
Kichwa: | Nyongeza ya Faharasa (Faharasa ya Msamiati) |
Msimbo: | A-03-SCRL-B-CH |
Toleo: | 1.5 |
Inatumika kwa: | Wamiliki wa Vyeti vya Kilimo na Mnyororo wa Ugavi |
Utekelezaji: | Maudhui ya kuunganisha (Maudhui yanayofungamana kisheria) |
Kuanzia: | Machi 1, 2026 |
Inamalizika ifikapo: (Inakamilika kufikia:) | Hadi itakapotangazwa vinginevyo |
Imechapishwa mnamo: | Septemba 23, 2025 |
Imeunganishwa na: | Viwango vya shirika la Rainforest Alliance na Mahitaji ya Mnyororo wa Ugavi, viambatisho vyote husika, uthibitisho, kanuni za ukaguzi na nyaraka za uhakikisho zinazofungamana kisheria. |
Huchukua nafasi ya: |
Hati hii inahusu nini?
Kiambatisho hiki kinatoa kamusi ya istilahi zinazotumika katika Mpango wa Uthibitisho wa shirika la Rainfrorest Alliance. Masharti yote katika viwango vya shirika la Rainforest Alliance, Mahitaji ya Mnyororo wa Ugavi na nyaraka husika yamejumuishwa katika kamusi hii ya istilahi. Pia, maelezo ya istilahi katika nyaraka za uhakikisho kisheria, zimejumuishwa.
Lini na jinsi ya kutumia hati hii?
Hati hii imekusudiwa Wamiliki wa Vyeti, Mamlaka ya Uthibitishaji, na wadau wote ili kuhakikisha uelewa thabiti wa istilahi zilizopo katika muktadha wa shirika la Rainforest Alliance.
Mabadiliko muhimu katika sasisho kutoka v1.4 hadi v1.5
Mada | Nini kimebadilika |
Vifafanuzi vilivyosasishwa | Ufafanuzi wa istilahi zifuatazo ulisasishwa ili kuongeza uwazi: Kiambato hai, kemikali za kilimo, kilimo-misitu, mboji, uuzaji mara mbili, mbolea, dawa ya fangasi, dawa ya magugu, nyumbani, utambulisho uliohifadhiwa, mbolea isiyo ya kikaboni, dawa ya wadudu, Udhibiti shirikishi wa Wadudu (IPM), Viwango vya Juu vya Masalio (MRLs), mimea asilia, maadui wa asili, dawa za kuua wadudu zilizopitwa na wakati, Vifaa vya Kujikinga (PPE), wadudu, dawa ya kuua wadudu, bei ya juu, ufufuaji wa mazao, urekebishaji wa mazao, Muda wa Marufuku ya Kuingia Shambani (REI), bafa ya kingo za mito, dawa ya kuua panya, mrabaha, mti wa kivuli, usambaaji wa dawa ya kunyunyizwa kwa upepo na wanyama pori waharibifu. |
Istilahi mpya zilizoongezwa na ufafanuzi wake | Istilahi zifuatazo zinazohusiana na kilimo rejelevu, pamoja na ufafanuzi wake, zimeongezwa: Bioanuwai, viambajengo vya kibiolojia, mimea funikizi, idadi ya nyungunyungu ardhini, ukataji wa nyasi unaozingatia ikolojia, athari za kiuchumi za wadudu/magonjwa, afya ya mfumo ikolojia, mpango wa matumizi ya mbolea, tathmini ya hali ya majani ya mimea, uunganishaji miche ya mimea, mikanda ya kijani, Udhibiti Shirikishi wa Magugu (IWM), viashiria vya mikrobiolojia, mikrobiota, hesabu ya vidubini, matandazo, mfuniko wa mimea asili ya miti, miti inayounda nitrojeni, vyanzo vya virutubisho vya asili, kilimo rejelevu, uhuishaji wa mazao, aina ya mmea sugu, maji yanayotiririka, mbolea ya kutoa virutubisho polepole, magugu laini, viashiria vya afya ya udongo, maada hai ya udongo (SOM), ungóaji mashina ya miti, mbolea ya kemikali, aina ya mmea stahimilivu, uathirifu wa sumu ya viuatilifu, uvukizi wa kemikali za udongo, mvukizo na vizuia upepo. |
Istilai zilizofutwa | Istilai zifuatazo zimepitwa na wakati na zimefutwa: Tofauti ya Uendelevu (SD) na Uwekezaji wa Uendelevu (SI). |
A
Ada ya uajiri | Ada yoyote au gharama zinazohusiana na mchakato wa uajiri, zinazotumika ili wafanyakazi wapate ajira au nafasi ya kazi, pasipo kujali namna, muda, au mahali zinapotozwa au kukusanywa. |
Ada ya ziada | Malipo ya ziada ya kifedha juu ya bei ya soko, malipo ya ziada kwa ubora, au tofauti nyingine, yanayolipwa kwa Mmiliki wa Cheti cha Shamba na wanunuzi wa kiasi kilichothibitishwa na wanunuzi wa kiasi kilichothibitishwa chini ya Uzalishaji Endelevu wa Kilimo wa shirika la Rainforest Alliance na/au Kilimo cha kuzalisha upya. |
Afya na usalama | Sheria, kanuni, taratibu, misingi, na miongozo inayohusu usalama, afya, na ustawi wa wafanyakazi ili kuzuia ajali au majeraha katika maeneo ya kazi au mazingira ya umma. Hii pia inajulikana kama afya na usalama kazini (OHS) na afya na usalama nje ya kazi kwa ajili ya usalama wa shughuli za ndani na je ya kazi. |
Afya na Usalama Kazini (OHS) | Masuala ya afya, usalama na ustawi mahali pa kazi, yanayolenga kuboresha mazingira ya kazi kwa mfanyakazi/mwajiriwa na wadau wengine. Kuna msisitizo mkubwa juu ya kinga ya kinga ya awali ya hatari. Afya na usalama kazini (OHS) inaweza kujumuisha sheria, viwango, programu, na programu za hiari. |
Afya ya mfumo ikolojia | Ustawi wa jumla, uwiano wa kiutendaji na uadilifu wa mazingira asilia. Mfumo ikolojia wenye afya ni ule unaotekeleza kwa ufanisi michakato yake ya asili, kama vile usafishaji wa maji, uchavushaji, na mzunguko wa virutubisho, na unaoweza kustahimili misukosuko. |
Aina ya mmea stahimilivu | Mmea unaoweza kustahimili wadudu, magonjwa, au vichocheo vya mazingira bila kupungua kwa kiasi kikubwa kwa mavuno au ubora, hata ikiwa mdudu au kisababishi cha ugonjwa bado kipo ndani ya mmea au shambani. Ingawa uharibifu fulani unaweza kutokea, mmea huendelea kufanya kazi vizuri, na hivyo kuchangia usimamizi endelevu wa mazao na kupunguza utegemezi wa matumizi ya kemikali za kudhibiti wadudu na magonjwa. |
Aina ya mmea sugu | Mimea yenye uwezo wa kustahimili, kuzuia au kufukuza wadudu na magonjwa, hivyo kuzuia visisababishe uharibifu. Aina zinazostahimili hupunguza hitaji la matumizi ya kemikali za kudhibiti wadudu.[1] |
Aina ya ufuatiliaji wa bidhaa | Njia inayotumika kushughulikia kiasi kilichoidhinishwa na kufuatilia chanzo chake, kwa mfano: uwiano wa wingi, utenganishaji, na uhifadhi wa utambulisho wa bidhaa. |
Ajira ya Watoto | Kazi inayowanyima watoto utoto wao, uwezo wao wa maendeleo, na heshima yao kibinadamu, na ambayo ni hatari na yenye madhara kwa watoto kiakili, kimwili, kijamii, au kimaadili. Inajumuisha kazi inayovuruga masomo yao kwa kuwanyima fursa ya kuhudhuria shule au kuwalazimisha kuacha shule mapema; au kuwalazimu kujaribu kuchanganya kuhudhuria shule na kufanya kazi nzito na kwa muda mrefu kupindukia.[2] Hii inajumuisha:
Tafadhali angalia mchoro hapa chini kuhusu vikwazo vya umri kati ya kazi ya watoto na ajira ya watoto.
Mchoro 1. Kuonyesha tofauti za umri katika kazi ya watoto, Ajira ya Watoto na Aina Mbaya Zaidi za Ajira ya Watoto.[6] Kumbuka: Nambari zilizo kwenye mabano ni umri wa chini zaidi unaoruhusiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kwa nchi wanachama ambazo uchumi na miundombinu ya elimu yake haijakua vya kutosha. |
Alama ya eneo | Jozi ya viwainishi vya latitudo na longitudo vinavyokusanywa kupitia Takwimu za Mfumo ya Taarifa za Kijiografia (GIS). Sehemu ya mahali ni nukta moja ya data. Inaweza kutumika kuwakilisha eneo la shamba/kitengo cha shamba pale ambapo taarifa za mipaka (poligoni) hazipatikani. |
Athari za kiuchumi za wadudu waharibifu/magonjwa | Kiwango cha athari za kiuchumi zinazoweza kutokea na zile halisi zinazotokana na kuingia, kuanza kujitokeza, au kuenea kwa mdudu mharibifu au ugonjwa katika eneo maalum.na yaliyopo yanayotokana na kuanzishwa, kuimarika, au kuenea kwa mdudu/ugonjwa katika eneo maalum. Hii inajumuisha kupungua kwa mavuno na tija ya mazao, ongezeko la gharama za uzalishaji kutokana na hatua za ziada za udhibiti, vikwazo vya upatikanaji wa masoko, vizuizi vya biashara, na uharibifu wa mazingira unaoathiri tija na faida ya kilimo.[7] |
B
Baada ya mavuno | Hatua ya uzalishaji wa mazao inayofuata mara moja baada ya mavuno. Hii inaweza kujumuisha ushughulikiaji, usafishaji, uhifadhi, upangaji, uchakataji, ufungashaji, na usafirishaji. |
Bei ya soko | Bei ya kawaida inayolipiwa bidhaa yenye ubora na asili sawa, iliyotengenezwa kwa njia za kawaida (yaani, isiyo na cheti cha uthibitishaji). |
Bidhaa iliyopotea | Bidhaa iliyoharibika kiasi kwamba haiwezi tena kuuzwa. |
Bidhaa iliyothibitishwa | Bidhaa au viambato vinavyotoka kwenye Shamba lililothibitishwa na kupitishwa kwenye Mnyororo wa Ugavi uliothibitishwa (pasipo kuzingatia iwapo bidhaa hiyo inauzwa jinsi ilivyothibitishwa au imejumuishwa katika madai ya uthibitishaji). |
Bidhaa ya mwisho kwa mtumiaji | Bidhaa yenye lebo ya cheti cha shirika la Rainforest Alliance, ambayo iko tayari kwa matumizi na haihitaji mabadiliko zaidi kwa upande wa usindikaji au ufungashaji. |
Bidhaa ya ziada | Ni mazao ya ziada yanayopatikana wakati wa uzalishaji, uchakataji, au usambazaji wa bidhaa za kilimo, lakini sio bidhaa kuu iliyokusudiwa.[8] |
Bioanuwai | Aina mbalimbali za viumbe hai, ikiwa ni pamoja na mimea, wanyama, fangasi, vijidudu, pamoja na kazi zao na mwingiliano wao, ambao huchangia huduma za mfumo wa ikolojia, afya, uthabiti na ustahimilivu.[9] |
D
Data ya mahali | Data inayotambulisha kijiografia zilipo mashamba na mipaka ya mashamba, vitengo vya mashamba, na miundombinu mingine ya Wamiliki wa Vyeti. Data ya mahali kijiografia huwakilishwa kwa viwianishi vinavyokusanywa kwa kawaida kupitia mifumo ya kijiografia ya uwekaji nafasi (GPS), kwa kutumia ramani za alama binafsi za eneo (ikiwa ni pamoja na mipaka yao) au poligoni zinazofafanua mipaka kamili ya eneo husika. |
Dawa ya kuangamiza fangasi | Dutu za kemikali au viumbe vya kibiolojia vilivyoundwa kuzuia, kudhibiti au kuondoa fangasi na mbegu zake kwenye mimea, mazao ya kilimo, vyakula vilivyohifadhiwa, au mimea ya mapambo.[10] |
Dawa ya kuua magugu | Dutu za kemikali au kibiolojia zilizosanifiwa kuharibu au kuzuia ukuaji wa mimea isiyotakikana, kama vile magugu na spishi vamizi, bila kuathiri mazao ya kilimo.[11] |
Dawa ya kuua wadudu | Dutu za kemikali au za kibayolojia zilizoundwa kuzuia, kudhibiti, au kuondoa wadudu na viumbe wengine wa jamii ya athropoda wanaosababisha uharibifu kwa mimea, mazao ya kilimo, vyakula vilivyohifadhiwa, au mimea ya mapambo. Matumizi yao yanalenga kulinda uzalishaji, kupunguza hasara za uzalishaji, kuboresha ubora wa bidhaa, na kuzuia uharibifu.[12] |
Dawa ya kuua wadudu | Kila dutu ya kemikali au ya kibayolojia, au mchanganyiko wa dutu mbalimbali, inayokusudiwa kufukuza, kuangamiza au kudhibiti wadudu waharibifu na spishi zisizotakikana za mimea au wanyama wanaosababisha madhara au kuingilia uzalishaji, usindikaji, uhifadhi, usafirishaji au uuzaji wa chakula na bidhaa za kilimo. Neno hilo pia linajumuisha dutu zinazotumika kama viondoa majani, vikaukishaji au wakala wa kupunguza idadi ya matunda au kuzuia matunda kuanguka mapema. Viuatilifu vinaweza kutumika kwenye mazao kabla au baada ya kuvuna ili kuzuia mazao hayo yasiharibike wakati wa uhifadhi na usafirishaji.[13] |
Dawa ya panya | Hii ni kemikali au dutu za kemikali au kibaolojia zilizoundwa kuzuia, kudhibiti, au kuangamiza panya wanaosababisha uharibifu kwa mimea, mazao ya kilimo, chakula kilichohifadhiwa, au miundombinu husika. Matumizi yao yanalenga kulinda uzalishaji, kupunguza hasara za kiuchumi, kuhakikisha usalama wa chakula, na kuzuia uharibifu kwa mifumo ya uzalishaji na uhifadhi. |
Dharura | Tukio katika mazingira na/au eneo fulani ambalo linaweka hatari ya haraka kwa afya, maisha, riziki, haki za binadamu, mali, au mazingira. |
Dutu hai ya udongo (SOM) | Ni misombo ya kikaboni katika udongo inatokana na mabaki ya mimea na wanyama, viumbe hai, na vifaa vilivyooza. Dutu hai ya udongo (SOM) ni kiashiria muhimu cha kibiolojia cha afya ya udongo, kwa sababu huhimili maisha ya vijidudu, mzunguko wa virutubisho, na utendaji kazi wa jumla wa mfumo wa ikolojia. Pia huonyesha kiasi cha biomasi iliyorejelewa na virutubisho vilivyorejeshwa kwenye udongo, na kwa kawaida huonyeshwa kwa asilimia.[14] |
E
Eneo | Kituo kilichotenganishwa kijiografia kinachomilikiwa na Mmiliki wa Cheti (Shamba au Mnyororo wa Ugavi) ambapo idadi maalum na aina maalum za shughuli hufanyika. |
Eneo la kijiografia | Kundi la nchi kadhaa zilizoainishwa ambazo huamua mipaka ambamo vyeti vya maeneo tofauti vya Wamiliki wa Vyeti vya Mnyororo wa Usambazaji, vinaweza kutolewa. |
Eneo la makazi | Jumla ya eneo la makazi ya wafanyakazi linaotolewa na usimamizi. |
Eneo lililolindwa | Eneo la ardhi lililotangazwa au kuamuliwa na mamlaka husika kuwa eneo lililohifadhiwa kutokana na thamani zake za asili, za kiikolojia na/au za kitamaduni, ili kufanikisha uhifadhi wa muda mrefu wa mazingira asilia pamoja na mali za mfumo wa ikolojia na thamani za kitamaduni. Mifano ni pamoja na mbuga za taifa, hifadhi za wanyamapori, hifadhi za kibiolojia au misitu, hifadhi za kibinafsi, na maeneo ndani ya Hifadhi za Mazingira ya UNESCO (Biosphere Reserves) au Maeneo ya Urithi wa Dunia. Uzalishaji unaweza kuruhusiwa katika eneo lililohifadhiwa chini ya sheria husika, na hilo linaweza kujumuisha mgawanyo maalum wa maeneo ndani ya mpango wa usimamizi (maeneo ya matumizi mengi), aina fulani ya maeneo yaliyohifadhiwa (vipengele V na VI vya IUCN), au vibali (kwa mfano, mashamba yaliyoruhusiwa). |
Eneo lisilotumika | Eneo ambalo hakuna viuatilifu vinavyotumika. Umbali kwa mita unaonyesha upana wa eneo lisilotumika viuatilifu na hutegemea njia inayotumika kupulizia dawa, kama ifuatavyo:
|
Eneo tamba | Maeneo yanayozunguka eneo maalum lililolindwa, yaliyotambuliwa na mamlaka husika, ambapo vikwazo vya matumizi ya rasilimali na/au hatua maalum za maendeleo huchukuliwa na mamlaka ili kuimarisha thamani ya uhifadhi wa eneo hilo lililolindwa. |
G
Gesi chafuzi (GHGs) | Mchanganyiko wa gesi zinazohifadhi joto au mionzi ya mawimbi marefu katika angahewa. Uwepo wao katika angahewa hufanya uso wa Dunia kuwa na joto zaidi. Shughuli za binadamu ndizo chanzo kikuu cha gesi chafu. Uchomaji wa nishati ya kisukuku, ukataji miti, ufugaji wa mifugo kwa wingi, matumizi ya mbolea za kemikali, na michakato ya viwandani vyote vinachangia. |
