
Taarifa zaidi?
Kwa msaada wa kupata cheti cha shirika la Rainforest Alliance, wasiliana na timu yetu ya Huduma kwa Wateja kupitia customersuccess@ra.org.
Kwa taarifa zaidi kuhusu shirika la Rainforest Alliance, tembelea http://www.rainforest-alliance.org wasiliana kupitia info@ra.org au Ofisi ya shirika la Rainforest Alliance Amsterdam, De Ruijterkade 6, 1013AA Amsterdam, Uholanzi.
Futnodi
Kwa maua, ufuatiliaji kwa kutumia mizani ya misa hufanywa kwa kuzingatia idadi ya pembejeo zilizoidhinishwa (mashina) ambazo mmiliki wa cheti (CH) hupokea katika kipindi fulani (siku/wiki/mwaka) na humruhusu CH kudai asilimia ya pembejeo zilizoidhinishwa katika bidhaa yake ya mwisho. ↑
Mimea ya viungo na vikolezo muhimu ni rooibos, vanilla, zafarani, pilipili, mdalasini, pilipili kali, oregano, giligilani, paprika, iliki, bizari, karafuu, kotimiri, kungumanga, thyme, jani la mpera, rosemary na tarragon. ↑
Thibitisha = Mumiliki wa (CH) hukagua na kuidhinisha maelezo (kiasi, kiwango cha ufuatiliaji, na marejeleo mengine yoyote yaliyotolewa) ya miamala inayoingia kutoka kwa wasambazaji walioidhinishwa, iwapo maelezo hayo yanalingana na yale yaliyo kwenye ankara na mikataba na wasambazaji wao
Komboa = Mmiliki wa cheti anayemiliki chapa hufuatilia kiasi cha bidhaa kutoka kwenye jukwaa la ufuatiliaji, ambacho kinauzwa kama bidhaa za mwisho zinazoelekezwa kwa mtumiaji. Shughuli ya 'kukomboa' inaashiria mwisho wa ufuatiliaji wa mtandaoni kwa bidhaa zilizoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance. ↑