H
Haki tano ya ustawi wa wanyama | Kanuni ya kuhakikisha ustawi wa wanyama kwa kutimiza masharti yafuatayo matano:
|
Haki za binadamu | Haki za kimsingi za binadamu zipo kwa kila mtu kwa sababu tu yeye ni binadamu - hazitolewi na serikali yoyote. Haki hizi za wote ni za asili kwa wanadamu wote, pasipo kujali utaifa, jinsia, kabila, asili, rangi, dini, lugha, au hali nyingine yoyote. |
Haki za kazi/ Haki za wafanyakazi | Haki na ulinzi unaotolewa kwa wafanyakazi mahali pa kazi ili kuhakikisha wanafanya kazi katika mazingira ya haki, salama na yenye staha. Haki hizi zimesanifiwa kulinda watu binafsi dhidi ya unyonyaji, ubaguzi, na mazingira hatarishi ya kazi, huku pia zikihakikisha wanapata malipo ya haki na uwezo wa kuandaa au kuunda vyama vya wafanyakazi.[16] |
Haki za watumiaji zilizoidhinishwa na kutambuliwa rasmi | Idhini hutolewa kwa Mmiliki wa Cheti cha Mnyororo wa Ugavi, ili kufanya miamala kwenye mfumo wa ufuatiliaji wa bidhaa kwa niaba ya Mmiliki wa Cheti cha Shamba. |
Hatari | Chanzo kinachoweza kusababisha madhara au athari mbaya kiafya kwa mtu mmoja au watu. Kuna aina tofauti za hatari, zikiwemo 'hatari za kimwili' (kama kuteleza au kujikwaa, moto, kufanya kazi na vitu vya moto, au kutumia vifaa visivyotunzwa vizuri) au 'hatari za kiafya' (kama kelele, mtetemo, viwango visivyofaa vya mwanga, vumbi hatari, au msongo wa mawazo) au 'hatari za kemikali' (kama kufanya kazi na bidhaa za viambatanishi vya kusafisha, gundi, hadi viuatilifu). |
Hatari | Uwezekano wa kutokea kwa hali inayoweza kuwa hatarishi, unaopimwa kwa kuchanganya uwezekano wa tukio na ukali wa matokeo yake.[17] |
Hatari inayokaribia | Hali, mazingira, au mazoea yoyote ambayo yanaweza kutarajiwa kusababisha kifo au madhara makubwa ya kimwili, iwe mara moja au kabla tishio hilo kuondolewa. |
Hatari kubwa | Hatari yenye uwezekano mkubwa wa kutokea na athari zake kubwa kwa malengo yaliyopo. Aina hii ya hatari inahitaji umakini maalum na usimamizi wa kipekee kutokana na uwezo wake wa kusababisha madhara makubwa au kuvuruga utekelezaji wa malengo. |
Hatari ndogo | Hatari yenye uwezekano mdogo sana wa kutokea na, ikitokea, itakuwa na athari ndogo sana kwa malengo. Aina hii ya hatari mara nyingi huchukuliwa kuwa ndogo sana kiasi cha kupuuzwa, na hivyo haihitaji juhudi kubwa za usimamizi au hatua za kupunguza athari zake.[18] |
Hatua ya kurekebisha | Hatua za kuondoa chanzo (vyanzo) vya kutofikia viwango na kuzuia kujirudia kwake. Hatua za urekebishaji lazima zilenge suluhisho za muda mrefu na endelevu, ambazo huondoa chanzo kikuu cha kutofikia viwango.[19] |
Hatua za kupunguza hatari | Hatua zinazochukuliwa kuzuia matukio hasi yasitokee, na/au kupunguza athari zake iwapo yatatokea.[20] |
Hatua za kupunguza mabadiliko ya tabianchi | Uingiliaji wa binadamu ili kupunguza mabadiliko ya tabianchi kwa kupunguza vyanzo vya utoaji wa gesi chafuzi, au kuongeza hifadhi ya gesi chafuzi (GHGs) katika mazingira.[21] |
Hatua za urekebishaji | Mchanganyiko wa marekebisho na hatua za urekebishaji zinazochukuliwa na Mmiliki wa Cheti ili kuondoa tatizo la kutofikia viwango. |
Hesabu ya nyungunyungu | Mbinu ya kibiolojia inayotumika kutathmini muundo wa udongo, kiwango cha mabaki ya kikaboni na shughuli za viumbe hai, kwa kupima uwepo na wingi wa nyungunyungu katika eneo maalum la udongo.[22] |
I
Idadi ya vijidudu | Kipimo cha kiasi cha uwepo wa mikrobiota ya udongo kinachotumika kama kiashiria cha afya ya udongo. Hutoa taarifa kuhusu shughuli za kibiolojia na uwezo wa udongo wa kusaidia mzunguko wa virutubisho na ukuaji wa mimea.[23] |
J
Jamii | Makundi ya watu wanaoishi katika eneo au mkoa mmoja, wanaoathiriwa na uwepo au uendeshaji wa shamba, kikundicha mashamba, au kampuni. Wafanyakazi wa vijijini, wakazi wa mashamba, majirani, watu wa asili, na wakazi wa vijiji au miji ya karibu wanaweza kuwa jamii zinazoathiriwa na shamba fulani, kikundi cha mashamba, au kampuni fulani. Tazama Watu wa Asili na jamii za wenyeji. |
Jinsia | Sifa za wanawake na wanaume zilizoundwa kijamii, kama vile kanuni, majukumu, na mahusiano ya na kati ya makundi ya wanawake na wanaume. Inatofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine na inaweza kubadilishwa. Ingawa watu wengi huzaliwa wakiwa wanaume au wanawake, hufundishwa kanuni na tabia zinazofaa – ikiwemo jinsi wanavyopaswa kuingiliana na wengine wa jinsia ile ile au tofauti, nyumbani, katika jamii, na mahali pa kazi. Utambulisho wa kijinsia hauzuiliwi tu kwa mwanamume na mwanamke, kwani watu wanaweza kujitambua kama mwanaume na mwanamke kwa pamoja au hakuna kati ya hivi viwili.[24] |
Jinsia | Tofauti za kibiolojia na kifiziolojia kati ya wanaume na wanawake, kama vile viungo vya uzazi, kromosomu, homoni, n.k. Ni ya ulimwengu mzima na mara nyingi haibadiliki, bila upasuaji.[25] |
Jinsia | Haki, majukumu, na fursa sawa za wanawake, wanaume, wasichana, na wavulana. Usawa haumaanishi kwamba wanawake na wanaume watakuwa sawa, bali kwamba haki, majukumu na fursa za wanawake na wanaume hazitategemea jinsia yao. Usawa wa kijinsia unamaanisha kwamba maslahi, mahitaji, na vipaumbele vya wanawake na wanaume vinazingatiwa, kwa kutambua utofauti wa makundi mbalimbali ya wanawake na wanaume. Usawa wa kijinsia sio suala la wanawake pekee, bali linawahusisha na kuwashirikisha kikamilifu wanaume pamoja na wanawake. Usawa kati ya wanawake na wanaume huonekana kama suala la haki za binadamu na pia kama sharti la awali na kiashiria cha maendeleo endelevu yanayomlenga mwanadamu.[26] |
Jukwaa la Ufuatiliaji Bidhaa | Jukwaa la kidijitali la shirika la Rainforest Alliance linalotumika kuripoti miamala na shughuli za kiasi kilichothibitishwa katika mnyororo mzima wa ugavi. |
K
Karatasi ya Takwimu za Usalama wa Nyenzo (MSDS) | Nyaraka inayotoa taarifa muhimu za usalama na afya kazini, kuhusiana na matumizi ya bidhaa/dawa. Hii inaweza kujumuisha, lakini sio tu, maelekezo ya matumizi salama, maelekezo ya kushughulikia bidhaa, vifaa binafsi vya kinga vinavyofaa (PPE), hatari zinazoweza kuhusishwa na nyenzo au bidhaa fulani, pamoja na taratibu za kushughulikia umwagikaji au uvujaji wa dutu. |
Kauli ya shirika la Rainforest Alliance | Rejeleo lolote linalofanywa kuhusu Uthibitishaji wa shirika la Rainforest Alliance au kuhusu upatikanaji wa bidhaa au viambato vilivyoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance. Kauli ya uthibitisho inaweza kutolewa kwenye bidhaa au nje ya bidhaa, na/au kuhusiana na utoaji au uuzaji wa bidhaa. Hii inaweza kuwa kati ya biashara na biashara, na pia kati ya biashara na mtumiaji.[27] |
Kazi nyepesi | Watoto wenye umri wa miaka 12 hadi 15 wanaruhusiwa kufanya kazi ambazo hazidhuru afya na maendeleo yao, na haziingiliani na masomo yao au mafunzo yao. Mtoto lazima awe chini ya usimamizi wa mtu mzima, na muda wa kazi usizidi saa 14 kwa wiki.[28] |
Kazi ya malipo kwa kipande | Kazi ya kulipwa kulingana na idadi ya kazi au vipande vilivyokamilishwa, badala ya muda uliotumiwa kufanya hiyo kazi. |
Kazi ya watoto | Ushiriki wa watoto au vijana katika kazi ambayo haiathiri afya yao na maendeleo yao binafsi au haiingiliani na masomo yao, kwa ujumla huchukuliwa kuwa jambo nzuri. Hii inajumuisha shughuli kama vile kuwasaidia wazazi wao nyumbani, kusaidia katika biashara ya familia au kujipatia pesa za mfukoni nje ya muda wa masomo na wakati wa likizo za shule. Aina hizi za shughuli huchangia katika maendeleo ya watoto na ustawi wa familia zao; huwapatia ujuzi na uzoefu na kuwasaidia kujiandaa kuwa wanajamii wenye tija katika maisha yao ya utu uzima.[29] Hii inajumuisha: Ajira/kazi ya kawaida: Kuanzia umri wa miaka 15 (katika baadhi ya nchi zinazoendelea miaka 14) watoto wanaweza kuanza ajira ya kawaida au kazi isiyozidi saa 48 kwa wiki. Katika nchi ambapo umri wa chini ni mkubwa zaidi au idadi ya saa za kazi zinazoruhusiwa ni ya chini zaidi, umri wa chini uliowekwa kitaifa na idadi ya juu ya saa za kazi zilizowekwa kitaifa hutumika. Kazi za watoto zinapaswa kuwa zisizo hatarishi, ziwe salama, na zinazolingana na umri wao, na zisivuruge elimu ya lazima. Kazi nyepesi: Kazi ambayo haina madhara kwa afya na maendeleo ya mtoto, haiingiliani na masomo au mafunzo yake, inasimamiwa na mtu mzima, na haizidi saa 14 kwa wiki. Kulingana na Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) wa Umri wa Chini wa Kuingia katika Ajira Namba 138, watoto wenye umri wa miaka 12-14 wanaweza kufanya kazi nyepesi katika nchi zenye uchumi unaoendelea. Katika nchi ambako sheria ya kitaifa hairuhusu watoto kufanya kazi nyepesi, umri wa chini wa kitaifa wa kuingia katika ajira hutumika. Kazi ya familia: Kazi za kilimo zinazofanywa na watoto kwenye mashamba madogo ya familia/nyumbani, ambazo zinajumuisha majukumu mepesi na yanayoingiliana na umri wao, na kuwapa fursa ya kukuza ujuzi, hazihesabiwi `kuwa ajira ya watoto mradi shughuli hizo hazina madhara kwa afya na maendeleo yao, haziingiliani na masomo yao, na zinafanyika chini ya usimamizi wa mtu mzima.vurugi masomo, na ziko chini ya usimamizi wa mtu mzima. |
Kazi ya ziada | Muda wa kazi unaofanywa zaidi ya saa za kawaida za kazi. |
Kazi za nyumbani | Kazi inayofanywa ndani ya kaya moja au kwa ajili ya kaya moja au zaidi. Kazi na majukumu yanayochukuliwa kuwa kazi za nyumbani hutofautiana kati ya nchi; yanaweza kujumuisha kupika, kusafisha, kuwatunza watoto, wazee na watu wenye ulemavu, kutunza bustani au wanyama wa kufugwa, au kuendesha gari la familia. Kazi ya watoto katika kazi za nyumbani inahusisha hali ambapo kazi za nyumbani hufanywa na watoto walio chini ya umri wa chini unaoruhusiwa kisheria kufanya kazi husika, au katika mazingira hatarishi, au katika hali zinazofanana na utumwa.[30] |
Kemikali za kilimo | Dutu za kemikali ambazo kwa kawaida huzalishwa kibiashara viwandani, na ambazo hutumika katika uzalishaji wa kilimo, kama vile mbolea, viuatilifu, vidhibiti vya ukuaji mimea, dawa za kuua nematodi na viboreshaji vya udongo. Kemikali za kilimo zinadhibitiwa kwa sababu ya hatari ya athari zao kuwa kwa afya ya binadamu na mazingira.[31] |
Kesi iliyorekebishwa | Kesi iliyothibitishwa ya ajira ya watoto, kazi ya kulazimishwa, ubaguzi, na/au ukatili na unyanyasaji kazini, ambayo imerekebishwa kulingana na Itifaki ya Urekebishaji ya shirika la Rainforest Alliance. |
Kesi iliyoripotiwa | Malalamiko yanayohusiana na ajira ya watoto, kazi ya kulazimishwa, ubaguzi na/au ukatili na unyanyasaji kazini, yaliyowasilishwa katika mifumo wa malalamiko na kunakiliwa na Kamati ya Malalamiko. |
Kesi iliyothibitishwa | Kesi ambayo imethibitishwa kupitia uchunguzi wa awali kwa kutumia ushahidi wa wazi na unaoweza kuthibitishwa, ikiwa ni pamoja na ushuhuda, nyaraka, na/au ripoti kutoka vyanzo vya kuaminika, na kusababisha hitimisho kwamba tukio hilo limetokea. Itifaki ya Urekebishaji ya shirika la Rainforest Alliance inahitaji kwamba kesi iliyothibitishwa lazima ifuatiwe na uchunguzi wa kina. |
Kiambato tendaji | Dutu au mchanganyiko wa dutu zilizomo katika bidhaa ya kiuatilifu iliyo na nguvu za kuangamiza, kufukuza, kuvuta, kupunguza nguvu za au kudhibiti mdudu. Vitu vingine visivyo hai vinaweza ongeza athari hii moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Majina ya viambato tendaji huonyeshwa kwenye lebo ya bidhaa ya kiuatilifu.[32] |
Kiashiria | Kigezo cha kiasi au ubora au kipimo kinachochunguzwa, na ambacho kinatoa njia ya kufuatilia na kuelewa mabadiliko na utendaji unaohusiana na mpango, wateja wake, au vyote viwili[33]. |
Kigezo cha Mshahara wa Kujikimu Kimaisha | Makadirio ya mshahara wa kujikimu kimaisha kwa kipindi maalum, eneo na/au mazao. [34] |
Kilimo cha uzalishaji upya | Njia ya kilimo kamilifu na inayozingatia mfumo mzima, inayotumia kanuni za kilimo-kiikolojia ili kuongeza ustahimilivu wa mazao, kurejesha afya ya udongo, kuimarisha bioanuwai, kuboresha mizunguko ya maji na kunasa kaboni. Shughuli hizi zinahimili maisha thabiti na kuchangia ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.[35] |
Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabianchi | Mchanganyiko wa mbinu mbalimbali endelevu zinazotumika kukabiliana na changamoto mahususi za mabadiliko ya tabianchi katika jamii maalum ya wakulima. Inajumuisha nguzo tatu kuu:
|
Kilimo mseto cha miti na mazao | Mbinu za usimamizi wa ardhi zinazojumuisha kwa makusudi mimea ya kudumu yenye matawi magumu (miti, vichaka, mitende, n.k.) na mazao ya kilimo au mifugo kwenye ardhi ile ile. Mfumo huu wa utofauti wa uzalishaji una manufaa mengi, ikiwa ni pamoja na ongezeko la uzalishaji, uboreshaji wa afya ya udongo, kuimarika kwa bioanuwai, ustahimilivu wa mabadiliko ya tabianchi, na michango katika uhifadhi wa maji na ufyonzaji wa kaboni.[37] |
Kima cha chini cha mshahara | Kiwango cha chini kabisa cha malipo ambacho mwajiri anapaswa kuwalipa wafanyakazi kwa kazi iliyofanywa katika kipindi fulani, ambacho hakiwezi kupunguzwa kwa makubaliano ya pamoja au mkataba wa mtu binafsi. |
Kipande cha shamba | Kipande cha ardhi endelevu chenye muundo unaofanana na mipaka iliyoainishwa, ambasho ni sehemu ya shamba. Shamba linaweza kujumuisha vitengo vya kilimo pamoja na vitengo visivyo vya kilimo. Vitengo vya shamba vinaweza kujumuisha mazao yaliyoidhinishwa, mazao mengine, miundombinu ya majengo, maeneo ya uhifadhi, n.k. Ndani ya mipaka ya kizio cha shamba kunaweza kuwa na vipengele kama vile mimea ya asili, vyanzo vya maji, miongoni mwa vingine.
Mchoro 2. Mchoro wa vitengo vya shamba. |
Kipengele cha data | Ni taarifa au thamani mahususi inayohusishwa na kiashiria na inayohitajika kukusanywa na au kwa niaba ya Mmiliki wa Cheti na/au mkulima kwa ajili ya uchambuzi. |
Kipindi kabla ya kuvuna | Muda kati ya matumizi ya mwisho ya kiuatilifu na wakati uvunaji wa mazao yaliyotibiwa au katika eneo lililotibiwa, unaoruhusiwa. Kipindi hiki hutofautiana kulingana na kiuatilifu kilichotumika. |
Kiumbe hai kilichobadilishwa vinasaba (GMO) | Kiumbe ambacho nyenzo zake za kijenetiki zimebadilishwa kwa njia isiyotokea kiasili kupitia uzazi na/au mchanganyiko wa kiasili wa vinasaba. |
Kiwango kilichothibitishwa | Kiasi cha mazao, bidhaa au viambato vinavyotokana na mazao yaliyothibitishwa na shirika la Rainforest Alliance, vinavyozalishwa na kuuzwa na Wamiliki wa Vyeti, ambavyo vimehakikiwa na kupata uthibitisho chini ya Mpango wa Uthibitishaji wa shirika la Rainforest Alliance. |
Kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi | Marekebisho ya mbinu na usimamizi wa kilimo ili kupunguza athari hasi ambazo mabadiliko ya tabianchi ya sasa au yanayotarajiwa yanaweza kuwa nazo kwenye mazao, mifumo ya kilimo, mifumo ya ikolojia, na maisha ya watu.[38] |
Kulipiza Kisasi | Kitendo cha mwajiri kumwadhibu mfanyakazi kwa kushiriki katika shughuli iliyolindwa kisheria. Kisasi kinaweza kujumuisha hatua yoyote hasi kazini, kama vile kushushwa cheo, kuadhibiwa, kufukuzwa kazi, kupunguzwa mshahara, au kuhamishiwa kazi au zamu. Hata hivyo, kisasi kinaweza pia kuwa cha hila, kama vile kubadilishwa majukumu ya kazi. |
Kundi | Chama cha wazalishaji waliopangwa ambacho kina Mfumo wa Usimamizi wa Ndani (IMS) wa pamoja na kinathibitishwa kwa pamoja chini ya Kanuni za Uthibitishaji za shirika la Rainforest Alliance. Kundi la wazalishaji waliopangwa linaweza kuundwa katika chama au ushirika, au kusimamiwa na mhusika wa mnyororo wa ugavi (kama vile muuzaji nje ya nchi), au taasisi nyingine. |
Kundi lililo katika mazingira hatarishi | Makundi ya watu ambao wako katika hatari kubwa zaidi ya umaskini na kutengwa kijamii kuliko watu wengine katika jamii. Makundi ya walio wachache kwa misingi ya kabila, watu wa asili, wahamiaji, watu wenye ulemavu, wazee wanaoishi katika upweke na waliotengwa, wanawake na watoto, mara nyingi hukumbana na matatizo yanayoweza kusababisha kutengwa zaidi kijamii, kama vile kiwango cha chini cha elimu na ukosefu wa ajira au ajira zisizokidhi uwezo wao kimahitaji. |
Kuondoa visiki | Kukata shina au kigogo cha mti wa mazao ambacho hakizalishi vizuri hadi kubaki kisiki, ili kuhimiza ukuaji mpya kutoka kwenye mzizi, kwa lengo la kuufufua mti na kuongeza uzalishaji bila kuhitaji kuupanda upya. |
Kupogoa | Shughuli ya msimu au ya kila mwaka ya kuondoa matawi yaliyokufa, yaliyoathirika na magonjwa au yasiyotoa mazao, ili kudhibiti wadudu na magonjwa na/au kudhibiti mzigo wa mazao. |
Kutofuata matakwa | Hakuna utimilifu kamili wa mahitaji katika Viwango vya shirika la Rainforest Alliance.[39] |
M
Maadui wa asili | Viumbe hai wanaopatikana kiasili katika mifumo ya ikolojia, ambao huua, hupunguza uwezo wa kuzaana, au kwa namna nyingine hupunguza idadi ya kiumbe hai mwingine. Ni sehemu muhimu za programu za udhibiti wa wadudu waharibifu na zinajumuisha viumbe wawindaji, vimelea wauaji na vimelea vya magonjwa. Uhifadhi na ongezeko lao husaidia kudumisha uwiano wa kiikolojia na kupunguza haja ya matumizi ya viuatilifu vya kemikali kudhibiti wadudu waharibifu.[40] | ||||||||||
Mabadiliko ya tabianchi | Mabadiliko ya tabianchi yanahusisha mabadiliko makubwa katika halijoto la dunia, kiwango cha mvua, unyevunyevu, mifumo ya upepo na mifumo mingine ya hali ya hewa yanayotokea kwa kipindi cha miongo kadhaa au zaidi. Mabadiliko haya katika mifumo ya hali ya hewa yana athari kubwa kwa hali za kilimo, mazingira, na viwango vya maji ya bahari duniani kote. Mwelekeo wa sasa wa mabadiliko ya tabianchi unahusishwa kwa kiwango kikubwa na shughuli za binadamu, kama vile kuongezeka kwa viwango vya gesi chafuzi, ikiwemo dioksidi kaboni, katika angahewa kutokana na matumizi ya nishati za kisukuku, pamoja na mabadiliko ya matumizi ya ardhi, yakiwemo ukataji miti.[41] | ||||||||||
Maeneo mengi | Shirika ambalo halijumuishi kilimo katika wigo wake wa uthibitishaji katika shirika la Rainforest Alliance, na lina eneo kuu lililotambuliwa ambapo maeneo mawili au zaidi yanafanya kazi chini yake. | ||||||||||
Magugu laini | Mimea inayoota kiasili miongoni mwa mazao (mara nyingi aina ya nyasi au mimea laini), lakini isiyoenea kwa kasi wala kushindana sana na mazao kwa virutubisho, maji, au mwanga wa jua. Hudhibitiwa kwa urahisi kupitia mbinu za Udhibiti Jumuishi wa Magugu, na zinaweza kutoa manufaa ya kiikolojia na kilimo bila kusababisha hasara ya kiuchumi. Manufaa haya ni pamoja na kuboresha muundo wa udongo, kuzuia mmomonyoko wa ardhi, kuvutia wachavushaji na wanyama wanaowinda wadudu waharibifu, na kukandamiza magugu hatari zaidi.[42] | ||||||||||
Maji salama ya kunywa | Maji yenye ubora unaomwezesha binadamu kuyatumia bila kuwepo hatari ya madhara ya papo hapo au ya muda mrefu. Vigezo vya maji salama ya kunywa kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO) ni kama ifuatavyo:
| ||||||||||
Maji taka | Maji machafu na taka ngumu zenye kinyesi. Mtiririko wowote wa maji machafu unaojumuisha maji yanayotoka vyooni huchukuliwa kuwa maji taka, iwe yamechanganywa au hayajachanganywa na maji ya matumizi ya kawaida. | ||||||||||
Maji taka | Maji yoyote ambayo ubora wake umeharibika kutokana na matumizi ya binadamu kwa shughuli za nyumbani, viwandani, kibiashara au kilimo. | ||||||||||
Majitaka kutoka kwa shughuli za uchakataji | Maji ambayo ubora wake umeathiriwa vibaya kutokana na shughuli za uchakataji kama vile viwanda vya kusaga (kwa mfano,vinu vya kahawa kwa njia ya maji, viwanda vya kusaga mafuta ya mawese, na vinu vya miwa), shughuli za uoshaji, au vituo vya kufungasha au kuchakata bidhaa (kama vile viwanda vya juisi au puree). | ||||||||||
Makazi | Makazi yanayotoa ulinzi dhidi ya hali ya kimazingira (kama vile, lakini sio tu, mvua, theluji, upepo, joto, baridi, unyevu, mwangaza wa jua) na pia hutoa ulinzi dhidi ya wawindaji. Makazi salama, safi, na yenye heshima ni kipengele muhimu cha ustawi wa binadamu na haki za wafanyakazi, na yanapaswa kutoa mazingira muafaka ya kuishi kwa kuhusiana na eneo la ujenzi, afya na usafi, pamoja na starehe na heshima. | ||||||||||
Malalamiko | Ni malalamiko au wasiwasi wa mtu yeyote kuhusu vitendo vya mtu mwingine au shirika, au kuhusu kanuni na sera zake, ambazo zimeathiri vibaya mlalamikaji. | ||||||||||
Malazi nje ya eneo la mali | Makazi yanayotumiwa na wafanyakazi wa muda kukaa kwa kipindi chote cha kazi zao, lakini ambayo sio lazima yatolewe na shamba, kwa mfano, kambi rasmi na zisizo rasmi za mahema, au malazi ya pamoja yaliyo karibu na mashamba. | ||||||||||
Mapato ya kujikimu kimaisha | Mapato halisi ya mwaka yanayohitajika kwa familia ili iweze kumudu kiwango cha maisha bora kwa kila mmoja. Vipengele vya kiwango bora cha maisha vinajumuisha chakula, maji, makazi, elimu, huduma za afya, usafiri, mavazi, na mahitaji mengine muhimu, ikiwa ni pamoja na maandalizi ya matukio ya dharura yasiyotarajiwa. Mapato ya kujikimu kimaisha yanatambua kwamba kipato ambacho familia hupata kinaweza kutokana na vyanzo vingi. Kwa mfano, kwa wakulima wadogo, kipato kinaweza kupatikana kupitia biashara zisizo za kilimo na fedha za kutumiwa, pamoja na mauzo ya mazao.[43] | ||||||||||
Mashamba mengi | Mashamba mawili au zaidi yanayomilikiwa au kukodishwa na taasisi moja, ambayo shughuli na mbinu zake za kilimo zinasimamiwa kwa pamoja kutoka kituo kimoja cha usimamizi, bila kujali hali ya utjibitishaji. | ||||||||||
Mavazi ya msingi ya kinga | Mavazi na viatu kwa watu wanaoshughulikia viuatilifu vinajumuisha ovaroli zinazovaliwa juu ya shati lenye mikono mirefu, suruali ndefu, soksi, na viatu imara, glavu zinazostahimili kemikali, ulinzi wa macho (yaani barakoa au miwani ya kinga), na ulinzi wa kupumua (yaani kipumulio). | ||||||||||
Mazao funikizi | Nyasi, mikunde, na mimea mingine inayopandwa ili kusaidia kufunika udongo katika eneo la uzalishaji. Hutoa manufaa mbalimbali kama vile kupunguza mmomonyoko wa udongo, kuongeza mabaki ya kikaboni, kuboresha muundo wa udongo, kuhifadhi unyevu, kufunga nitrojeni, kudhibiti magugu makali na kuimarisha makazi ya viumbe wenye manufaa.[44] | ||||||||||
Mboji | Nyenzo imara, inayofanana na humus, inayotokana na ukuoaji uliodhibitiwa wa vitu vya kikaboni, inayoweza kutumika kama mbolea ya kikaboni kuboresha afya na rutuba ya udongo.[45] | ||||||||||
Mbolea | Kitu cha kemikali au cha asili kinachowekwa moja kwa moja kwenye udongo au majani ya mimea, ambacho hutoa virutubisho muhimu ili kusaidia ukuaji wenye afya wa mimea na kudumisha rutuba ya udongo.[46] | ||||||||||
Mbolea ya asili | Vitu vinavyotokana na mimea au wanyama, vyenye virutubisho vya mimea, na vinavyotumika kama mbolea. Mifano ni pamoja na mboji, samadi, mabaki ya mimea iliyooza kwenye maeneo ya majimaji (peati), na slari.[47] | ||||||||||
Mbolea ya utoaji wa polepole | Aina ya mbolea inayotoa virutubisho hatua kwa hatua kwa muda, badala ya vyote kwa pamoja. Hii husaidia kupunguza upotevu wa virutubisho, kuokoa muda, na kupunguza hitaji la kutumia mbolea mara kwa mara. Baadhi ya mbolea za utoaji wa polepole zinaweza kufunikwa kwa mipaka au kutengenezwa kwa njia maalum ili virutubisho vitolewe polepole kadri mimea inavyovihitaji.[48] | ||||||||||
Mbolea ya viwandani | Tazama mbolea isokaboni | ||||||||||
Mbolea za madini | Dutu zilizotengenezwa na binadamu au za kisintetiki, zinazozalishwa hasa kutokana na misombo ya kemikali na au madini yaliyotengenezwa na binadamu. Hutoa virutubisho muhimu kama vile nitrojeni, fosforasi, na potasiamu moja kwa moja kwa mazao na udongo.[49] | ||||||||||
Mdau wa mnyororo wa ugavi | Shirika lolote linalohusika na bidhaa iliyoidhinishwa kuanzia hatua ya uzalishaji hadi uuzaji wa mwisho. | ||||||||||
Mfanyakazi | Mtu aliyeajiriwa na kampuni, au taasisi yoyote inayohusiana nayo, ambaye yuko chini ya udhibiti na uelekezi wa kampuni kuhusu kazi inayopaswa kufanywa pamoja na namna na mbinu ya utekelezaji wake.[50] | ||||||||||
Mfanyakazi | Mtu anayefanya kazi ya kutumia nguvu kwa malipo ya fedha. Mfanyakazi inajumuisha aina zote za watu wanaofanya kazi bila kujali hali yao ya mkataba, kama vile wa kudumu, wa muda, wa msimu, wahamiaji, wafanyakazi wanaolipwa kwa kipande cha kazi, wenye hati na wasio na hati, pamoja na wale walioajiriwa kupitia mtoa huduma za ajira, watu walioko kwenye mafunzo, wafanyakazi wa usimamizi wa kikundi, ikiwa ni pamoja na wakufunzi kazini na wanagenzi, na pia watu waliokuwa hawapo kwa muda kazini au katika taasisi waliokuwa wakifanya kazi hivi karibuni kutokana na ugonjwa, likizo ya uzazi, likizo ya kawaida, mafunzo, au mgogoro kazini. [51] | ||||||||||
Mfanyakazi asiye wa utawala | Wafanyakazi wanaofanya kazi za nguvu za mwili shambani au katika maeneo mengine ya shamba (kama vile vitalu vya miche, vituo vya usindikaji, vituo vya ununuzi, maghala, n.k.), pamoja na wale wanaofanya kazi kama walinzi, madereva, wafanyakazi wa usafi, wapishi, watumishi wa posta, watunza bustani, na wafanyakazi wa jumla. Haijumuishi wafanyakazi wanaotekeleza kazi zao ofisini, wakaguzi wa ndani, au wale waliopewa mamlaka ya usimamizi mashambani/vituo vya usindikaji, n.k. | ||||||||||
Mfanyakazi kijana | Mtoto aliye na umri unaozidi kiwango cha chini cha kuajiriwa (miaka 15) lakini chini ya umri wa miaka 18, anayefanya kazi zisizo hatarishi na zinazofaa kwa umri wake. Tazama mtoto akifanya kazi. | ||||||||||
Mfanyakazi mhamiaji | Mtu anayehama ndani ya nchi na/au kuvuka mipaka ya kimataifa kwa ajili ya kazi. | ||||||||||
Mfanyakazi wa familia | Mtu (wa jinsia yoyote) anayemsaidia jamaa mwingine wa familia kushughulikia shamba la kilimo au biashara nyingine, mradi tu hahesabiwi kuwa mfanyakazi aliyeajiriwa na pia anajali maslahi ya familia hiyo. Ubadilishanaji wa wafanyakazi (watu wanaofanyiana kazi bila malipo) pia uanjumuishwa katika ufafanuzi huu. | ||||||||||
Mfanyakazi wa kudumu/ mfanyakazi | Mtu aliye na mkataba wa kazi ambao hauna tarehe maalum ya mwisho ya ajira. | ||||||||||
Mfanyakazi wa muda/ mfanyakazi | Mfanyakazi/mwajiriwa mwenye mkataba wa ajira, au anayetarajiwa kufanya kazi kwa kipindi cha chini ya miezi 12. | ||||||||||
Mfumo wa ikolojia wa asili | Mfumo wa ikolojia unaofanana kwa kiasi kikubwa – katika muundo wa spishi, maumbile, na utendaji wa kiikolojia – na ule ambao ungepatikana katika eneo fulani pasipo athari kubwa za kibinadamu. Hii inajumuisha mifumo ya ikolojia inayosimamiwa na binadamu ambapo sehemu kubwa ya muundo, maumbile, na shughuli za kiikolojia wa spishi asilia vipo. Mifumo asili ya ikolojia inajumuisha mifumo yote ya ikolojia asili ya ardhini (ikiwemo misitu ya asili, maeneo ya miti, maeneo ya vichaka, savana, nyanda za nyasi, na páramo) na mifumo yote ya ikolojia asili majini. Mifumo ya ikolojia asili ni pamoja na:
Mifumo ya ikolojia ya asili ambayo imeharibiwa kwa kiasi fulani kutokana na shughuli za kibinadamu au za kiasili (kwa mfano, uvunaji wa rasilimali, moto, mabadiliko ya tabianchi, spishi vamizi, au sababu nyinginezo), lakini ambapo matumizi ya ardhi hayajabadilishwa, na sehemu kubwa ya muundo, mpangilio, na shughuli za spishi hizi za kiikolojia bado vipo, au zinatarajiwa kujirejesha kwa njia ya asili, au kupitia usimamizi wa urejeshaji wa ikolojia.[52] | ||||||||||
Mfumo wa kushughulikia malalamiko | Mchakato unaowawezesha watu binafsi, wafanyakazi/waajiriwa, jamii, na/au mashirika ya asasi ya kiraia (ikiwemo watoa taarifa za siri), kuwasilisha malalamiko yao kuhusu kuathiriwa vibaya na shughuli au uendeshaji maalum wa kilimo au biashara. Mfumo wa kushughulikia malalamiko unaweza kuwa rasmi au usio rasmi, kisheria au usio wa kisheria. Inajumuisha hatua za kuwasilisha malalamiko, kuyashughulikia, kurekebisha athari, na ufuatiliaji. | ||||||||||
Mfumo wa Usimamizi wa Ndani (IMS) | Mfumo wa usimamizi wa ubora ulioandikwa, unaolenga kurahisisha ufanisi wa upangaji na uendeshaji wa kikundi, na kuhakikisha kwamba kikundi na wanachama wake wanazingatia masharti husika ya Viwango vya Shirika la Rainforest Alliance. | ||||||||||
Mhusika | Mtu yeyote, kampuni au shirika lolote linalofanya shughuli zinazohusiana na bidhaa iliyothibitishwa, kuanzia uzalishaji hadi bidhaa ya mwisho, ndani ya wigo wa uthibitishaji.[53] | ||||||||||
Mifumo ya ikolojia ya majini | Vyanzo vya maji yanayotiririka na tulivu na maeneo mengine ya ardhi oevu. Hii inajumuisha: Vyanzo vya maji yanayotirirka na tulivu: Mito yote ya asili, vijito, mabwawa madogo, mabwawa makubwa, maziwa, na lago, pamoja na vijito vya msimu vinayotiririka mfululizo kwa angalau miezi miwili katika kipindi cha miaka mingi, au vinayotiririka kwa vipindi na vina upana wa angalau mita moja. Vijito na mito ambayo imeathiriwa na mkusanyiko wa mashapo, maji yaliyochafuliwa yanayotiririka, mmomonyoko wa kingo za mito, uchafuzi wa joto, au vizuizi vya maji vilivyo chini ya mita moja kwa urefu bado vinachukuliwa kuwa mifumo ya ikolojia ya asili ya majini. Mabwawa ya bandia, mabwawa ya kutibu maji, na mabwawa ya umwagiliaji, hayachukuliwi kuwa mifumo asili ya ikolojia majini, isipokuwa: a) maeneo haya ya maji yamevamiwa na spishi zilizo hatarini kutoweka; na/au b) eneo hilo la maji lilijengwa ili kutoa makazi kwa samaki au wanyamapori. Maeneo mengine ya ardhi uowevu: Ardhi oevu zote zinazotokea kiasili, ambapo hali ya asili ya mzunguko wa maji husababisha mojawapo au zote kati ya hali zifuatazo:
Kwa madhumuni ya Viwango vya shirika la Rainforest Alliance, ifuatayo haichukuliwi kuwa mifumo asili ya ikolojia majini:
a) Maeneo haya ya maji vimevamiwa na spishi zilizo katika hatari ya kutoweka. b) Ardhi oevu hiyo iliundwa na binadamu ili kutoa makazi kwa viumbe wanaishi katika mazingira haya. | ||||||||||
Mikanda ya kijani | Maeneo ya uoto wa mimea yenye miti, vichaka, au mimea ya kudumu iliyopandwa ndani au kuzunguka mandhari za kilimo, ili kutoa manufaa mbalimbali ya kimazingira kama vile kuongeza bioanuwai, kuboresha afya ya udongo (ikiwemo tabianchi ya eneo dogo maalum lililo tofauti na sehemu inayolizingira), kulinda dhidi ya upepo, mafuriko au uchafuzi, na kutumika kama hifadhi za kaboni zinazosaidia kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. | ||||||||||
Mikrobiota (udongo) | Jamii ya vijidudu hai vinavyoishi udongoni, ikiwemo bakteria, fangasi, chachu au virusi. Vijidudu hivi huchangia katika mzunguko wa virutubisho, kuoza kwa mabaki ya viumbe hai, na kuendesha michakato muhimu ya kibiolojia inayoathiri muundo wa udongo, rutuba na afya ya mimea. Katika kilimo, mikrobiota ya udongo ni muhimu kwa kudumisha mifumo ya kilimo yenye tija na ustahimilivu.[54] | ||||||||||
Mimea asilia | Mimea asilia inahusu spishi za mimea za kiasili zinazopatikana katika eneo maalum la kijiografia au mfumo wa ikolojia, na ambayo imezoea kutokana na mageuko kwa mamia au maelfu ya miaka, pasipo mwingilio wa binadamu. Zina jukumu muhimu katika kudumisha uwiano wa mfumo wa ikolojia na bioanuwai.[55] | ||||||||||
Misitu ya asili | Misitu ambayo ni mifumo ya ikolojia ya asili na ina sifa nyingi au nyingi zaidi za msitu wa asili wa eneo husika, ikiwa ni pamoja na muundo wa spishi, mpangilio na utendaji wa kiikolojia. Misitu ya asili inajumuisha:
Misitu ya asili inaweza kupimwa na kubainishwa kwa kutumia mbinu ya High Carbon Stock Approach (HCSA); kwa ujumla, aina za unakili wa matumizi ya ardhi za HCSA—msitu wenye msongamano mkubwa (HDF), msitu wenye msongamano wa kati (MDF), msitu wenye msongamano mdogo (LDF), na ukuaji mpya (YR)—yote huchukuliwa kuwa aina za misitu ya asili.[56] | ||||||||||
Miti inayofunga nitrojeni | Miti yenye uwezo wa kubadilisha nitrojeni ya hewani kuwa aina inayoweza kutumiwa na mimea. Mchakato huu huboresha rutuba ya udongo, husaidia ukuaji wa mimea mingine, na hupunguza haja ya matumizi ya mbolea za viwandani. Mifano ya miti inayofunga nitrojeni ni pamoja na spishi za miti za jamii ya mikunde.[57] | ||||||||||
Miti ya msitu iliyosalia | Miti iliyopo shambani ambayo ilikuwa sehemu ya mfumo asilia wa ikolojia wa eneo hilo na ina thamani kubwa kwa bioanuwai. Kwa kawaida huwa ni miti mikongwe na mikubwa kuliko miti mingine iliyopandwa na kusimamiwa ndani ya mfumo wa kilimo au kilimo-msitu. | ||||||||||
Mkandarasi mdogo | Shirika au mtu binafsi aliyepewa mkataba wa kutekeleza shughuli moja au zaidi mahususi zinazohusiana na bidhaa zilizoidhinishwa, kwa mfano, usindikaji, uhifadhi, ufungashaji, na/au uwekaji lebo kwenye bidhaa. | ||||||||||
Mkataba wa ajira | Makubaliano ya maandishi kati ya mwajiri, kama vile usimamizi wa shamba, usimamizi wa kikundi au usimamizi wa kampuni, na mfanyakazi/mwajiriwa. Mkataba wa ajira unapaswa kujumuisha taarifa kuhusu maelezo ya kazi, saa za kazi, kiwango cha malipo, kanuni za malipo ya kazi za ziada, mafao na makato, likizo ya mwaka yenye malipo, ulinzi dhidi ya kupoteza mshahara katika hali ya ugonjwa, ulemavu au ajali, na notisi ya kusitisha mkataba. | ||||||||||
Mkulima mshirika | Ushirikiano wa kimkataba kati ya wakulima au wamiliki wa ardhi na kampuni, kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa za kibiashara. | ||||||||||
Mkulima wa mgao | Mkulima mpangaji anayelima ardhi ya mmiliki kwa makubaliano ya kupokea sehemu ya mazao au asilimia ya mapato yanayotokana na mauzo ya mazao hayo. | ||||||||||
Mmiliki wa chapa | Mtu binafsi, kampuni au taasisi ya rejareja inayouza bidhaa chini ya jina la chapa lililosajiliwa au lebo. Hii inaweza kujumuisha chapa za kibinafsi/chapa za maduka zinazomilikiwa na kampuni za rejareja. Taasisi hii inaweza kuchakata na kufungasha bidhaa yenyewe au kupitia kampuni nyingine, lakini hiyo ndio inamiliki na kuwajibikia chapa hiyo. | ||||||||||
Mnunuzi wa kwanza | Mwenye Cheti ambaye kisheria anamiliki bidhaa iliyothibitishwa baada ya Mmiliki wa awali wa Cheti cha Shamba. | ||||||||||
Mnyama mwenye uti wa mgongo | Kiumbe kinachotambulika kwa kuwa na uti wa mgongo, ikiwa ni pamoja na mamalia, ndege, reptilia, amfibia, na samaki. | ||||||||||
Mpango wa matumizi ya mbolea | Mpango uliorekodiwa unaotokana na mahitaji ya virutubisho vya mazao na hali ya rutuba ya udongo, unaoainisha aina ya mbolea, muda wa matumizi, mbinu na viwango vya matumizi. Mpango huo huzingatia hali maalum za eneo, kama vile tabianchi, aina ya zao na hali ya udongo, ili kupunguza mtiririko wa virutubisho na uchafuzi wa mazingira. | ||||||||||
Mpango wa usimamizi | Nyaraka iliyotengenezwa na usimamizi inayofafanua malengo na hatua zitakazotekelezwa ili kutimiza Viwango vya shirika la Rainforest Alliance. Hatua hizo zinaweza kujumuisha mbinu za kupunguza hatari, kurekebisha masuala ya haki za binadamu, chati ya mtiririko na taratibu za ufuatiliaji wa bidhaa, na utoaji huduma kwa wafanyakazi na/au wanachama wa kikundi, kama vile mafunzo, usaidizi wa kiufundi, na shughuli za kuongeza ufahamu. Mpango wa Usimamizi unaonyesha maelezo ya hatua zitakazochukuliwa ikiwemo ratiba ya utekelezaji, mara ngapi hatua hizo zitatekelezwa, mtu anayehusika, kundi lengwa, na hali ya utekelezaji wake. | ||||||||||
Mrabaha | Kiasi kinacholipwa kwa shirika la Rainforest Alliance kama yalivyoainishwa katika Ratiba ya Mrabaha ulioambatanishwa na Masharti na Vigezo vya Jumla vya Mkataba wa Leseni wa shirika la Rainforest Alliance, kwa ajili ya matumizi ya Alama za RA au kwa haki ya kununua au kuuza kiasi cha bidhaa zilizoidhinishwa chini ya Kilimo Endelevu na/au Kilimo Rejelevu. | ||||||||||
Msambazaji bihaa | Mtu binafsi, kampuni, au shirika linalotoa au kusambaza bidhaa au huduma kwa mtu mwingine, kampuni au shirika lingine. Wasambazaji bidhaa wana jukumu muhimu katika mnyororo wa ugavi kwa kuhakikisha kuwa malighafi, bidhaa, au huduma muhimu zinapatikana ili kukidhi mahitaji ya wateja wao. | ||||||||||
Mshahara wa Kujikimu | Malipo anayopokea mfanyakazi kwa wiki ya kawaida ya kazi katika eneo fulani, yanayotosha kumwezesha yeye na familia yake kuishi maisha ya hadhi. Vipengele vya kiwango bora cha maisha vinajumuisha chakula, maji, makazi, elimu, huduma za afya, usafiri, mavazi, na mahitaji mengine muhimu, ikiwa ni pamoja na akiba au maandalizi ya matukio ya dharura yasiyotarajiwa.[58] | ||||||||||
Msitu | Ardhi yenye ukubwa wa zaidi ya hekta 0.5 yenye miti yenye urefu wa zaidi ya mita 5 na mwavuli wa miti unaofunika zaidi ya asilimia 10, au miti inayoweza kufikia viwango hivi mahali ilipo. Hii haihusishi ardhi ambayo kwa kiasi kikubwa inatumika kwa kilimo au matumizi mengine ya ardhi. Msitu unajumuisha misitu ya asili na mashamba ya miti. Kwa madhumuni ya kutekeleza minyororo ya usambazaji isioyusisha ukataji miti katika muktadha wa uthibitisho wa shirika la Rainforest Alliance, lengo likiwa kuzuia ubadilishaji wa misitu ya asili.[59] | ||||||||||
Mtaalamu/fundi mwenye umahiri | Mtu mwenye utaalamu wa kitaaluma uliothibitishwa, ujuzi, uzoefu, na vyeti katika eneo maalum la somo au taaluma. Kwa shughuli maalum za kiufundi kama vile kuendesha ndege au droni kwa ajili ya kunyunyizia viuatilifu, mtaalamu/fundi mwenye umahiri ni mtu aliyeidhinishwa au kuthibitishwa na mamlaka husika ya kitaifa. | ||||||||||
Mti wa kivuli | Aina mbalimbali za miti ya kudumu inayotoa kivuli katika eneo la shamba lenye zao lililoidhinishwa. Miti ya kivuli hutoa huduma mbalimbali za mfumo wa ikolojia, kama vile kulinda na kuimarisha bioanuwai, kuongeza rutuba ya udongo, kudhibiti wadudu na magonjwa, kurekebisha hali ya hewa ya eneo husika, kufyonza kaboni, na kuhifadhi maji na udongo. Miti ya kivuli pia inaweza kutoa manufaa ya kiuchumi, kama vile matunda, mbao, au bidhaa nyingine.[60] | ||||||||||
Mtiririko wa maji juu ya ardhi | Maji yanayotiririka juu ya uso wa ardhi badala ya kupenywa ndani ya udongo. Maji ya mvua yanayotiririka yanaweza kubeba udongo, mbolea, na viuatilifu kutoka shambani, hivyo kupunguza rutuba ya udongo na kusababisha uchafuzi wa mito, maziwa au vyanzo vingine vya maji vilivyo karibu.[61] | ||||||||||
Mtoa huduma | Shirika au mtu binafsi aliyepewa mkataba na usimamizi wa shamba au mzalishaji ili kutekeleza kazi maalum zilizo ndani ya wigo wa uthibitishaji wa shirika la Rainforest Alliance, ndani ya mipaka ya kijiografia ya shamba. Kwa mujibu wa ufafanuzi, watoa huduma hawachukui umiliki halali wa bidhaa iliyothibitishwa na shirika la Rainforest Alliance. | ||||||||||
Mtoa huduma za kazi | Shirika, wakala mdogo au mtu binafsi anayetoa huduma za uajiri na upangaji wa wafanyakazi, ikiwemo kusambaza wafanyakazi wa kudumu, wa muda au wa msimu, kwa mashamba au vituo vya uzalishaji. Watoa huduma za kazi wanaweza kuwa katika aina nyingi, iwe ni mashirika yanayolenga faida au yasiyo ya kibiashara. | ||||||||||
Mtoto | Mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka 18.[62] | ||||||||||
Muda wa Kuzuiwa Kuingia Shambani (REI) | Muda mdogo kabisa kinachopaswa kupita baada ya matumizi ya kiuatilifu, kabla ya wafanyakazi kuruhusiwa kuingia tena kwa usalama katika eneo lililotibiwa bila kuvaa mavazi au vifaa vya kujikinga. Muda hutofautiana kulingana na aina ya kiuatilifu, sumu yake, muundo wake, njia ya matumizi, zao husika.[63] | ||||||||||
Mwaka wa kalenda | Kipindi cha miezi 12 mfululizo kuanzia tarehe 1 Januari na kukamilika tarehe 31 Desemba, kulingana na mwaka wa kalenda ya Gregorian. | ||||||||||
Mwakilishi wa mwanachama wa kikundi | Mwanachama wa kikundi aliyechaguliwa au kuteuliwa kutenda au kuzungumza kwa niaba ya wanachama wengine wa kikundi. | ||||||||||
Mwakilishi wa usimamizi | Mtu mwenye mamlaka ya kufanya maamuzi aliyeteuliwa na uongozi kushiriki katika kamati, kuwajibika na kusaidia utekelezaji wa mada kuhusiana na masuala ya haki za binadamu na utaratibu wa kushughulikia malalamiko. | ||||||||||
Mwakilishi wa wafanyakazi | Watu wanaotambuliwa hivyo chini ya sheria za kitaifa au utaratibu wa kampuni, iwe wao ni:
| ||||||||||
Mwamuzi | Mhusika yeyote anayefanya biashara (kununua na kuuza) na/au kushughulikia bidhaa zilizoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance, kwa niaba ya shamba au Mmiliki wa Cheti cha Mnyororo wa Ugavi. Mifano ya kawaida ya wapatanishi katika minyororo ya ugavi iliyoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance, ni wafanyabiashara wadogo kama vile "pisteurs" nchini Côte d'Ivoire au "manavs" nchini Uturuki, ambao hununua bidhaa zao kutoka kwa wazalishaji, ili kuwasilisha kwa Mmiliki wa Cheti cha Shamba. Wanaposhughulikia viwango vidogo vya mazao, shirika la Rainforest Alliance halihitaji wapatanishi kuwa na vyeti huru au kusajiliwa kwenye majukwaa ya mifumo ya shirika ka Rainforest Alliance. Hata hivyo, wanapaswa kuzingatia masharti husika ya Viwango vya shirika la Rainforest Alliance, na usimamizi wa Mmiliki wa Cheti utachukua jukumu la kuhakikisha uzingativu wao. | ||||||||||
Mwanachama wa kundi | Mtayarishaji aliyeidhinishwa kama sehemu ya kikundi. Mtu huyu ndiye mwendeshaji halisi wa shamba (kwa mfano mkulima mdogo au mkulima mshiriki) na hahitaji kuwa mmiliki wa ardhi. | ||||||||||
Mwenye Cheti | Yeyote anayepewa cheti na shirika la Rainforest Alliance. Cheti kinaweza kuwa ni kibali kilichotolewa na shirika la Rainforest Alliance au cheti kilichotolewa na Mamlaka ya Uthibitishaji. Mwenye Cheti yaweza kuwa shamba au mhusika katika mnyororo wa ugavi, au taasisi inayosimamia cheti kwa niaba ya mashamba mengi au wahusika wengi kwenye mnyororo wa ugavi. | ||||||||||
Mzalishaji | Mtu (mwanaume au mwanamke) anayemiliki na/au kuendesha biashara ya kilimo, iwe kibiashara au kwa ajili ya kujikimu mwenyewe au familia yake. | ||||||||||
Mzunguko wa mazao | Utaratibu wa kupanda kwa mzunguko aina mazao ya aina tofauti na familia tofauti za mimea katika misimu kadhaa ya kilimo kwenye shamba lilelile kwa mpangilio ukuaji kwenye shamba moja kwa mpangilio au mlolongo, ili kuvunja mizunguko ya magugu, wadudu na magonjwa, na kudumisha au kuboresha rutuba ya udongo pamoja na kiwango cha mabaki ya kikaboni.[65] |
N
Nishati jadidifu | Nishati inayopatikana kutoka vyanzo ambavyo kwa asili havina kikomo, tofauti na, kwa mfano, nishati ya visukuku, ambayo ina akiba finyu. Vyanzo vya nishati jadidifu ni pamoja na kuni, taka, jotoardhi, upepo, nishati ya fotovoltaiki, na nishati ya jua [66]ya joto. |
Nishati ya visukuku | Rasilimali za nishati zinazowaka lakini haziwezi kurejeshwa upya, zilizoundwa kutokana na viumbe hai vilivyofunikwa na kuathiriwa na joto na shinikizo kwa mamilioni ya miaka, ikiwa ni pamoja na makaa ya mawe, mafuta ya petroli, na gesi asilia.[67] |
Nyumbani | Familia ni kitengo cha kijamii na kiuchumi kinachojumuisha mtu mmoja au zaidi, wanaoishi pamoja kwa kawaida, na kutumia kwa pamoja rasilimali zao kwa maisha ya kila siku. Wanafamilia wanaweza kuwa na uhusiano wa damu au wa ndoa, au wasiwe na uhusiano huo. Wanajumuisha watu wanaoishi kawaida katika makazi hayo, pamoja na wategemezi wanaoishi sehemu zingine kwa muda (kwa mfano, wanafunzi walioko shuleni). Wafanyakazi au watumishi wa ndani ambao kwa kawaida huishi na kushiriki milo na familia hiyo, pia wanaweza kuchukuliwa kuwa sehemu yake. Muundo wa familia unaweza kubadilika na muda kutokana na hali za kijamii, kiuchumi, na kibinafsi. Familia zinaweza kuongozwa na wanaume, wanawake, au watoto, huku wanawake na watoto mara nyingi wakikumbana na hatari kubwa zaidi na changamoto za kiuchumi.[68] |
P
Pasipo ukataji miti | Uzalishaji ambao haukusababisha wala kuchangia ukataji miti. [69] |
Poligoni (maeneo ya kijiografia yenye mipaka) | Mpaka wa kijiografia unaozunguka eneo linalowakilisha shamba/kitengo cha shamba. Poligoni hizo zinaweza kuchorwa kwenye ramani na kupewa msimbo na data muhimu kuhusu shamba (inayoitwa sifa), kama vile kitambulisho cha shamba, ukubwa wa shamba (hekta), eneo la uzalishaji, zao linalolimwa, mmiliki, na hali ya uthibitishaji. |
R
Ridhaa Huru, ya Awali na Yenye Taarifa (FPIC) | Haki ya watu wa kiasili na jamii nyingine za wenyeji, ya kufanya maamuzi huru baada ya kupata taarifa kamili kuhusu matumizi au maendeleo ya ardhi na rasilimali zao. FPIC hutekelezwa kupitia mchakato wa ushiriki unaohusisha makundi yote yanayoathirika, unaofanyika kabla ya kukamilishwa au kutekelezwa kwa mipango yoyote ya maendeleo. Mchakato wa FPIC unahakikisha kuwa jamii hazilazimishwi wala kutishwa; kwamba maamuzi hufikiwa kupitia taasisi au wawakilishi waliochaguliwa na jamii zenyewe; kwamba ridhaa ya jamii hutafutwa na kutolewa kwa hiari kabla ya kuidhinishwa au kuanza kwa shughuli zozote; kwamba jamii hupata taarifa kamili kuhusu wigo wa maendeleo yoyote yanayopendekezwa na athari zake zinazoweza kuwa kwa ardhi zao, mapato yao, na mazingira yao; na kwamba hatimaye chaguo lao la kutoa au kuto kutoa ridhaa huheshimiwa.[70] |
S
Saa za kawaida za kazi | Saa za kawaida za kazi ni idadi ya saa ziadaanazofanya mfanyakazi kulingana na mkataba wake wa ajira wa mfanyakazi/mwajiriwa,ndani ya siku, wiki, mwezi na/au mwaka, bila kujumuisha saa za ziada. |
Shamba | Ardhi yote na miundombinu inayotumika kwa shughuli za uzalishaji na usindikaji wa mazao ya kilimo katika shamba lililo thibitishwa na shirika la Rainforest Alliance. Shamba linaweza kujumuisha vitengo kadhaa vya mashamba vilivyo jirani au vilivyotengana kijiografia ndani ya nchi moja, mradi tu viwe chini ya mamlaka moja ya usimamizi. |
Shamba dogo | Mashamba yote yenye wafanyakazi wa kudumu chini ya 10. Mashamba madogo yanaweza kuthibitishwa moja kwa moja au kama sehemu ya kikundi. |
Shamba kubwa | Shamba zote zilizo na wafanyakazi wa kudumu 10 au zaidi. Mashamba makubwa yanaweza kuthibitishwa kwa kila shamba moja moja au kama kama sehemu ya kikundi. |
Shamba lililothibitishwa | Shamba au kikundi cha mashamba yaliyothibitishwa kufikia Viwango na/au suluhisho lingine lolote la uthibitisho wa Mpango wa Uthibitisho wa shirika la Rainforest Alliance. |
Sheria inayotumika | Sheria za kitaifa na za kimataifa zilizothibitishwa zinazotumika katika muktadha au hali maalum. Sheria za kitaifa zinajumuisha sheria na kanuni za mamlaka zote ndani ya taifa (za mitaa, za kikanda, na za kitaifa). Sheria za kimataifa zilizoidhinishwa na mataifa husika, pia zinatambuliwa kuwa sheria zinazotumika.[71] |
Sheria na kanuni zilizopitwa na wakati | Neno hili hutumika kwa sheria ambazo hazitumiki tena kwa sababu ya kupitwa na wakati, iwe kutokana na kuwa sababu ya kuzipitisha haipo, au mada zake hazipo tena, au hazifai tena kwa mazingira yaliyobadilika, au zimepuuzwa kimyakimya na watu wote, japo hazijafutwa rasmi wala kubatilishwa. Uamuzi wowote kwamba kanuni au sheria imepitwa na wakati, lazima upate idhini ya awali kutoka kwa shirika la Rainforest Alliance. |
Shirika la wafanyakazi | Shirika lolote la hiari na huru la wafanyakazi linaloundwa ili kuendeleza na kutetea haki na maslahi yao.[72] |
Spishi vamizi | Aina ya spishi za mmea au mnyama ambazo wanapokuzwa au kuishi sio asili kyake, na ambazo uwepo wake au kuingizwa kwake katika eneo hilo husababisha au kuna uwezekano wa kusababisha madhara ya kiuchumi, kimazingira, au madhara kwa afya ya binadamu. [73] Kwa Viwango vya Shirika la Rainforest Alliance, spishi vamizi ni zile zinazotajwa na Muungano wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Asili IUCN/ Kundi Maalum la Wataalam wa Spishi Vamizi (SSC) chini ya Tume ya Uhai wa Spishi (ISSG), kama Spishi 100 za Kigeni Vamizi Hatari sana Duniani. Spishi za mazao au mifugo hazizingatiwi kuwa spishi vamizi. |
Sumu ya viuatilifu | Uwezo wa kiuatilifu kusababisha athari mbaya kwa viumbe hai, ikiwa ni pamoja na binadamu, wanyama, mimea, au mazingira. Athari hizo zinaweza kujitokeza kama hitilafu za kiutendaji, vidonda vya magonjwa, au kupungua kwa uwezo wa kiumbe hai kukabiliana na vichocheo vya msongo wa mazingira. Ukubwa na aina ya uharibifu hutegemea aina ya kiuatilifu, muundo wake, kipimo kinachotumika, na njia ya mfiduo. Kusumisha, hivyo basi, ni kipengele muhimu katika kutathmini na kupunguza athari za matumizi ya viuatilifu. |
T
Taasisi | Tazama mhusika. |
Taasisi ya Uthibitishaji | Taasisi ya tathmini ya ulinganifu inayotoa uhakikisho huru, na inayofanya kazi kwa kutumia Mpango wa Uthibitishaji wa na iliyoidhinishwa kufanya ukaguzi na kutoa vyeti chini ya Mpango wa Uthibitishaji wa Rainforest Alliance. [74] |
Taka | Kitu au dutu yoyote isiyotakiwa au isiyohitajika. Pia huitwa takataka, taka, uchafu, au vikorokoro, kutegemea aina ya nyenzo na matumizi ya istilahi katika eneo husika. Taka nyingi hujumuisha karatasi, plastiki, metali, kioo, taka za chakula, vitu vya kikaboni, kinyesi, na mbao. Inajumuisha vifaa hatari. Inajumuisha taka za majumbani au za viwandani, bidhaa zilizokataliwa, mabaki ya ujenzi au vifusi, udongo na mawe kutoka kwenye uchimbaji, takataka na udongo unaotokana na usafishaji na utayarishaji wa ardhi. |
Tarehe ya mwisho | Tarehe maalum iliyowekwa na shirika la Rainforest Alliance ambayo baada yake baadhi ya hatua, mbinu au masharti fulani hazikubaliki tena na husababisha kutotimiza viwango maalum. |
Tathmini binafsi | Tathmini ya utimizaji matakwa husika ya Viwango vya shirika la Rainforest Alliance inayofanywa na Mmiliki wa Cheti. Hufanywa kila mwaka na hujumuisha utimizaji wa masharti ya wakandarasi wadogo, watoa huduma, na watoa huduma za ajira (inaphusika). Kwa mashamba makubwa ambayo ni wanachama wa kikundi mchanganyiko, tathmini binafsi inaweza kufanywa kupitia ukaguzi wa ndani unaofanywa na usimamizi wa kundi au kupitia tathmini binafsi inayofanywa na usimamizi wa shamba kubwa husika. Kwa makundi, tathmini binafsi inajumuisha ukaguzi wa ndani wa wanachama wa kundi na tathmini binafsi ya usimamizi wa kundi dhidi ya mahitaji yanayotumika. |
Tathmini na Shughulikia | Mfumo wa usimamizi ambapo Wamiliki wa Vyeti hutambua, hupunguza, na kufuatilia hatari za kuwepo kwa Ajira ya watoto, Ajira ya Kulazimishwa, Ubaguzi, na Dhuluma na Unyanyasaji kazini, na kisha kutatua matatizo yanayotokea. Mbinu hii huchochea wamiliki wa vyeti kujenga uwezo endelevu kwa muda ili kutambua na kushughulikia masuala haya. |
Tathmini ya hatari | Mchakato wa kimfumo wa kubaini na kuchambua masuala yanayoweza kuathiri utiifu kwa masharti ya Viwango vya shirika la Rainforest Alliance na kufanikisha matokeo ya uendelevu yanayotarajiwa. Shirika la Rainforest Alliance limebuni Zana ya Tathmini ya Hatari ili kusaidia uchambuzi huu. |
Tathmini ya Hatari katika Mnyororo wa Ugavi (SCRA) | Sehemu ya mchakato wa usajili unaojumuisha mfululizo wa maswali, ambayo kupitia majibu yake Jukwaa la Uthibitishaji la shirika la Rainforest Alliance, hutathmini hatari zinazoweza kutokea katika shughuli za Mmiliki wa Cheti wa Mnyororo wa Ugavi, ili kubaini aina na mara kwa mara ya uthibitishaji unaohitajika. |
Tathmini ya majani | Tathmini ya majani ya mimea ili kubaini hali yake ya kimaumbile, lishe au mwitikio wake kwa vichocheo vya kimazingira. Tathmini za majani zinaweza kujumuisha ukaguzi wa macho ili kutambua dalili za upungufu wa virutubisho au wadudu na magonjwa, pamoja na uchunguzi wa maabara wa tishu za majani ili kupima viwango vya virutubisho. |
Tathmini ya udongo | Mchakato wa kimfumo wa kuchambua hali ya udongo kwa kuangalia sifa zake kama vile maumbile ya udongo, muundo wa udongo, hidrologia ya udongo, wasifu wa udongo, topografia, viumbe hai vya kikaboni, vipengele vya mimea, na matumizi ya ardhi. Lengo la tathmini ya udongo ni kusaidia uchaguzi wa mazao na hatua za usimamizi wa udongo na maji. |
Thamani ya Juu ya Uhifadhi (HCV) | Thamani za kibayolojia, kiikolojia, kijamii au kitamaduni zinazochukuliwa kuwa na umuhimu wa kipekee au muhimu sana katika ngazi ya kitaifa, kikanda au kimataifa: HCV1: Maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa bioanuwai, ikiwemo spishi za asili za eneo husika, spishi adimu, na spishi zilizo hatarini au zinazokaribia kutoweka, ambazo zina umuhimu mkubwa katika ngazi ya kimataifa, kikanda, au kitaifa. HCV2: Mandhari ya misitu isiyoharibiwa na mifumo mikubwa ya ikolojia, pamoja na mchanganyiko wa mifumo ya ikolojia ambayo ni muhimu katika ngazi ya kimataifa, kikanda au kitaifa, na ambayo ina idadi endelevu ya spishi nyingi zinazopatikana kiasili kwa wingi katika mifumo yao asili. HCV3: Mifumo ya ikolojia, makazi ya viumbe hai, au maeneo ya hifadhi ambayo ni adimu, yamo hatarini, au yanakabiliwa na hatari ya kutoweka. HCV4: Huduma za msingi za mifumo ya ikolojia katika hali za dharura, ikiwemo ulinzi wa maeneo ya vyanzo vya maji na udhibiti wa mmomonyoko wa udongo na miteremko dhaifu. HCV5: Maeneo na rasilimali muhimu kwa kukidhi mahitaji ya msingi ya jamii za wenyeji au watu wa kiasili (kwa maisha, afya, lishe, maji, n.k.), yaliyotambuliwa kupitia ushirikiano na jamii hizo au watu wa asili. HCV6: Maeneo, rasilimali, makazi ya viumbe hai na mandhari yenye umuhimu wa kimataifa au kitaifa, kitamaduni, kiakiolojia au kihistoria, na kiikolojia, kiuchumi au umuhimu wa kidini/takatifu kwa tamaduni za jadi za jamii za wenyeji au watu wa kiasili, yaliyotambuliwa kupitia ushirikiano na jamii hizi au watu wa kiasili.[75] Hati maalum ya mwongozo ya shirika la Rainforest Alliance kwa uhifadhi wa maeneo ya HCV, na mifumo ya ikolojia ya asili inajumuisha fasili za kina zaidi na maelekezo ya kutambua maeneo ya HCV. |
U
Ubadilishaji Mdogo | Kiwango kidogo cha mabadiliko ambacho hakina umuhimu kuambatana na muktadha wa eneo husika, kutokana na udogo wake na kwa sababu hauathiri kwa kiwango kikubwa thamani za uhifadhi wa mifumo ya ikolojia asili, au huduma na thamani zinazotoa kwa watu[76]. |
Ubadilishaji wa (matumizi ya ardhi) | Kubadilisha matumizi au madhumuni ya eneo la ardhi kwenda matumizi mengine ya ardhi, mara nyingi husababisha mabadiliko makubwa katika muundo wa spishi, umbo, au utendaji wa mfumo asilia wa ikolojia. Hii inajumuisha, lakini sio tu kwa, ubadilishaji wa mfumo asilia wa ikolojia kuwa mashamba ya miti ya biashara, mashamba ya kilimo, malisho, hifadhi za maji, miundombinu, uchimbaji madini, na maeneo ya mijini. Ukataji miti ni mojawapo ya ubadilishaji wa matumizi ya ardhi (ubadilishaji wa misitu). Ubadilishaji unahusisha uharibifu mkubwa wa mazingira, au kuanzishwa kwa mbinu za usimamizi zinazosababisha mabadiliko makubwa na ya muda mrefu katika muundo, mpangilio na utendakazi wa awali wa viumbe vya mfumoikolojia. Mabadiliko katika mifumo asilia ya ikolojia yanayoambatana na ufafanuzi huu, huchukuliwa kuwa ubadilishaji, pasipo kuzingatia iwapo ni halali au la.[77] |
Ubaguzi | Tofauti yoyote, ubaguzi au upendeleo unaotokana na misingi ya rangi, ngozi, kabila, jinsia, mwelekeo wa kijinsia, dini, maoni ya kisiasa, asili ya kitaifa au kijamii, na mengineyo ambayo yanasababisha kuondoa au kudhoofisha usawa wa fursa au haki na matendo katika ajira au kazi.[78] Mienendo ya kibaguzi inajumuisha, lakini sio tu, malipo yasiyo sawa kwa kazi sawa, upatikanaji usio sawa wa ajira zenye malipo ya juu na nafasi za usimamizi, vipimo vya lazima vya ujauzito wakati wa kuajiri au wakati wowote katika mchakato wa kazi.[79] |
Ubaguzi wa Kijinsia | Tofauti yoyote, ubaguzi au upendeleo unaofanywa kwa misingi ya jinsia au utambulisho wa kijinsia unaosababisha kubatilishwa au kudhoofishwa kwa usawa wa fursa au matibabu katika ajira au kazi. Hii inajumuisha, lakini haiishii tu kwa ubaguzi dhidi ya wanawake.[80] |
Uchakataji | Mchakato wa kubadilisha kimaumbile bidhaa iliyothibitishwa na kusababisha matokeo tofauti (kwa mfano utengenezaji, uchomaji, uchanganyaji). |
Uchambuzi wa chanzo kikuu cha tatizo | Mbinu ya kubaini sababu za msingi za kutozingatia matakwa au matatizo, ikijumuisha tathmini ya ukubwa wa kiwango cha tatizo ili kubaini ikiwa limetokea mahali pengine.[81] |
Uchunguzi wa kina | Mchakato endelevu wa kudhibiti hatari ambao kampuni inapaswa kuufuata ili kuhakikisha ufuataji sheria na kanuni zote husika, na kuepuka athari mbaya kwa mazingira au haki za binadamu, zinazotokana moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia shughuli zake au zile za mnyororo wake wa ugavi. Uchunguzi wa kina hufanywa kupitia mchakato wa kutambua, kuzuia, kupunguza, na kuelezea jinsi inavyoshughulikia athari mbaya za ukiukaji wa haki za binadamu na za kimazingira zinazotokana na shughuli za kampuni. Inajumuisha hatua nne muhimu: kutathmini athari halisi na zinazoweza kutokea, kuunganisha na kuchukua hatua kulingana na matokeo yaliyopatikana, kufuatilia hatua zilizochukuliwa, na kuwasilisha taarifa kuhusu jinsi athari zinavyoshughulikiwa.[82] |
Udhibiti Shirikishi wa Magugu (IWM) | Mbinu ya usimamizi wa ardhi inayochanganya njia zinazokamilishana za udhibiti wa magugu kama vile malisho ya mifugo, matumizi ya viua magugu, kuacha ardhi kupumzika, udhibiti wa mitambo, na udhibiti wa kibayolojia, ili kupata suluhisho bora zaidi, endelevu na maalum kuambatana na muktadha wa kudhibiti magugu. IWM inalenga kupunguza shinikizo la magugu, kulinda uzalishaji wa mazao, kupunguza athari kwa mazingira, na kukuza uendelevu wa muda mrefu wa mifumo ya ikolojia ya kilimo.[83] |
Uendeshaji wa biashara kwa uwajibikaji | Kuhakikisha ulinzi wa mazingira, watu, na jamii unajumuishwa katika kiini cha mazoea na uendeshaji wa biashara. Uendeshaji wa biashara kwa uwajibikaji unahusisha, zaidi ya yote, kufuata sheria kama vile zile zinazohusu kuheshimu haki za binadamu, ulinzi wa mazingira, mahusiano ya kazi, na uwajibikaji wa kifedha, hata pale ambapo sheria hizi hazitekelezwi ipasavyo kwa njia za kisheria.[84] |
Uendeshaji wa shamba | Mtu au chombo kinachohusika na kupanga na kusimamia shughuli za kilimo na za kiutawala za shamba lililoidhinishwa. Hii inajumuisha Meneja wa Shamba au Msimamizi ambaye ana jukumu la kuhakikisha kwamba mahitaji yote ya Viwango vya shirika la Rainforest Alliance yanatekelezwa. Usimamizi wa shamba unamaanisha chombo kinachohusika na usimamizi, meneja wa shamba, au mwakilishi wa kiufundi anayetekeleza jukumu hili katika mashamba binafsi au mashamba yenye maeneo mengi chini ya mmiliki mmoja. |
Ufunikaji wa uoto wa miti ya asili | Maeneo shambani yanayofunikwa na mwavuli wa miti ya spishi za asili zilizozoea mazingira ya eneo husika. Maeneo haya yanadumishwa au kuanzishwa ili kuchangia ustahimilivu wa mfumo wa ikolojia kwa kulinda udongo, kuongeza uhifadhi wa maji, kusaidia bioanuwai, kudhibiti hali ya hewa ndogo ya eneo husika, na ufyonzaji wa kaboni. Ufunikaji wa uoto wa miti unasimamiwa kwa mujibu wa sheria za kitaifa zinazotumika na ahadi za kimataifa.[85] |
Ufyekaji wa misitu | Ubadilishaji wa misitu asilia kuwa kilimo au matumizi mengine ya ardhi. Uwiano wa Kanuni za Umoja wa Ulaya kuhusu Ukataji na uharibifu wa Misitu: Ubadilishaji wa misitu kuwa matumizi ya kilimo, iwe umesababishwa na binadamu au la, ambayo inajumuisha hali zinazotokana na majanga ya asili (kwa mfano, moto kisha eneo hilo kubadilishwa kuwa ardhi ya kilimo).[86] |
Uharibifu wa mfumo wa ikolojia | Mabadiliko ndani ya mfumo asilia wa ikolojia ambayo yanaathiri vibaya kwa kiasi kikubwa muundo wa spishi zake, umbo na/au utendaji wake, na kupunguza uwezo wa mfumo huo kutoa bidhaa, kusaidia bioanuwai, na/au kutoa huduma za ikolojia.[87] |
Uhifadhi | Ulinzi wa mfumo ikolojia wa asili dhidi ya ubadilishaji au uharibifu wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja unaosababishwa na binadamu. Mifumo ikolojia ya asili inaweza kuhifadhiwa kupitia mchanganyiko wowote wa uhifadhi mkali, urejeshaji, au usimamizi endelevu. |
Uhuishaji wa mazao | Taratibu za utunzaji wa miti ya mazao zinazojumuisha kupogoa au kukata shina ili kuhuisha miti iliyopo bila kuibadilisha. Shughuli hizi kwa kawaida hufanywa kwa mzunguko wa miaka miwili hadi kumi, kwa lengo la kuhuisha baadhi au mashina yote makuu. Kulingana na mzunguko, hutumika kwenye asilimia 10 hadi 50 ya eneo la mazao lililothibitishwa. |
Uhuru wa kujumuika | Haki ya wafanyakazi na waajiri, bila ubaguzi wowote, ya kuanzisha na kujiunga na mashirika wanayochagua wenyewe bila idhini ya awali.[88] |
Uidhinishaji | Uidhinishaji ni kibali kinachotolewa moja kwa moja na Rainforest Alliance kwa Mmiliki wa Cheti cha Mnyororo wa Ugavi ili kujiunga na Mpango wa Uthibitishaji wa shirika hilo. |
Ujira | Malipo au mapato, yaliyotolewa kwa fedha na kuamuliwa kwa makubaliano ya pande zote husika au kwa mujibu wa sheria au kanuni za kitaifa. Ujira hulipwa na mwajiri kwa mfanyakazi/mfanyakazi kwa kazi iliyofanywa au itakayofanywa au kwa huduma zilizotolewa au zitakazotolewa. |
Ukaguzi | Mchakato wa kimfumo, huru na wenye kumbukumbu wa kupata ushahidi na kuutathmini kwa njia isiyo na upendeleo ili kubaini kiwango ambacho masharti ya uthibitisho yametimizwa.[89] |
Ukaguzi wa ghafla | Pia hujulikana kama ukaguzi usio tangazwa, ni ukaguzi unaofanywa bila kutoa taarifa ya awali kwa shirika linalokaguliwa. Aina hii ya ukaguzi husaidia kubaini tofauti au maeneo ya kutofuata matakwa ambayo huenda yasionekane wakati wa ukaguzi wa kawaida unaopangwa mapema. |
Ukaguzi wa kushuhudia | Tathmini ambapo mkaguzi wa Shirika la Uthibitishaji humtazama na kutathmini utendaji wa mkaguzi/wakaguzi wa ndani, ukaguzi wa ndani unapofanyika. Madumuni ya ukaguzi wa kushuhudia ni kuhakikisha kuwa mchakato wa ukaguzi unafanywa kwa umahiri, bila upendeleo, na kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa. [90] |
Ukaguzi wa ndani | Wigo wa shamba: Ukaguzi wa upande wa kwanza au wa pili unaofanywa na mtu mmoja au watu (wakaguzi wa ndani) walioteuliwa na uongozi wa kikundi, unaohakikisha utiifu katika mashamba yote ya wanachama na vitengo vya mashamba vilicyo na masharti yote husika ya Viwango vya shirika la Rainforest Alliance. Wigo wa mnyororo wa ugavi: Ukaguzi wa upande wa kwanza au wa pili unaofanywa na mtu (wakaguzi wa ndani) aliyeteuliwa na usimamizi, unaohakiki utiifu wa masharti ya Viwango vyote vya shirika la Rainforest Alliance, yanayotumika katika taasisi zote zilizo ndani ya wigo wa uthibitishaji. |
Ukaguzi wa nje | Ukaguzi huru unaofanywa na Shirika la Uthibitishaji la upande wa tatu ili kutathmini kiwango cha utiifu wa Wamiliki wa Vyeti kuambatana na Viwango vya shirika la Rainforest Alliance. |
Ukaguzi wa uchunguzi | Ukaguzi usiotangazwa mapema unaoweza kufanywa na shirika la Rainforest Alliance au na Shirika la Uthibitishaji, ili kuthibitisha uzingatiaji wa masharti ya viwango kutokana na malalamiko maalum, tukio lililoripotiwa, au taarifa muhimu kuhusu ulinganifu wa Mmiliki wa Cheti. |
Ukanda wa kinga kando ya mto | Eneo lenye mimea ya kudumu (miti, vichaka, na nyasi) lililoko kando ya kingo za mito, vijito, na vyanzo vingine vya maji, ambapo mazao na mifugo hairuhusiwi kuwepo. Hutumika kama maeneo ya kinga yanayochuja uchafuzi, kuimarisha kingo za mito, kutoa makazi kwa wanyamapori, na kudhibiti joto la maji, hivyo kuimarisha ubora wa maji kwa ujumla.[91] |
Ukarabati wa mazao | Mbinu ya kilimo inayolenga kurejesha au kuboresha afya, uzalishaji, na msongamano wa miti ya mazao. Inahusisha kuondoa kabisa miti ya zamani isiyozalisha katika eneo fulani na kuibadilisha na miti mipya, au kuongeza mimea mipya ndani ya mashamba yaliyopo, au kupanda kwenye ardhi mpya.[92] |
Ukataji Nyasi Kiikolojia | Ukataji wa kimitambo wa mimea ya ardhini kwa mpangilio na kwa wakati unaofaa. Hii hufanywa ili kudhibiti magugu, kukabili ueneaji wa spishi uvamizi, kudumisha utofauti wa mimea na kuepuka mrundikano mkubwa wa biomasi. Kwa kurekebisha muda, marudio na urefu wa kukata nyasi, husaidia kazi za mfumo wa ikolojia kama vile afya ya udongo, makazi ya wachavushaji, udhibiti wa asili wa wadudu waharibifu, na hunapunguza ushindani na mazao.[93] |
Ukatili na Unyanyasaji Mahali pa Kazi | Inahusu aina mbalimbali za tabia na vitendo visivyokubalika, au vitisho vya vitendo hivyo, iwe vinatokea mara moja au kwa kurudiwa, ambavyo vinalenga, husababisha, au vina uwezekano wa kusababisha madhara ya kimwili, kisaikolojia, kijinsia au kiuchumi, na vinajumuisha pia Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia.[94] |
Ukatili wa kijinsia | Ukatili na unyanyasaji unaowalenga watu kwa sababu ya jinsia yao, utambulisho wao kijinsia, au unaowaathiri watu wa jinsia fulani kwa kiwango kikubwa zaidi; unajumuisha unyanyasaji wa kingono. |
Ulinganifu | Uamuzi kwamba mahitaji ya Viwango vya shirika la Rainforest Alliance yametimizwa.[95] |
Umeme | Aina ya nishati inayojumuisha mtiririko wa chaji za umeme, katika muundo ambao ni wa manufaa zaidi kwa kubadilisha nishati na kuwa huduma kama vile taa, kupasha joto, usafiri, na kutoa nguvu kwa mashine.[96] |
Umwagiliaji | Utoaji wa maji kwa njia bandia kwenye udongo au mazao ili kuziba pengo la uhaba wa mvua, na hivyo kuboresha ukuaji wa mimea, na kudumisha uzalishaji wa [97]kilimo. |
Unyanyasaji wa Kijinsia | Tabia ya kijinsi isiyotakiwa na inayomkera anayefanyiwa hivyo. Ili unyanyasaji wa kijinsia uwepo, hali hizi mbili lazima ziwepo: "Quid Pro Quo" ni pale ambapo faida ya kazi – kama vile nyongeza ya mshahara, kupandishwa cheo, au hata kuendelea kubaki kazini – inawekwa masharti ya mhusika kukubali matakwa ya kushiriki katika aina fulani ya tabia ya ngono. Mazingira ya kazi ya uhasama ambapo tabia husababisha hali ya vitisho au udhalalishaji kwa mhusika. Tabia inayofikia vigezo vya unyanyasaji wa kijinsia:
|
Uoto wa asili | Uoto unaoundwa kwa kiasi kikubwa na spishi za asili au zilizozoea mazingira ya eneo husika, unaofanana kwa muundo na mpangilio wa spishi, na uoto unaopatikana au ungepatikana katika mazingira yasiyo na uingiliaji wa binadamu. Uoto wa asili unaweza kusimamiwa (au, katika kesi ya urejeshajaji wa ikolojia, kupandwa) ili kujumuisha sehemu ndogo ya spishi za kigeni, iwapo zina manufaa ya kurejesha ardhi, kurekebisha mfumo wa ikolojia ili uendane na tabianchi ya sasa au ya baadaye, na/au kuimarisha bioanuwai. Ikiwa spishi vamizi zipo, uoto wa asili hudhibitiwa ili kupunguza uwepo wao. |
Upandikizaji | Mbinu ya uzalishaji wa mimea kwa kutumia tishu ambapo tishu za mimea miwili huunganishwa ili zikue pamoja kama mmea mmoja. Upandikizaji hutumika kuchanganya sifa nzuri za mimea tofauti, kwa mfano ili kuboresha ustahimilivu dhidi ya wadudu na magonjwa, kuongeza uzalishaji na kuimarisha uwezo wa kustahimi mabadiliko ya tabianchi.[99] |
Urekebishaji / Suluhisho | Istilahi zinazotumika kwa kubadilishana au kwa pamoja kurejelea mchakato wa kutoa fidia kwa athari hasi, pamoja na matokeo halisi yanayoweza kufidia au kurekebisha athari hizo hasi.[100] Matokeo haya yanaweza kuchukua aina mbalimbali kama vile kuomba radhi, kurejesha haki, urejesho, fidia ya kifedha au isiyo ya kifedha, na adhabu za kinidhamu (iwe za jinai au za kiutawala, kama faini), pamoja na kuzuia madhara kupitia, kwa mfano, amri za mahakama au dhamana za kutorudiwa kwa tukio hilo. |
Urekebishaji wa mazao | Kikundi cha mbinu za kilimo zinazolenga kurejesha au kuboresha uzalishaji, afya na msongamano wa mazao ya miti iliyozeeka, iliyoathiriwa na magonjwa, au isiyotoa mazao bora, bila kuyabadilisha. Inajumuisha upandikizaji, ukataji shina na kupogoa.[101] |
Urekebisho | Hatua za haraka zilizochukuliwa na Mmiliki wa Cheti ili kuondoa tatizo la kutofikia viwango. Mmiliki wa Cheti lazima arekebishe matukio yote ya kutofikia viwango.[102] |
Usafi wa afya, Usafi wa mazingira | Utoaji wa miundombinu na huduma kwa ajili ya utupaji salama wa mkojo na kinyesi cha binadamu. Neno "usafi wa mazingira" pia linahusu utunzaji wa hali ya usafi, kupitia huduma kama vile ukusanyaji wa taka na utupaji wa maji machafu.[103] |
Usafirishaji | Usafirishaji wa bidhaa zilizoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance kutoka kwa Mmiliki Mmoja wa cheti hadi mwingine. |
Usambazaji wa dawa kwa upepo | Kupeperushwa kwa dawa hewani na kutua bila kukusudiwa katika maeneo nje ya eneo lililolengwa. |
Usawa wa kiasi cha bidhaa | Ufuatiliaji wa kiutawala unaomruhusu Mmiliki wa Cheti kudai bidhaa ambayo haijathibitishwa kuwa na kupewa Cheti cha shirika la Rainforest Alliance, endapo kiwango sawa na hicho kimenunuliwa kikiwa kimeidhinishwa na shirika la Rainfrorest Alliance. |
Usimamizi Shirikishi wa Wadudu Waharibifu (IPM) | Tathmini makini na ujumuishaji wa mbinu zote zilizopo za kudhibiti wadudu waharibifu ili kuzuia au kupunguza idadi ya wadudu, huku wakidumisha matumizi ya viuatilifu na hatua nyingine za udhibiti kwa viwango salama kiuchumi, na kupunguza hatari kwa afya ya bianadamu na mazingira. IPM huendeleza ukuaji wa mazao na mifugo yenye afya kwa kuvuruga kidogo mifumo ya ikolojia ya kilimo, huhimiza matumizi ya mifumo asili ya kudhibiti wadudu, na huweka matumizi ya viuatilifu kutegemea ufuatiliaji wa mara kwa mara wa mashambulizi ya wadudu au magonjwa.[104] |
Usimamizi wa kikundi | Taasisi inayohusika na kuandaa na kutekeleza mfumo wa usimamizi wa ndani katika kundi, na kuhakikisha kwamba mashamba ya wanachama yanazingatia Viwango vya shirika la Rainforest Alliance. Usimamizi wa kikundi unamaanisha chombo cha usimamizi kinachohusika, meneja wa kikundi, au mwakilishi wa kiufundi anayetekeleza jukumu hili kwa niaba ya chama cha wazalishaji waliopangwa, kinachopata uthibitisho wa kikundi. |
Usiri | Wajibu wa mtu binafsi au taasisi kujiepusha kushiriki taarifa za siri na wengine, isipokuwa kwa ridhaa ya wazi ya mhusika mwingine, na katika kesi ya mtoto, kwa idhini ya walezi wake. |
Utambulisho Umehifadhiwa | Chaguo la ufuatiliaji ambalo linawezesha kutambua kiungo au bidhaa iliyoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance au kufuatiliwa hadi kwa Mmliki Cheti cha Shamba. Hii ndiyo aina kali zaidi ya ufuatiliaji. Hakuna kuchanganywa kwa kiungo au bidhaa iliyoidhinishwa na kiungo au bidhaa isiyoidhinishwa, au kuchanganywa kati ya vyenyewe. Ikiwa bidhaa iliyoidhinishwa inatoka kwenye vyanzo/mashamba mbalimbali yaliyoidhinishwa, lakini utambulisho wake unalindwa katika mnyororo mzima wa ugavi, aina ndogo ya Mchanganyiko wa Utambulisho Uliolindwa (Mixed IP) inaweza kutumika. |
Utandazaji wa udongo | Mbinu ya kufunika uso wa udongo kwa kutumia vifaa vya asili au visivyo vya asili ili kuhifadhi unyevu wa udongo, kudhibiti joto la udongo, kuzuia ukuaji wa magugu, kuzuia mmomonyoko wa udongo, na kuboresha afya ya udongo, na kuimarisha muundo wake na shughuli za vijidudu vya udongo. Baadhi ya mifano ya matandazo ya asili ni mimea hai au mabaki ya mazao, inayooza, kama vile mabaki ya mazao, majani makavu ya nafaka, majani, mabaki ya nyasi zilizokatwa, au mboji.[105] |
Utenganishaji | Mchakato wa ufuatiliaji ambapo bidhaa iliyothibitishwa huwekwa tofauti na bidhaa isiyothibitishwa, na pia hutenganishwa kati yao, kwa njia ya kimwili na katika nyaraka. Utenganishaji huu hutokea katika hatua zote za kupokea, kuchakata, kufungasha, kuhifadhi, na kusafirisha ndani ya mnyororo wa ugavi. Hakuna kuchanganywa kwa bidhaa isiyoidhinishwa na bidhaa iliyoidhinishwa. Hii inamaanisha kuwa maudhui yote ya bidhaa yamethibitishwa, ingawa yanaweza kutoka katika vyanzo/mashamba tofauti yaliyothibithswa, ikiwa ni pamoja na nchi nyingine za asili ya uzalishaji. |
Uthibitishaji | Ni mchakato wa kuthibitisha, kupitia utoaji wa ushahidi usio na upendeleo, kwamba masharti maalum yametimizwa.[106] |
Uthibitisho | Utambuzi rasmi unaotolewa na Taasisi ya Uthibitishaji kuthibitisha kwamba shamba, kikundi cha mashamba, au wahusika katika mnyororo wa ugavi wanakidhi mahitaji ya Viwango vya shirika la Rainforest Alliance.[107] |
Utumwa wa Kazi | Kazi au huduma yoyote inayohitajika kutoka kwa mtu yeyote chini ya tishio la adhabu yoyote, na ambayo mtu huyo hakujitolea kuifanya kwa hiari yake mwenyewe. Mtu huchukuliwa kuwa katika Kazi ya Kulazimishwa ikiwa anashiriki katika kazi isiyo ya hiari (bila ridhaa huru na yenye taarifa ya mfanyakazi/mwajiriwa) na inayofanywa kwa njia ya vitisho, adhabu, au aina fulani ya kulazimishwa. Aina za kutokuwa na hiari zinaweza kujumuisha, lakini sio tu:
Aina za kulazimishwa zinaweza kujumuisha, lakini haziishii tu kwa:
|
Utumwa wa madeni (kazi ya kulazimishwa) | Hali au mazingira yanayotokana na mdaiwa kutoa ahadi ya huduma zake binafsi au za mtu aliye chini ya udhibiti wake kama dhamana ya deni. Utumwa wa madeni hutokea iwapo thamani ya huduma hizo, kama ilivyokadiriwa kwa haki, haitumiki katika kulipia deni, au muda na aina ya huduma hizo hazijawekewa mipaka na kufafanuliwa. Utumwa wa madeni (pia unajulikana kama kazi ya kulazimishwa kutokana na deni) unaweza kujitokeza kwa njia tofauti. Ni aina ya kazi ya kulazimishwa.[109] |
Uuzaji maradufu | Utaratibu wa kuuza kiasi kilekile cha bidhaa zilizozalishwa au kununuliwa kulingana na uthibitisho wa shirika la Rainforest Alliance, mara mbili; mara moja chini ya Kiwango cha shirika la Rainforest Alliance na tena chini ya Kiwango kingine cha shirika la Rainforest Alliance, mpango mwingine wa uthibitishaji, au kama kawaida. Kwa mfano, tani 100 za kahawa zilizozalishwa na shamba zinaweza kuthibitishwa kuwa za kilimo hai (organic) na pia chini ya Kiwango cha Kilimo Endelevu cha shirika la Rainforest Alliance na kuuzwa kama:
Hata hivyo, kiasi hicho hicho cha kahawa hakiwezi kuuzwa kama tani 100 za kahawa ya kilimo hai, pamoja na pia tani 100 za kahawa iliyothibitishwa chini ya Kiwango cha Kilimo Endelevu cha shirika la Rainforest Alliance au Kilimo cha Urejeshaji. Uuzaji mara mbili hauruhusiwi chini ya kanuni za shirika la Rainforest Alliance. |
Uvukizaji | Mchakato ambao dutu, kama vile kirutubisho kutoka kwenye mbolea (hasa nitrojeni katika mfumo wa amonia au urea) au baadhi ya viuatilifu, hubadilika kuwa gesi na kupotea kwenda angani. Mchakato huu unaweza kupunguza ufanisi wa matumizi ya virutubisho na ufyonzwaji wake na mazao, kupunguza ufanisi viuatilifu, na kuchangia matitizo ya kimazingira kama vile uchafuzi wa hewa, ongezeko la uzalishaji wa gesi chafuzi, na kusambaa kwa kemikali kupitia upepo kwenda maeneo yasiyolengwa.[110] |
Uvunaji endelevu | Mazao yanayovunwa mara kwa mara katika mwaka mzima badala ya msimu maalum ya mavuno. [111] |
Uwezeshaji | Inamaanisha kuwapa watu/jamii maarifa, ujuzi, ujasiri, na rasilimali ili waweze kudhibiti maisha yao na kutetea haki zao. Inahusisha kuondoa vikwazo vya ushiriki, kuangazia suala la ukosefu wa usawa, na kutoa fursa za kufanya maamuzi yenye uelewa.[112] |
Uwindaji | Kumkimbiza na kumuua mnyama kwa ajili ya chakula, michezo, au faida. |
Uzingativu wa jinsia | Kanuni, majukumu, na mahusiano ya kijinsia huzingatiwa, na hatua huchukuliwa kulingana na uelewa huo ili kushughulikia ukosefu wa usawa wa kijinsia na mahitaji maalum ya wanaume na wanawake, kubadilisha matarajio, majukumu, na mahusiano hatari ya kijinsia, na kuhimiza mabadiliko ya nguvu katika mahusiano kati ya wanawake na wanaume. |
V
Viashiria vya afya ya udongo | Sifa zinazopimika za kibiolojia, kikemikali, au kimaumbile za udongo, zinazoonyesha rutuba, tija, na hali yake ya jumla ya kiikolojia. Viashiria hivi husaidia kufuatilia uwezo wa udongo kusaidia ukuaji wa mimea, kudhibiti maji, kuzungusha virutubisho, na kudumisha bioanuwai.[113] | ||||||||||||||||
Viashiria vya vijidudu | Sifa na vipimo vinavyoakisi shughuli, utofauti, au afya ya vijidudu vya udongo. Mifano ni pamoja na biomasi ya vijidudu, shughuli za vimeng'enya, utofauti wa vijidudu, na upumuaji wa udongo. Viashiria hivi hutoa taarifa kuhusu shughuli za kibayolojia udongoni na uboreshaji wake, na hutumika kutathmini rutuba ya udongo, mzunguko wa virutubisho, na athari za mbinu za kilimo. | ||||||||||||||||
Vichocheo vya kibiolojia | Vitu vya asili au viumbe hai, kama vile mboji, samadi, mbolea hai, viuatilifu hai, vichocheo vya vijidudu vya manufaa (bakteria wanaofunga nitrojeni, fangasi wa mykoriza), au dondoo zinazotokana na mimea zinazotumika kuongeza rutuba ya udongo, kusaidia lishe na ukuaji wa mimea, na kudhibiti wadudu na magonjwa kwa njia endelevu kimazingira.[114] | ||||||||||||||||
Vifaa hatari | Nyenzo zinazoweza kuwadhuru watu au mazingira. Hii inajumuisha betri za asidi ya risasi zilizotumika, asbesto, taa za zebaki za kuokoa nishati, taka za kielektroniki, transfoma za umeme zenye POPs (PCBs), vifaa vya matibabu, nyenzo zenye mionzi, viuatilifu, dawa za binadamu na za mifugo zilizopitwa na muda, mafuta yaliyotumika, taka za maambukizi ya kibayolojia, visafishaji, sehemu za miili ya wanyama na mizoga, na chembechembe (majivu, vumbi, mchanganyiko wa viuatilifu vinavypsambaa hewani). | ||||||||||||||||
Vifaa vya Kujikinga Binafsi (PPE) | Mavazi au vifaa vinavyovaliwa ili kupunguza uwezekano wa kuathiriwa na hatari zinazoweza kusababisha ugonjwa au jeraha. Hatari kama hizo zinaweza kujumuisha zile za kemikali, kibiolojia, redioolojia, kimwili, umeme, mitambo, au aina nyingine. Vifaa vya kujikinga binafsi vinaweza kujumuisha vitu kama glavu, miwani na viatu vya usalama, vizibo vya masikio, kofia ngumu, barakoa za kupumua, au ovaroli, fulana za kinga na mavazi ya mwili mzima.[115] | ||||||||||||||||
Vigezo vya maji taka | Vigezo vya shirika la Rainforest Alliance kwa ajili ya utoaji wa maji taka kwenye mifumo ya ikolojia ya majini ni:
Vigezo vya maji taka vya shirika la Rainforest Alliance kwa umwagiliaji ni:
| ||||||||||||||||
Viuatilifu vilivyopitwa na wakati | Viuatilifu ambavyo usajili wake umefutwa, umeondolewa, au umesitishwa, na ambavyo haviwezi tena kutumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa. Kwa hiyo, viuatilifu hivyo vinapaswa kuondolewa kwa njia salama kuambatana na masharti ya udhibiti.[116] | ||||||||||||||||
Viwango vya Juu vya Masalio vinavyoruhusiwa (MRLs) | Kiwango cha juu zaidi kilichowekwa kisheria cha mkusanyiko wa mabaki ya kiuatilifu au kemikali, kinachoruhusiwa kubaki juu au ndani ya bidhaa ya chakula. Viwango vya juu vya masalio (MRLs) hutumika kama viashiria vya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu, kuhakikisha usalama wa watumiaji, kurahisisha biashara ya kimataifa, na kuwasaidia wasimamizi kufuatilia utekelezaji wa kanuni za matumizi ya viuatilifu.[117] | ||||||||||||||||
Viwango vya kikomo | Kiwango cha juu kabisa cha uharibifu (au dalili za uharibifu) unaosababishwa na mdudu au ugonjwa kwenye mmea au katika kundi la mimea, ambacho kinaweza kukubalika kabla ya kuchukua hatua maalum za kudhibiti mdudu au ugonjwa huo. Ikiwa uharibifu utaongezeka, hasara za kiuchumi zitazidi gharama za udhibiti. | ||||||||||||||||
Vizuizi vya mimea | Vizuizi vya mimea vilivyoundwa kupunguza kupeperuka kwa viuatilifu wakati wa unyunyiziaji, na vyenye sifa zifuatazo:
| ||||||||||||||||
Vizuizi vya upepo | Safu za miti au vichaka vinavyopandwa kupunguza kasi ya upepo na kulinda mazao, udongo, au miundombinu ya shamba.[118] | ||||||||||||||||
Vyanzo vya virutubisho vya kikaboni | Nyenzo zinazotokana na viumbe hai au bidhaa zao za ziada zinazotoa virutubisho kwa mazao na kuboresha rutuba na muundo wa udongo. Hizi ni pamoja na mboji, samadi ya wanyama, mabaki ya mazao, na mazao ya kufunika ardhi ambayo hupandwa ili kulinda udongo. Matumizi yake huboresha afya ya udongo kwa muda mrefu na hupunguza utegemezi wa mbolea za kemikali.[119] |
W
Wadudu waharibifu | Spishi yoyote, aina, au biotipu ya mmea (mfano magugu), mnyama (mfano nematoda, wadudu, arthropoda, panya), au kijidudu kinachosababisha magonjwa (mfano fangasi, bakteria, virusi) ambacho kinachoweza kusababisha madhara kwa mimea, bidhaa za mimea, au uzalishaji wa kilimo. Wadudu waharibifu wanaweza kupunguza mavuno, ubora, au uwezo wa mazao kuuzika sokoni na wanaweza kuvuruga uwiano wa kiikolojia, hivyo udhibiti wao ni muhimu katika kilimo endelevu.[120] |
Wafanyakazi wa kikundi | Wafanyakazi wanaofanya kazi kwa kikundi kilichoidhinishwa na shirika la Rainforest Alliance. Hii inajumuisha wafanyakazi wa usimamizi wa kikundi (kama wakaguzi wa ndani na watumishi wa ofisi wanaofanya kazi kwa niaba ya usimamizi wa kikundi), na wafanyakazi katika maeneo makuu ya uzalishaji, usindikaji, na matengenezo. |
Wafanyakazi wa msimu | Tazama wafanyakazi wa muda mfupi. |
Wanyama na mimea iliyo katikahatari ya kutoweka | Spishi zilizotajwa kuwa katika hatari ya kutoweka kwa mujibu wa sheria za kitaifa au mifumo ya uainishaji, na/au zilizoainishwa katika Orodha Nyekundu ya IUCN ya Spishi Zilizo katika hatari ya kutoweka kama zilizo Hatarini Sana, zilizo Hatarini, au zilizo katika Hali ya Hatari, na/au zilizoorodheshwa katika Viambatisho I, II, au III vya Mkataba wa Biashara ya Kimataifa ya Spishi Zilizo Hatarini za Wanyamapori na Mimea (CITES) zilizo katika Hatari ya Kutoweka. |
Wanyamapori | Spishi zote za wanyama wenye uti wa mgongo wanaoishi nchi kavu, isipokuwa wale wanaofugwa na binadamu kama mifugo au wanyama wa kufugwa nyumbani. |
Wanyamapori waharibifu | Aina yoyote ya nymama mwenye uti wa mgongo kutoka katika mifumo ya ikolojia ya asili ambayo husababisha uharibifu kwa mazao, mimea, au bidhaa za mimea. Wanyama hawa waharibifu wanaweza kusababisha kupungua kwa mavuno, kuathiri ubora wa bidhaa, na kuvuruga mifumo ya kilimo, hivyo kuhitaji mikakati ya usimamizi inayosawazisha udhibiti na uhifadhi.[121] |
Watu wa asili na jamii za wenyeji | Makundi tofauti ya watu ambao sifa zao zinaambatana na mojawapo ya fasili zinazokubalika za watu wa kiasili ambazo huzingatia (miongoni mwa masuala mengine) iwapo kundi hilo:[122]
Kwa madhumuni ya Viwango vya shirika la Rainforest Alliance, fasili hii pia inachukuliwa kujumuisha jamii nyingine za wenyeji ambazo sifa zake muhimu zinazofanana na za watu watu wa kiasili, kama vile:
|
Wigo wa cheti | Mkusanyiko wa shughuli, michakato, wahusika, na bidhaa zinazojumuishwa chini ya cheti cha Mmliki wa chetimliki wa Cheti. |
Wigo wa uthibitishaji | Tazama wigo wa uthibitishaji. |
Wigo wa uthibitisho | Mipaka na wigo wa shughuli, michakato, bidhaa, au huduma zinazojumuishwa chini ya Mpango wa Uthibitishaji wa shirika la Rainforest Alliance kuhusiana na Mmiliki maalum wa Cheti. |
Z
Zao lililothibitishwa | Zao ambalo limo kwenye orodha ya mazao yanayoweza kuthibitishwa na Mpango wa Uthibitishaji wa shirika la Rainforest Alliance. Tazama Mazao yaliyothibitishwa na shirika la Rainforest Alliance. |
Zao lililothibitishwa | Zao lolote lililopandwa na kuvunwa na Mmiliki wa Cheti aliyejumuishwa katika wigo wa cheti cha shamba lililothibitishwa na shirika la Rainforest Alliance. |
Zao linalostahimili kivuli | Aina ya zao lililobadilika kimaumbile na kifiziolojia kuweza kukua chini ya kivuli kamili au kivuli cha sehemu. |
Taarifa nyinginezo
Tarehe ya kwanza ya kuchapishwa kwa hati hii (v 1.0): Juni 30, 2020.
Nyaraka zilizotajwa kuwa "zinazofunganisha" lazima zizingatiwe ili kupata uthibitisho. Nyaraka zinazotajwa kama "zisizo funganisha" hutoa taarifa zisizo za lazima ili kuwasaidia wasomaji kuelewa na kutekeleza masharti pamoja na maudhui mengine yanayolazimisha.
Kanusho la Tafsiri
Kwa swali lolote linalohusu na maana sahihi ya taarifa katika tafsiri, wasiliana na toleo rasmi la Kiingereza kwa ufafanuzi. Makosa yoyote au tofauti za maana zinazotokana na tafsiri, hazilazishi na hazina athari kwa madhumuni ya ukaguzi au uthibitisho.
Unakili, urekebishaji, usambazaji, au uchapishaji upya wa maudhui haya ni marufuku kabisa bila idhini ya maandishi ya awali kutoka kwa shirika la Rainforest Alliance.
Taarifa zaidi?
Kwa msaada wa kupata cheti cha shirika la Rainforest Alliance, wasiliana na timu yetu ya Mafanikio ya Wateja kupitia customersuccess@ra.org
Kwa taarifa zaidi kuhusu shirika la Rainforest Alliance, tembelea http://www.rainforest-alliance.org, wasiliana kupitia info@ra.org au Ofisi ya shirika la Rainforest Alliance Amsterdam, De Ruijterkade 6, 1013AA Amsterdam, Uholanzi.
Viambatanisho
Chanzo: Imetoholewa kutoka Kamusi ya Bioteknolojia ya Kilimo ya USDA 2025. ↑
Chanzo: Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO). ↑
Chanzo: Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), kuhusu Matukio Mabaya Zaidi ya Ajira ya Watoto mwaka 1999 (Na. 182). ↑
Chanzo: Kifungu cha 3 cha Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Na. 182 na Kifungu cha 3 cha Pendekezo la ILO Na. 190. ↑
Chanzo: Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) wa Umri wa Chini wa Kazi wa mwaka 1973 (Na. 138). ↑
Chanzo: Zana ya mwongozo ya Shirika la Kazi Duniani ( ILO) na Shirikisho la Waajiri Duniani (IOE) kuhusu ajira ya watoto kwa biashara / Ofisi ya Kimataifa ya Kazi (ILO), Mpango wa Kimataifa wa ILO wa Kurokomeza Ajira ya Watoto; Shirikisho la Kimataifa la Waajiri (IOE) - Geneva: ILO, 2015. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Mfumo wa Uchambuzi wa Hatari za Wadudu Waharibifu, Mkataba wa Kimataifa wa Ulinzi wa Mimea (IPPC) ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka ISO 16559:2014, na kulingana na Shirika la Kulinda Mazingira (EPA). ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Jukwaa la Kimataifa la Sayansi na Sera kuhusu Bioanuwai na Huduma za Mifumo Ikolojia, ipbes 2025. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Chama cha Amerika cha Magonjwa ya Mimea na FAO, 2004. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka FAOTERM-FAO na CADDIS – EPA 2025. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Mwongozo wa Usajili wa Viuatilifu wa FAO 2016 na EPA. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Codex Alimentarius FAO-WHO 2025 na Udhibiti wa wa viuatilifu katika mazingira EPA 2025. ↑
Chanzo: Mabaki Hai ya Udongo, Mwongozo wa Afya ya Udongo USDA-NRCS ↑
Chanzo: Chanzo: Kamati ya Ustawi wa Wanyama (AWC) 2019. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Azimio la Shirika la Kazi Duniani (ILO) kuhusu Kanuni na Haki za Msingi Kazini. ↑
Imetoholewa kutoka Kanuni ya ISEAL ya Mazoea Mzuri kwa Mifumo ya Uendelevu. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka ISO 31000. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka ISO 9000:2015. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka ISO 31000:2009. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka IPCC, 2018: Kiambatisho I: Faharasa katika: Uongezekaji wa Joto Duniani wa nyuzi 1.5°C. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Huduma za Uhifadhi wa Rasilimali Asili (NRCS) USDA 2009. ↑
Chanzo: Vijidudu kama viashiria vya afya ya udongo. Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Mazingira, Denmark. Ripoti ya Kiufundi Na. 388, 2002 ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka UN Women, OSAGI Ujumuishaji wa Jinsia - Dhana na fasili ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka kwa Jinsia, usawa na haki za binadamu: Faharasa ya istilahi na zana za WHO, na Dhana na Tafsiri ya Jinsia, Mshirika wa Chuo Kikuu cha John Hopkins. ↑
Chanzo: UN Women, Ujumuishaji wa Jinsia wa OSAGI - Dhana na fasili. ↑
Chanzo: Imetolewa kutoka Kanuni ya ISEAL ya Mazoea Bora kwa Mifumo ya Uendelevu. ↑
Chanzo: Mkataba wa Umri wa Chini wa Kazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Na. 138 ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) wa Umri wa Chini wa Kuingia katika Ajira (Na. 138). ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Mkataba wa ILO kuhusu Wafanyakazi wa Nyumbani, 2011 (Na. 189). ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka AGROVOC – FAO 2024. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka kwa Kanuni ya Kimataifa ya Maadili ya Usimamizi wa Viuatilifu ya FAO na WHO 2014, na Shirika la Kulinda Mazingira la Marekani (EPA). ↑
Chanzo ISEAL kimetoholewa kutoka OECD Tathmini na Usimamizi unaotegemea Matokeo 2002. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Muungano wa Kimataifa kuhusu Mshahara wa Kujikimu. ↑
Chanzo: Imetolewa kutoka Mitazamo na Programu za USDA 2025. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka IPCC, 2018: Kiambatisho I: Fahirisi [Matthews, J.B.R. (mhariri)] Ndani ya: Uongezekaji wa Joto Duniani wa nyuzi 1.5°C. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Kuhusu Kilimo-misitu FAO 2025. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka IPCC, 2018: Kiambatisho I: Faharasa katika: Uongezekaji wa Joto Duniani wa nyuzi 1.5°C. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka ISO 9000:2005. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Mwongozo wa Natural Enemies Handbook, Chuo Kikuu cha California-Kilimo na Rasilimali Asilia 2019. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka IPCC, 2018: Kiambatisho I: Faharasa katika: Uongezekaji wa Joto Duniani wa nyuzi 1.5°C. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Udhibiti wa wadudu na magugu (USDA) 2025. ↑
Chanzo: Muungano wa Kimataifa wa Mishahara ya Kujikimu. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Mwongozo wa Kiufundi wa USDA-NRCS Taarifa Na. 256-10/2013. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Kanuni ya Kimataifa ya Maadili ya Matumizi Endelevu na Usimamizi wa Mbolea, FAO. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Kanuni ya Kimataifa ya Maadili ya Matumizi Endelevu na Usimamizi wa Mbolea, FAO 2019. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka FAO. ↑
Chanzo: Imetolewa kutoka Mwongozo wa uundaji na matumizi ya vipimo vya FAO na WHO kvya uatilifu (2001) na Huduma ya Misitu ya USDA 2012. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka AGROVOC-FAO, 2022 na Huduma za Istilahi za EPA 2004. ↑
Chanzo: Viwango vya ISO ↑
Chanzo: Mkataba wa ILO wa Mwaka 2019 kuhusu Vurugu na Unyanyasaji (Na. 190). ↑
Chanzo: Istilahi na Ufafanuzi, Mpango wa Mfumo wa Uwajibikaji 2024. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka ISO 9001. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Tovuti ya Udongo ya FAO 2025. ↑
Chanzo: Muungano wa Mandhari ya Kiikolojia 2025. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Mpango wa Mfumo wa Uwajibikaji, Istilahi na Ufafanuzi, 2024. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Kituo cha cha Kilimo Misitu Duniani 2025. ↑
Chanzo: Muungano wa Kimataifa wa Mishahara ya Kujikimu. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Istilahi na Ufafanuzi, Mpango wa Mfumo wa Uwajibikaji 2024, na FRA 2020, FAO. ↑
Chanzo: Imetolewa kutoka kwa Istilahi na Ufafanuzi FRA 2020, FAO. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka AGROVOC FAO 2022. ↑
Chanzo: Kifungu cha 1 cha Makubaliano ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Mtoto (UN CRC). ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Usalama wa Wafanyakazi Wanaoshughulika na Viuatilifu EPA (2025) na Kanuni ya Kimataifa ya Usimamizi wa Viuatilifu FAO - WHO 2020. ↑
Chanzo: Pendekezo la ILO kuhusu Wawakilishi wa Wafanyakazi, 1971 (Na. 143). ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka fasili za IFOAM na FAO. ↑
Chanzo: Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi UNFCCC ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Ripoti ya Mabadiliko ya Tabianchi ya AR4 ya IPCC. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka OECD, Kamusi ya Istilahi za Takwimu, 2008. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Masharti na Fasili, Mpango wa Uwajibikaji (Accountability Framework Initiative) 2024. ↑
Chanzo: Azimio la Haki za Watu wa Kiasili ↑
Chanzo: Istilahi na Ufafanuzi, Mpango wa Mfumo wa Uwajibikaji 2024. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka kwenye ufafanuzi katika Mkataba wa ILO kuhusu Uhuru wa Kujumuika na Ulinzi wa Haki ya Kuunda Vyama, (Mkataba wa ILO kuhusu Vurugu na Unyanyasaji, 2019 (Na. 190) Kifungu cha 10). ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Muungano wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Asili (IUCN). ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka ISO – Uthibitisho. ↑
Chanzo: Mtandao wa HCV ↑
Chanzo: Istilahi na Ufafanuzi wa Mpango wa Mfumo wa Uwajibikaji 2024. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Masharti na Fasili, Mpango wa Uwajibikaji (Accountability Framework Initiative) 2024. ↑
Chanzo: Mkataba wa ILO kuhusu Ubaguzi (Ajira na Kazi), 1958 (Na. 111) ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Mkataba wa Kuondoa Aina Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW). ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kuondoa Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka ISO 9001:2015. ↑
Chanzo: Mfumo wa Kuripoti wa Kanuni Elekezi za Umoja wa Mataifa na Mwongozo wake wa Utekelezaji na Uhakikisho. Shift Project Ltd. © 2015 Shift Project Ltd., © 2015 Forvis Mazars LLP. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Mkusanyiko wa FAO 2025 wa Kuongeza Uzalishaji Endelevu wa Mazao. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka OECD, Mfumo wa Sera za Uwekezaji, 2015. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Tathmini ya Rasilimali za Misitu (FRA 2020) FAO2018- ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Masharti na Fasili za EUDR 2023 na FRA 2020, FAO. ↑
Chanzo: Istilahi na Ufafanuzi, Mpango wa Mfumo wa Uwajibikaji 2024. ↑
Chanzo: Mkataba wa ILO Na. 87 kuhusu Uhuru wa Kujumuika na Ulinzi wa Haki ya Kuunda Mashirika ya Wafanyakazi. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka ISO 9001:2015. ↑
Chanzo: Imetolewa kutoka ISO/IEC 17011:2017. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Riparian Buffers for Agricultural Land USDA-NAC 1997. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Ukarabati na Uhuishaji wa Miti ya Mazao ya Wakulima Wadogo (R&R), IDH-Dalberg 2015. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka FAO / USDA-NRCS 2025. ↑
Chanzo: Mkataba wa ILO Na. 190. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka ISO 9000:2015. ↑
Chanzo: Idara ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii, Kitengo cha Takwimu, Umoja wa Mataifa. ↑
Chanzo: Kamusi ya Kimataifa ya Haidrolojia, WMO/UNESCO, 2011 ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka ILO, Unyanyasaji wa kijinsia katika ulimwengu wa kazi. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka AGROVOC / FAO 2024. ↑
Chanzo: Imetolewa kutoka Kanuni ya ISEAL ya Mazoea Bora kwa Mifumo ya Uendelevu. ↑
Chanzo: Imetolewa kutoka Uboreshaji na ukarabati wa mazao ya miti ya wakulima wadogo, IDH Dahlberg, 2015. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka ISO 9000:2015. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Mada za Afya. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Usimamizi wa Wadudu Waharibifu na Viuatilifu, FAO, na Kanuni za EPA za Usimamizi Shirikishi wa Wadudu (IPM) 2025. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka FAO TECA 2020 na Afya ya Udongo ya USDA. ↑
Chanzo: ISO 9000:2005. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka ISO/IEC 17000:2020. ↑
Chanzo: Mkataba wa Kazi ya Kulazimishwa wa ILO, Itifaki ya ILO ya mwaka 2014 kuhusu Mkataba wa Kazi ya Kulazimishwa wa mwaka 1930. ↑
Chanzo: Istilahi na Ufafanuzi, Mpango wa Mfumo wa Uwajibikaji 2024. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Shirika la Ulinzi wa Mazingira la Marekani (EPA) 2025. ↑
Chanzo: Iliyotoholewa kutoka kwa Mfululizo ya Maendeleo ya Takwimu wa FAO. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Hazina ya Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD). ↑
Chanzo: Imetolewa kutokaViashiria na Tathmini ya Afya ya Udongo Duniani FAO 2025. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka FAOTERM, FAO, 2022 ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO). ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Obsolete pesticide FAO 2025. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Codex Alimentarius FAO – WHO 2024. ↑
Chanzo: Imetolewa kutoka Matumizi ya Vizuizi vya Upepo kwa uhifadhi na kuboresha uzalishaji wa kilimo, NRCS-USDA ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka kwenye kitabu kwa jina Plant Nutrition for Food Security; FAO 2006. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Unoja wa Mataifa (FAO). ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka kitabu Udhibiti wa Wanyama Waharibifu Wenye Uti wa Mgongo na Matumizi ya Kemikali Zake katika Mazingira ya Mijini na Vijijini Mwongozo wa Sumu za Viuatilifu 2001. ↑
Chanzo: Imetoholewa kutoka Mkataba wa ILO Na. 169 kuhusu Watu wa Kiasili na wa Kikabila katika Nchi Huru, Utafiti kuhusu Tatizo la Ubaguzi dhidi ya Idadi ya Watu wa Kiasili, na Waraka wa Kazi wa umoja wa Mataifa kuhusu Dhana ya "Watu wa Kiasili". Idadi ya watu ↑

